Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,133
.... Where is the National Pride ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
safi saaaana. nimeipenda hiyo.Tanzania tuna laana jana yanga 2-0 leo simba nayo imefungwa 2-0 kwa mtazamo wangu cjui kama tutafika ..
Oooooh! Taifa kubwa haya ndo mambo gani sasa unafanya? I am angryyyyyyyyyyyyyyyyyyyyy!!!!!!!!!!!!!!!!!!
nasikia mlienda kwa mganga wa yanga ndio sababu..
Vipi matokeo ya Azam?
waganda waliizidi simba.Wangefunga hata matano
Mabingwa wa kombe la ujirani simba sports club, leo imetota kwa mabao 2-0
mbele ya watoza ushuru wa uganda (ura). Ni kilio kingine kwa mashabiki wa
simba na yanga..siku zote mwenzio akinyolewa nawe tia maji.:a s 465:
Watu kama nyie ndo mnatakiwa kuwa mnakuja mara kwa mara kwenye jukwaa la michezo, umejitahidi, analysis yako ni nzuri ingawa kuna watu watakupinga.Nimejaribu kuzichambua timu zote mbili Yanga na Simba ktk mechi zao za ufunguzi ktk kombe la Kagama 2012 na huu ndio MTAZAMO wangu
YANGA
Haikuwa ktk kiwango kizuri kama timu, lakini bado kwa mchezaji mmoja mmoja walijitahidi. Imeonekana kubadilisha style ya mpira wake kutoka kukimbiza, ku-force na hivyo kutumia nguvu nyingi na kuinyima timu pinzani utulivu. Kwa mechi ya juzi, Yanga ilicheza mchezo wa taratibu na utulivu lakini Atletico waliivuruga kwa kucheza mpira wa pasi za uhakika na kasi. Na ilivyo ni kwamba Yanga imebadilisha zaidi ya nusu ya wachezaji wake kwenye kikosi cha kwanza cha msimu uliopita kwa hiyo bado "chemistry" baina yao haijachanganya.
Na hili lilionekana karibu na mwishoni wa mchezo ambapo wachezaji wa Yanga waliamua kila mtu kucheza kivyake kwa nguvu kubwa nadhani ili kuwafurahisha mashabiki lkn hali ilizidi kuwa mbaya.
Kitu kingine nilichokiona ni kwamba Yanga haikuwafahamu kabisa wapinzani wao, na hivyo haikufanyia mazoezi udhaifu wa Athletico. Na hii ni tatizo kubwa kwa timu zetu za Tanzania kwa kuingia kichwa kichwa ktk mashindano bila kufanya home works za nguvu hasa kwa timu zile zinazoonekana kutokuwa na majina makubwa.
Wasiwasi wangu ni kwamba, nafasi ya Yanga kuvuka nusu fainali inatia shaka ukizingatia upya wa kocha, upya wa kikosi na kutengeneza timu wakati mashindano yanaendelea hasa ukuzingatia kuwa timu nyingi za nje kama URA na APR zinaonekana ziko vizuri.. Lakini hakuna lisilowezekana.
SIMBA
Simba katika mechi yake ya kwanza imecheza vizuri lakini haijafikia ubora wake. Inaendelea na style yake ile ile ya kupitishia mashambulizi yake kupitia upande wa kushoto ambako kwa mechi ya jana ulikuwa ndio eneo dhaifu kuliko yote. Kasi na uwezo binafsi wa wachezaji Danny Mrwanda na Abdallah Juma haujafikia au haukuwa sawa na ubora wa Okwi.
Vile vile pamoja na kuwa na kikosi kilichokaa pamoja kwa muda lakini ingizo la wachezaji wapya zaidi ya 4 katika kikosi cha kwanza limeonekana kuiyumbisha timu kwa kiasi fulani hasa katika namna ya kushambulia ambako wachezaji wa Simba walikuwa wanakwenda kwa kasi tofauti na wakiwa ama mbali mbali sana ama wakati mwingine kujikuta wako pamoja wakigombania kufunga.
Kama ilivyo kwa Yanga, bado nao Simba walioonekana kutokuwa wamefanya homework za kutosha kwa wapinzani wao URA ambayo ina nidhamu kubwa ya kimchezo hasa kwenye ulinzi na ushambuliaji. Hawakuwa na tamaa ya kuishambulia Simba kwa nguvu hata pale Simba walipoonekana kupoteza mwelekeo badala yake walicheza kwa utulivu, kumiliki mpira na kuziba njia.
Kama nilivyosema hapo juu Simba bado wana kikosi kizuri na kinachoweza kushindana kama watarudi darasani kuyafanyia kazi makosa ya jana na kusoma wapinzani kabla ya mechi. Ni ngumu kutabiri chochote kwao lakni wanapaswa kujua hawana cha kujitetea maana wamecheza mechi nyingi za kujipima nguvu na wamekuwa na kocha kwa muda sasa.
Naomba kuwasilisha.
Simba kapakatwa.