Simba Sports Club achaneni na nia yenu ya kumfukuza kocha wetu Patrick Aussems kwani tutakuja kujuta na kulia akiondoka

Simba Sports Club achaneni na nia yenu ya kumfukuza kocha wetu Patrick Aussems kwani tutakuja kujuta na kulia akiondoka

Nimezifuatilia sababu za baadhi ya Viongozi wa Simba SC na Mashabiki ' Wapuuzi ' wachache juu ya sababu zao kutaka Kocha Mkuu wa Simba SC Patrick Aussems aondoke na Kugundua kuwa zote ni za Kipopoma. Moja ya sababu ambayo hadi hivi sasa imeniacha hoi ni kwamba baadhi ya Viongozi hawamtaki Kocha Patrick Aussems kwakuwa huwa hataki Wachezaji wakae Kambini muda wote na badala yake huwa anataka Timu ikusanyike Siku mbili kabla ya Mechi.

Sasa kama Simba SC tumeshakubaliana Kuingia katika Mfumo wa Kisasa ni kwanini tena tunakuwa na Mawazo ya Kiswahili Kiswahili hivi? Hivi Vilabu vikubwa na vyenye Maendeleo makubwa duniani Wachezaji wao huwa wanashinda tu Kambini Msimu mzima wa Ligi kama wako Shule za ' Bodingi ' ambazo wengi wetu tumepita huko?

Maoni yangu kama GENTAMYCINE na naomba mnisikie Kiumakini kabisa ni kwamba kama kuna Kocha ambaye Simba SC tunaweza kuwa tumepata bahati ya kuwa nae basi ni huyu Patrick Aussems. Nina Wachezaji Waandamizi kabisa wa Simba SC na mwingine sasa anacheza nchi nyingine wote kila ninapozungumza nao wanasema hawajaona tatizo la Kocha Aussems hasa Kimbinu na Kiufundi na Kuondoka Kwake kutaiathiri Klabu kwa Kiasi kikubwa mno.

Sikatai Aussems kama Binadamu anaweza akawa na Matatizo ( Mapungufu ) yake ila tukisema tumfanyie ' Assessment ' hakuna Mtu ambaye anaujua vyema Mpira na amewahi pia Kuucheza anaweza kukubali Kocha Aussems afukuzwe Klabuni. Moja ya Sifa Kuu ya Kocha japo zipo nyingi ni Kocha kuwa na Upendo na Ukaribu hasa wa Kiurafiki na Wachezaji wake kwani hii husaidia Yeye kuweza Kupitisha Mafunzo yake Kiurahisi kabisa na akafanikiwa. Hili Kocha Aussems amefanikiwa nalo kwa 100% ndani ya Klabu ya Simba.

Hivi Kocha ambaye hadi hivi sasa ameifanya Simba SC iongoze Ligi, Timu inacheza vizuri na hata kama huwa inafungwa au inatoka Sare nayo ni sehemu ya Mchezo kwani Falsafa ya Mpira duniani kote inasema kuwa Mpira ni Mchezo wa Kushinda, Kufungwa na Kutoka Sare. Simba SC isifungwe au isitoke Sare yenyewe ni nani? Ni Timu ya Mungu? Kama ni sababu za Kiufundi Kocha Aussems hana tatizo ndani ya Simba SC ila kama Kocha Aussems anafukuzwa pengine kwakuwa hapendi Ujinga, Utoto na Upumbavu tena ule wa Kupangiwa Kikosi au wa kutoa 10% kwa baadhi ya Watu wa karibu wa Simba SC na Viongozi basi ni sawa afukuzwe tu na Mimi GENTAMYCINE nitapiga Goti kwa Mungu ili niiombee ' Laana ' Klabu yangu hii pendwa ya Simba SC.

Mwisho najua na nina uhakika kuwa ' Mwekezaji ' wa Simba SC ' Tajiri ' Mohammed Mo Dewji ni Mdau mzuri na mkubwa wa huu Mtandao wa JamiiForums, tunae hapa 24/7 japo huwa hakai muda mwingi kutokana na Ratiba zake lakini pia ni Mtu ambaye huwa anapenda Kunisoma GENTAMYCINE. Hivyo basi namwomba ( nakuomba ) Mohammed Dewji hebu na Wewe acha Kuingizwa katika huu ' Uswahili ' wa baadhi ya Viongozi wa Simba SC na Mashabiki ' Wapuuzi ' ambao wanakudanganya kuhusu Kocha Patrick Aussems na Wewe unawaamini na Kukubali kuwa atimuliwe.

Nina uhakika tena wa 100% kama Kocha Patrick Aussems atabaki Simba SC, akiaminiwa zaidi, akipewa Ushirikiano, Uweledi ukitawala ndani ya Uendeshaji wa Timu yetu ya Simba, akaongozewa Wachezaji Wawili au Watatu tu ( hasa Washambuliaji ), tukaachana na hawa Wabrazili wa ' Madili ' huku tukijitahidi Kuwarudisha akina James Kotei na Emanuel Okwi Simba SC itafanya vyema si tu katika Ligi Kuu yetu y VPL bali hata katika Mashindano ya Kimataifa ya Barani Afrika.

GENTAMYCINE nakataa na nasema Kocha Patrick Aussems asifukuzwe ndani ya Klabu yetu ya Simba kwani tutakuja Kujuta.
Tayari Kesha temwa mkuu. Naona wamegoma kufanyia kazi ushauri wako. Pole
 
Nategea Kusikiliza Vipindi vyote vya Michezo Redio leo kuanzia Wasafi, Efm,TBC Taifa, Radio One, Magic fm, East Africa Radio na mwishoni Clouds fm na nikisikia tu na Kuthibitishiwa kuwa Simba Sports Club imeachana na Kocha Patrick Aussems nami naachana rasmi Kuishabikia Simba SC ( japo sitoihama ) lakini sitoshughulika nayo kwa lolote na chochote kile badala yake sasa nitakaa zangu pembeni Kuangalia ' Anguko ' Kubwa la Kiwango cha Timu na hatimaye Kufanya vibaya. GENTAMYCINE bado sijaona sababu ya ' Kiutaalam ' ya Kuachana ( Kumuondoa ) Kocha Aussems isipokuwa najua kuna ' Wahuni ' wa 10% na Wazee wa Majungu, Fitina na Unafiki ndiyo wanasababisha huu ' Upuuzi ' wote na ' Laana ' yangu kama Aussems akifukuzwa kweli itawaangukia na watateseka mno. Nadhani huyu Kocha Simba SC ndiyo tulitakuwa tumuheshimu, tumtunze na tumpe Ushirikiano wote ili azidi kutupa Mafanikio badala yake tunaendeleza ule ule ' Uswahili ' wetu tuliobarikiwa na Kukomaa nao tokea enzi na enzi.

Naaam naaam
 
Back
Top Bottom