Imenichukua muda kidogo kabla ya kugundua kwamba Yanga tulifanya vema kutolewa na mtibwa.

Kwanza tulijiepusha na Ku risk,kwani kwenye derby lolote linaweza tokea,japo tuna uhakika Wa kuifunga simba hata tukicheza sasa hivi hapa ninavyoandika,ila kwa sababu mpira unadunda ingetokea wakatufunga timu ingepunguza morali tuliyonayo washabiki ktk kuiamini timu yetu.

Pili,tungekuwa tumechafua image ya brand yetu kwa mashindano ambayo hayana faida kwetu

Tatu, katika mchezo huo Simba wasingekuwa na cha kupoteza manake kama biashara wao wameshafanya kwa kuchukua hela zote ktk derby ya kwanza ambapo wao walikuwa wenyeji hivyo kama tungepunguza morali ya washabiki inamaana Yanga ndio ingekuwa na hasara kawani wao biashara yao wataifanya ktk mchezo Wa marudiano.

Nne, ili mchezo Wa pili uwe na msisimko zaidi inabidi hii tension iliyopo sasa ya Nani ni Mbabe kwa mwenzake iendelee kuimarika japo nyuma ya pazia tunajua kabisa Simba hawatuwezi na tutawakong'ota hadi Manara wamwite Manyaya.

Mwisho kabisa hatuna haja ya kulalamika kutokana na timu yetu kutolewa na mtibwa kwani hii ina faida kwetu wananchi kwani hadi sasa Simba bado wanaumia sana kwa kile tulichowafanyia na wanajiona bado wana deni .

HALAFU!!! HIVI NI KWELI JAMES KOTEI ANAKUJA!??
 
Acha porojo wewe kidunula1, Yanga ana misimu mi3 hawafunga Simba.
Droo kwenu ndio imekuwa furaha msimu wa 4 huu, sasa unakuja na maneno tupu bila haya mkuu
 
Acha porojo wewe kidunula1, Yanga ana misimu mi3 hawafunga Simba.
Droo kwenu ndio imekuwa furaha msimu wa 4 huu, sasa unakuja na maneno tupu bila haya mkuu
Ukweli unao moyoni. Mazingira ya Ile droo yaliwadhalilisha sana na kuwafanya muwe kama vi underdog tu.
 
Droo ndio mnashangilia wiki 2 ..??
Je mkishinda si ndio mtaenda hadi bungeni kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…