Simba Sports Club: Taarifa kwa Umma

Simba Sports Club: Taarifa kwa Umma

Hii tunasema ukipigwa ngumi ya sikio wewe mpige ya jicho
 
Hii senema ndio kwanza imeanza....ni bonge la movie wacha tufaidi sie..adi raha aisee
 
Karibu kwetu wananchi na si vibaya na wengine wasiotaka uswahili waje pia...sasa hapa tunamsubiri mwamba wa lusaka na konde boy...
 
Nachoweza kumshauri Senzo lazima kunamambo lazima akubali yaende kienyeji kidogo kwenye hz timu zetu lakini akikomaa ki professionalism hawezi kudumu ardhi hii ya Tanzania.
 
Hivi Senzo hajui kuwa mtendaji mkuu wa Simba ni MO Dewji.
Au hajui kuwa MO ndiye anayemlipa mshahara wake.
Yeye aliajiriwa ili kumshauri MO namna bora ya kuiendesha timu na sio kubishana naye.

Wajibu wake ulikuwa ni kumshauri MO na kama haafiki basi lazima ukubaliane na MO
na sio kumwamrisha.

Hapa duniani timu za mpira haziendeshwi na ma CEO kama senzo, bali wamiliki wa timu kama Katumbi T.P. Mazembe.

Ngoja tumsubiri namna atakavyo iendesha Yanga.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Natamani niendelee kuona vita vya matajiri GSM na MO.
Mwisho mi nawasubiri uwanjani
 
Senzo mwenyewe anaonekana ni professional ila kwenye kuondoka simba hajaonesha proffessionalism kwenye hili sakata,
Maana pamoja na kua ataenda Yanga bado inabidi abadilishe vibali vya kufanya kazi kutoka Taasisi ya Simba kwenda Yanga. Na kwa sheria za kazi mfanyakazi unapotaka kuacha kazi lazima uiandikie Taasisi barua ya kuacha kazi.
Ila Senzo kwa hili amekosea na kibaya ni kwamba ameacha kua professional na kujiingiza kwenye siasa za Simba na Yanga.
Kwa hili Senzo nimekutoa kwenye Professionalism
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Walitaka sana asepe huyu jamaa. Huyu njemba ni kichwa sana. Alizuia mambo ya ovyo pale simba. Viongozi wengi wapigaji walikuwa hawamtaki pale clubuni ksbb alikuwa anaendesha mambo kisasa kwa hiyo alizuia upigaji. Ukitaka kujua hilo wewe soma hiyo taarifa kwa umma ilivyokaa kikuda kuda,imekaa kibwege bwege,yaani kama mtu binafsi anaeandika hiyo taarifa. Imekaa kutaka kumshutumu hivi. Viongozi waliokuwa hawamtaki wamefurahi kujiuzuru ndio maana fasta wamejibu haraka kujiuzuru kwake.
Sasa ulitaka viongozi watoe barua ya kumuomba senzo abadili maamuzi ili muwacheke viongozi wa simba sc
 
Back
Top Bottom