Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
da! mi yanga dam,kwa mara ya kwanza nimesikia raha simba kuwa bingwa.....coz nahisi simba wangekuwa mabingwa kihalali kuliko azam!*
 
da! mi yanga dam,kwa mara ya kwanza nimesikia raha simba kuwa bingwa.....coz nahisi simba wangekuwa mabingwa kihalali kuliko azam!*

Bongo kila sehemu usanii tu! Si ajabu Azam wakawa Mabingwa mwaka huu!
 
da! mi yanga dam,kwa mara ya kwanza nimesikia raha simba kuwa bingwa.....coz nahisi simba wangekuwa mabingwa kihalali kuliko azam!*

azam isingeweza kuwa bingwa kutokana na wao mipango ilikuwa mshindi wa pili kwa hiyo tunasubiri hiyo hukumu tuone..
 
simba hajawa bingwa maana mechi ya azam ni Mtibwa waliogomea penati na hivuo kikanuni azam ana point tatu voyovyote iwavyo, so simba anatakiwa kwanza atoe sare walau mechi ijayo kujitangazia ubingwa, anything can happen, subirini kwanza msishangilie leo
Siasa zimeamia kwenye mpira!!!! duh hiki ni kindumbwe ndumbwe.
 
tunakuombaaaaaaaaaaaa taifa kubwa utujalieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
mnyamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
niulie wasudani weusi nipate rahaa
 
Tuko pamoja mkuu. Tunawatakia kila la kheri mnyama. AUNGURUMAPO SIMBA MCHEZA NANI?????????????????????????????????????
Jibu ni SIMBA WAZEE WA MJINI -MSIMBAZI-KARIAKOO.
 
Mungu ibariki Simba Sport club hapo kesho ishinde kuanzia goli 3 na zaidi bahati iwe upande wa simba na Tanzania katika michuano hii
 
Mungu ibariki Simba Sport club hapo kesho ishinde kuanzia goli 3 na zaidi bahati iwe upande wa simba na Tanzania katika michuano hii

haya dua lako lishakuwa kama uongo vile..
 
Milovan ataka mabao ya fasta Simba Send to a friend
Saturday, 28 April 2012 08:47
0
digg

Kocha wa Simba,Milovan cirkovic
Jessca Nangawe
KOCHA wa Simba Curkovic Milovan amesema haipo sababu kwanini kikosi chake kishindwe kupata mabao ya mapema kwenye mechi ya kwanza raundi ya tatu, Kombe la Shirikisho dhidi ya Al-ahly Shandy ya Sudan kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Milovan anaamini kuwa, ushindi wa mapema na mabao ya kutosha kwenye mchezo huo, utakuwa mhimili muhimu wa kuvuka kikwazo katika mchezo wa marudiano, nchini Sudan wiki mbili baadaye.

Simba ilifika hatua hiyo baada ya kutumia nguvu nyingi kuziondoa kwenye mashindano miongoni mwa timu bora na ngumu katika kinyang'anyiro hicho, Kiyovu ya Rwanda na ES Setif ya Algeria.

Ilitoka sare ya bao 1-1 na wawakilishi wa Rwanda katika mchezo walioanza ugenini, na kisha kuja kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam.

Raundi ya pili, iliifunga ES Setif 2-0 kwenye mechi ya nyumbani, na kisha kufungwa mabao 3-1 ugenini, kipigo ambacho hakikuwakwaza kusogeza mguu mbele kwa mzani wa sheria ya faida ya bao la ugenini.

Milovan atawategemea washambuliaji wake mahiri, akiwemo Emmanuel Okwi, Felix Sunzu, Patrick Mafisango na Haruna Moshi 'Boban' kuipenya na kufunga mabao ya kutosha dhidi ya ngome ya wapinzani wao, ambao sehemu kubwa ni vijana.

Simba imekuwa ikijifua vya kutosha kwenye viwanja wa Sigara, na kocha Milovan anaamini robo ya kwanza ya dakika 45, tayari watakuwa wameshazigusa kamba za wapinzani wao mara kadhaa.

"Nataka washambuaji wawe na kazi mbili, kwanza wahakikishe wanafunga magoli mapema, hii itasaidia kuwachanganya wapinzani wetu, pili wawe makini na washirikiane vyema na wenzao ili kuwanyima mwanya wa kupata bao la ugenini," alisema Milovan.

Pengine kama kuna kitu kinamnyima raha Milovan, basi ni kukosekana kwa beki wake wa kati, Juma Nyoso ambaye kadi nyekundu aliyopewa ugenini, Algeria inamuweka kando kwenye mchezo wa kesho.

"Nafikiria kumchezesha Mafisango katikati, halafu nafasi yake acheze Kapombe, lakini bado sina jibu la mwisho kwani nafasi ya Kapombe itaelemewa. Nina mashaka bado, naangalia nini cha kufanya," alisema Milovan.

Wakati Milovan akikuna kichwa kuelekea mchezo huo, wachezaji wa Simba wamesema watacheza kufa na kupona kupata ushindi mzuri utakaosindikiza furaha za mwisho wa wiki.

Wakizungumza mara baada ya mazoezi yao jana walisema: "Haipo nafasi ya kubweteka, huu ni wakati wetu wa kucheza kufa na kupona kuhakikisha tunashinda mchezo tena kwa mabao mengi. Heshima ni kucheza fainali," walisema.

"Tumejipanga vizuri lengo hasa ni kuhakikisha tunafika mbali, tumeanza vizuri na ni imani yetu tutaendelea kupata ushirikiano toka kwa mashabiki na wadau wa michezo," alisema Kelvin Yondan kwa niaba ya wenzake.
 
Simba Nguvu Moja na Ombi letu moja leo ni ushindi wa mabao ya kutosha
 
Haruna Mafisango wametuinua wanasimba kwenye viti
 
Back
Top Bottom