Simba SC yamtangaza Sven Vander Broeck kuwa kocha mpya akichukua mikoba ya Patrick Aussems

Simba SC yamtangaza Sven Vander Broeck kuwa kocha mpya akichukua mikoba ya Patrick Aussems

Huyu Sven Ludwig Vandenbroeck alimshinda Kocha wa sasa wa Unganda jonathan mckinstry katika kinyanyang'anyiro cha kugombea kuwa Kocha wa timu ya Taifa ya Zambia.








 
Simba SC ambao ni Mabingwa wa Nchi, leo Desemba 11, 2019, imetangaza Kocha Sven Vander Broeck kuwa kocha mkuu mpya akichukua mikoba ya Patrick Aussems.

Vander Broeck Mbelgiji, amewahi kuifundisha timu ya Taifa ya Zambia pia alishinda ubingwa wa Afrika AFCON akiwa kocha msaidizi katika timu ya Taifa ya Cameroon mwaka 2017.

Klabu ya Simba SC kwenye taarifa yake imesema kwamba, inaamini kocha Sven Vanderbroeck ataleta matokeo chanya na klabu imeahidi kumpa ushirikiano ili kutimiza malengo ya klabu.

This Is Simba SC Next Level.........SimbaNguvuMoja

View attachment 1289085
daaaaa garasaaaaaaa
 
Ndiyo huyu anaitwa "kuku kishingo" ??

Ndo huyo ndugu. Na hapa amelala bado hajaamka mpaka sahzi analalalala kishenzi
tapatalk_1556394582441.jpeg
 
Back
Top Bottom