SAFU YA USHAMBULIAJI YA SIMBA WANATUVURUGA WACHAMBUZI.
Anaandika @exaud_msaka_habar
Katika eneo ambalo msimu huu litatupa sana wakati mgumu kulijadili ni eneo la ushambuliaji la @simbasctanzania, unaweza kuongea kitu ukaonekana kama hujui mpira kumbe ni kuchanganywa tu.
Leo akicheza Bocco peke yake pale mbele tunasema Bocco ndiye mshambuliaji Bora, na anastahili kuanza kila siku tunamwaga sifa kibao.
Siku akianza Kagere peke yake tunasema sasa huyu ndiye mfungaji Bora kabisa wa Simba na tunamwaga sifa zote.
Sasa akianza Kagere na Mugalu hapo utatupenda wachambuzi, utaskia simba wakianza hivi wanakuwa hatari sana ni balaaa.
Akianza Mugalu peke yake sasa tunaanza WHAT A PLAYER, huyu jamaa ni hatari sana na sifa kibao.
Mi ndio maana nilishajitoa kwenye kwenda na Upepo. Mi nasemaga tu Simba ya Sasa ni Bora sana kwa kuangalia Timu nzima, ni bora kuanzia Inapoanza kwa Kipa mpaka unapofika Golini, yani wana Timu bora ukilinganisha na Timu nyingi za sasa.
Washambuliaji wake wote wanajua goli lilipo, kinachowatofautisha ni inategemea mpinzani wa siku hiyo anafungika vizuri akipangwa na Nani, Kagere, Mugalu au Bocco. ila wote wanajua kufunga.