Simba SC yatinga Robo Fainali Kombe la Dunia kwenye mtandao wa Twitter

Simba SC yatinga Robo Fainali Kombe la Dunia kwenye mtandao wa Twitter

Mributz

Senior Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
177
Reaction score
527
SIMBA SC ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

Klabu ya Simba Sc kutoka Tanzania imetinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia linaloendele kwenye mtandao wa Twitter likiendeshwa na mtandao wa Deportes &Finanzas kutoka Brazil likihusisha vilabu vyenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Kombe Hilo limehusisha vilabu mbalimbali duniani vikowemo vilabu vikubwa kutoka Bara la Ulaya ikiwemo, Real Madrid, Manchester United, Liverpool na linaendeshwa kwa watu kupiga kura kwa kuichagua timu moja wapo kati ya mbili zitakazokutanishwa.

Kutoka Tanzania Simba ndio Timu pekee inayoshiriki Kombe hilo kutoka na kuwa ndiyo klabu yenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii.

Simba ilicheza jana Aprili 12 hatua ya 16 bora dhidi ya Nacional ya Uruguay na kufanikiwa kupata kura Sawa na 65% huku Nacional wakipata 35% hivyo ikafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ambapo itakutana na River Plate ya Argentina.

Michezo mingine ya hatua ya 16 bora inayoendele leo Aprili 13, ni Fenerbahçe dhidi ya Real Mardid na Kerala B. dhidi ya Allianza Lima.
 
SIMBA SC ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

Klabu ya Simba Sc kutoka Tanzania imetinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia linaloendele kwenye mtandao wa Twitter likiendeshwa na mtandao wa Deportes&Finanzas kutoka Brazil likihusisha vilabu vyenye wafuasi wengi kwenye inayoendele leo Aprili 13, ni Fenerbahçe dhidi ya Real Mardid na Kerala B. dhidi ya Allianza Lima.
Ingeandikwa Yanga ndio imeingia robo fainali hizi kejeli zote zisingekuwepo[emoji3]
 
Kombe letu hilo
318611800_690017702490523_6112206769771611730_n.jpg
 
Back
Top Bottom