Kama una account ya BETPAWA ingia hapa ujaribu bahati yako
 
TFF inawafahamisha wadau kuwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni sasa itaanza saa 1 usiku.

TFF imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
 
Je Yanga walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa, NDIYO. Kisheria walikuwa sawa na walikuwa na haki ya kusimamia msimamo wao. Kumbuka walijiandaa kwa muda wa awali.

Je Simba walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa, NDIYO. Walichofanya ni kutii agizo la TFF ambao ni wasimamizi wa ligi.

Je TFF walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa NDIYO. Walipokea maagizo kutoka Wizara inayosimamia michezo. Kumbuka Serikali yoyote ipo kwa ajili ya usalama na maslahi ya raia wake.

Kama wote walikuwa sahihi, Je nani abebe lawama?? Je ni Wizara?? Hapana! Ninaamini maamuzi yalifikiwa kwasababu ya maslahi ya raia, ni mapema sana kulaumu bila kujua sababu.

Je busara ilipaswa kutumika? NDIYO. Lakini swali lingine litakuja, Je wahusika walihusishwa katika maamuzi yaliyofanyika kabla ya kutaka watumie busara??

Simba na Yanga ambao ni wahusika wakuu hapa, walisikilizwa maoni yao kabla muda haujasogezwa mbele?? Kama hawakuhusishwa katika kufanya maamuzi, basi busara haikutumika. Kivipi utake busara kutoka kwao kama wewe hukutumia busara??

Maswali yote haya ni magumu, yanayohitaji majibu magumu ambayo kwasasa hayataleta suluhu. Swali moja la msingi lililobaki sasa ni,

Nini kifanyike??

Mechi imeshaota mbwawa, aibu imeshatokea, hasara kubwa imeshapatikana, limebaki suala moja la msingi, NINI KIFANYIKE??

Mechi itarudiwa?? Kama itarudiwa kwa gharama za nani?? Hasara iliyopatikana nani anaifidia?? Vipi kuhusu mashabiki??

Tafaruku yote hii inajibiwa kwa swali moja la msingi, NINI KIFANYIKE??
 
Je TFF walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa HAPANA.
Sheria na taratibu ya kusogeza/kuhairisha mechi inasemaje?,ilibidi waishauri wizara husika katiba yao inasemaje
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
kaizer chiefs 3 - simba 0 kaeni kwa kutulia mdomo uliponza kichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…