Kocha aende zake, kimbinu anazidiwa na makocha wengi tu wa kitanzania. Kocha gani unafungwa nje ndani na timu kama Kagera Sugar, ina maana mechi ya kwanza hukujifunza.
Unacheza na Prison haijafungwa hata mechi moja, unashindwa kujua kwanini hawafungwi, mimi nafanyaje ili niwafunge.
Huyo kocha wenu is tactically inept, huwezi kumlinganisha na Leschante.
Hiyo timu mnayoidharau mkimpa kocha makini m'bongo tu itapiga mpira mkubwa sana. Huwa nasema hata akipewa dogo Matola Simba itakuwa moto tu maana anaujua mpira na ana mbinu za mpira.
Kuna wachezaji vijana wadogo kama akina Mlipili wanasugua benchi week in week out, unashindwa kuwapa mechi wakaanza kuwareplace akina Wawa na Nyoni.
Unafanya rotation ila top class goalkeeper Kakolanya anasugua benchi kila mechi, una mpango gani na keeper hodari kama Kakolanya ambae alicheza na Simba yote na hawakumfunga.
Get that coach out of Simba, as a matter of urgency!!