Ligi kuu msimu huu inajumla ya mechi 34 mpaka Sasa Simba na Yanga tayari zimecheza mechi 6 inamaana wamebakiza mechi 28 kumaliza ligi huku Azam akibakiza mechi 27 nani mwenye uhakika kuwa atashinda mechi zote 28 zilizobaki..??

Ligi ni ngumu na safari ya kumtafuta bingwa bado ni ndefu sana
 
Ni kweli lakini tunapoendelea kudondosha point kizembe hivi ubingwa tunaweza tusiupate mwaka huu
 
Azam kashinda, Yanga Kashinda, jitahidini na ninyi Leo mshinde Mana nimesikia mtacheza Leo jioni na kumbe zile habari za Jana huko sumbawanga zilikuwa si za kweli ni propaganda tu!
 
Kauli za kushindwa hizi ha ha ha
 
Mkuu safi sana kwa kutultea uzi wa Club yetu pendwa ya Wekundu wa Msimbazi!
Nazani itapendeza zaid kuuboresha huu uzi kwanza kwa kuuframe upya katika lugha yetu ya taifa, Simba kwa sasa ina mashabiki mpaka vijijini ambao wengine hii lugha ya Malkia kwao ni changa moto!
Pia uzi ungeongezea vikosi vya kumbukumbu kama kile kilichofika fainali ya CAF mwaka 1993 chini ya mlanda mlango nguli Mohamed Mwameja na kile kilicholirudisha kombe la Afrika Mashariki na kati baada ya kupotea Tanzania kwa miaka 17 chini ya wakali wa zama zile kama Zamoyoni Mogela, Hassan Affif na wengine!
 
Napendekeza uanzishwe uzi maalum kwa ajili ya kuchagiza ushiriki na msisimko wa wanasimba na watanzania wote katika ligi ya mabingwa Afrika 2020/2021. Na ikiwezekana uzi huo uwe na historia ya ushiriki wa timu yetu katika mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika
 
Siamini kama kikosi kipana kinaishi kwa shida namna hii. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ni mwendo wa kushika tama tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…