Simba SC yampa mapumziko Bernard Morrison hadi mwisho wa msimu huu 2021/ 2022

Simba SC yampa mapumziko Bernard Morrison hadi mwisho wa msimu huu 2021/ 2022

Kipaji cha mchezaji bila nidhamu na jududi ni hasara kwa Klabu

Na usidhani kuwa Klabu imekurupuka tu, huwezi kujua nidhamu mbaya yake kunaigharimu vipi Klabu, ndo maana ameshasimamishwa na kuonywa sana, mchezaji hawezi kucheza game 5 mfululizo bila ya kuwa matatizo uliona wapi hiyo...!?
Uonevu mbona mkude mtukutu miaka tu inakata?
 
Huyo jamaa ni bonge la mchezaji. Narudia tena ni bonge la mchezaji. Ila kichwani kwake anajua mwenyewe kuna nini. Nidhamu mbovu ni hatari sana kwa timu. Nafikiri Simba wameona kuwa:-
1. Anaweza kuambukiza tabia yake mbaya kwa wachezaji wengine.
2. Akiadhibiwa na timu maana yake timu inapungiwa wachezaji hasa ikitokea kuwa wachezaji wanaocheza nafasi yake ni majeruhi au wana kadi.
3. Akifanya utovu wa nidhamu asipoadhibiwa maana yake mchezaji mwingine akifanya kosa kama lake hataadhibiwa mwisho wa siku timu nzima inakuwa na nidhamu mbovu.
4. Akifanya kosa asipoadhibiwa anapunguza morali kwa wenzake na kuona kuwa anapendelewa.
5. .......................................
Yanga alikua hana ujinga huo kabisa
 
Kama nyie tu mlivyolamba matapishi kwa chama na ajib na siku si nyingi mtalamba ya konde boi
Chama hajawahi kuwa kero simba wala kuwa na mgogoro wa kuifanya club imsotee

Ila nyinyi ndio mmekuwa mkishoboka na wachezaji wetu mpaka kufikia hatua kwenye page ya official club inapost picha ya chama akiwa ameeditiwa kavaa jezi ya Uto

Simba haijawahi fika level hizo, yani hata official page ya simba haijawahi kuhusika kupiga vijembe dhidi ya Uto, ila kwa page ya yanga imekuwa ni tofauti
 
Limeandika gazeti la michezo la Mwanaspoti kuhusu mchezaji Bernard Morrison
20220514_113336.jpg
 
"Na safari yake ya soka hapo baadae" sijaelewa hapa..
safari yake ya baadae inaweza kuwa ni Simba pia. Kwamba msimu ukiisha atarejea. Kwahiyo wanamtakia heri arejee kuendelea na majukumu. Tatizo hakuna anayejua makubaliano ya mezani waliongea nini.
 
Kumbe GSM kashafanya yake tayari ndio maana Simba wameondoa kirusi mapema ndani ya kambi yao.

Ni maamuzi mazuri kwa Morson maana msimu ujao kaona hata benchi hatakuwepo Kutokana na ujio wa Luis, Tau na Adebayo
GSM anahusikaje?

Ikumbukwe kuwa mkataba wake wa miaka 2 unaisha msimu huu.

Swali, ni je , bado Simba walikuwa wanamhitaji bado?
 
kama mmeona ile video jinsi BM3 anaagana na wachezaji wenzake utaona ni kwa namna gani jamaa ni mtu poa saana .binafsi nimeumia sana na kuondoka kwa bm3 ,mchango wake katika timu yetu hakika tuliuona. haikua rahisi kufika hata robo fainali ya caf bila mchango wake.mambo ya kinidhamu mbona hata kina Mkude watukutu tu na bado tunaishi nao lakini kwa morison amewashinda kabisa kweli? bm3 hakutakiwa kuondoka kabisa bado tulimuhitaji.halafu cha ajabu utakuta bm3 anaondoka halafu Kina Mugulu wanabaki. uongozi wa simba fanyeni juu chini leteni mtu atakeyeweza kucover nafasi yake bila hivyo mtakua mmefeli katika hili
 
hakika bm3 atabaki kuwa mchezaji aliyejitengenezea historia ya pekee katika soka la bongo. anastahili kuzungumzwa
Historia ya kuwa na Ban Afrika Kusini, kuvua bukta na kubaki na chupi kukimbiza mashabiki wa Uto, kutoroka kambini usiku, kuchagua baadhi ya game..!

Kwa mchango wake Simba SC unatosha sana na kila la kheri aendako.
 
Historia ya kuwa na Ban Afrika Kusini, kuvua bukta na kubaki na chupi kukimbiza mashabiki wa Uto, kutoroka kambini usiku, kuchagua baadhi ya game..!

Kwa mchango wake Simba SC unatosha sana na kila la kheri aendako.
hakika mkuu.
 
ni ngumu sana kujua umuhimu wa mtu ingali bado upo naye
 
Nashangaa wao mpaka leo hatuoni tamko rasmi kuhusu kuachwa kwa golia machachari na imara mwamba RAMADHANI KABWILI[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wee yule shost yupo sana palee, alisema akitoka atawalipua mazima.
 
Back
Top Bottom