Simba sport club ipo kuwakomoa wachezaji

Simba sport club ipo kuwakomoa wachezaji

wakimataifa

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Posts
942
Reaction score
168
ukifatilia baadhi ya wachezaji wanavyolalamika kwa jinsi wanavyofanyia na viongozi wao utasikitika
wachezaji wazawa wanalipwa mshahara kidogo malipo ya nyumba ya kuishi wanaahidiwa hawapewi wanaofaidi simba ni wachezaji wa kigeni ndio wanapewa nyumba wakidai haki wanakaripiwa wanatishwa wanawafojia mikataba kama alivyofanyiwa mesi ukiwauelewa wa haki yako utaambiwa huna nidhamu kama yaliowatokea kina chanongo amri kiemba na wengi hawa viongozi wachunguzwe si watu wazuri nimemsikia kiongozi mmoja kwenye radio moja anasema uongo kabisa
 
Wachezaji wetu wanahitaji kubadilika. Nimeshuhudia wakisaini mikataba kwenye ofisi za viongozi wa hizo timu. Sina uhakika kama wanapewa hiyo mikataba week nzima ili kuitafakari na kuomba ushauri kabla ya kusaini.

Inaelekea wanafika ofisini wanapewa dakika kadhaa wapitie na kusaini. Wakati huo fedha ambazo kamwe mchezaji hajawahi kuzipata zipo mezani. Hawalipani Bank. Hiyo ingekuwa kazi ya wakala wa mchezaji. Nahisi wakati Messi anaongezewa mshahara walichomeka nyongeza ya mwaka mmoja kwenye mkataba yeye akasini bila kujua. Ndiyo hayo malumbano sasa kwamba bado ana mwaka mmoja.

Ukweli wenyewe kuna udanganyifu mkubwa sana. Hayo Okwi anayakwepa kwa kuwa na wakala anayepitia mkataba kabla ya kusaini.

TRA mpo? mpate nakala za kila mkataba ili kodi stahiki itozwe bila ajizi. Iweje mfanyakazi mwenye mshahara wa laki mbili unusu kwa mwezi ndio alipe kodi wakati mtu anapata million 20 za usajili halipi? Bado mchezaji huyo ana mshahara wa million mbili kwa mwezi.

Sheria iwawezeshe TRA kupata nakala ya mikataba pale TFF. Kama wastani wa mishahara ya Yanga, Azama na Simba ni 1.5M kwa mwezi na kila timu iwe na wachezaji 25, TRA inaweza kupata zaidi ya million 200 kila mwaka kwa vilabu hivyo vitatu kama kodi ya mishahara tu. Hapo bado kodi kwenye hela za usajili.
 
Ili kuweka kumbukumbu sawa, ifuatayo ni orodha ya malipo ya usajili wa wachezaji wazawa Simba Sc msimu huu.

1. Jonas Mkude = 60m
2. Said Ndemla = 30m
3. Hassan Isihaka = 30m
4. Peter Mwalyanzi = 25m
5. William Lucian = 20m

... na bado usajili unaendelea. Alafu mkuu wakimataifa ukiwa unaandika uwe unakumbuka kuweka nukta katika sentensi zako.
 
Last edited by a moderator:
Mleta uzi sijui ni shabiki wa yanga au una bifu na Simba, kwenye uzi wako wa Singano umeongea upuuzi upuuzi kama huu. wala hata hueleweki nini hasa unataka kusema zaidi ya poroje za vijiweni.
 
Ili kuweka kumbukumbu sawa, ifuatayo ni orodha ya malipo ya usajili wa wachezaji wazawa Simba Sc msimu huu.

1. Jonas Mkude = 60m
2. Said Ndemla = 30m
3. Hassan Isihaka = 30m
4. Peter Mwalyanzi = 25m
5. William Lucian = 20m

... na bado usajili unaendelea. Alafu mkuu wakimataifa ukiwa unaandika uwe unakumbuka kuweka nukta katika sentensi zako.


Kaka jamaa hana hata data na anaonekana ni mtu asiye jitambua, sijui ana bifu gani na Simba
 
Kaka jamaa hana hata data na anaonekana ni mtu asiye jitambua, sijui ana bifu gani na Simba

Mkuu, huyu jamaa sidhani hata kama anaelewa anachokiandika. Ila hatuna budi kumrudisha kwenye reli.
 
Baada ya kumsajili,selinKUMA,Simba jana usiku wamemsajili fuckkk
 
Back
Top Bottom