binafsi nimefurahi kwa performance kwenye mechi mbili zilizopita, zimetusaidia tumerudi kileleni sawa na mtani ijapo yeye katuzidi tofauti ya goli moja, kwa morali ilivyo ina maana we are on ascendence while mtani is on descendence na ukijumlisha na kizungumkuti cha kocha wao kutokuwa na mkataba, ina maana tutawapita

go go go wekundu wa msimbazi ubingwa ni wetu 2010/2011
 
Atleast Simba imenipa raha leo baada ya kuchoka sana.....
 
.....nadhani tunarudi kwenye reli ....... na mziki kama kawaida
:car::violin:
Walitufunga lakini hawatatuzuia kuwa mabingwa,walidai watavunja record yetu, na sasa wameshindwa wasubiri mwakani maana mpaka sasa wamedroo mara 3 na raundi ya pili bado,so in the end a better team(SSC) will win VPL.
 
Mnyama aliyejeruhiwa aendelea kuua,
Yanga mmh!

Monday, 25 October 2010



Kiungo wa Simba Rashidi Gumbo akaipiga hesabu za kumtoka beki wa JKT Ruvu, Stanley Nkombo wakati wa mechi ya ligi kuu iliyofanyika kwenye uwanja wa Jamuhuri mjini Morogoro, Simba ilishinda 2-1

Juma Mtanda, Moro na Clara Alphonce, Tanga

MABINGWA watetezi Simba wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo tangu walipofungwa na mahasimu wao Yanga waliopoteza dira kwa suluhu nyingine jana.

Simba wailishuka kwenye uwanja wa Jamhuri kuwakabaili maafande wa JKT Ruvu na kuwachakaza kwa mabao 2-1 ikiwa na siku tatu tangu ilipoicha AFC Arusha 3-1 na kukalia kiti cha uongozi wa ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga mbele ya Yanga iliyolazimishwa suluhu ya pili na Azam kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Kiungo Rashidi Gumbo alikuwa wa kwanza kufunga bao kwa Simba dakika 25, kwa shuti na kumshinda kipa wa JKT Ruvu, Shaibu Issa, kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi kuifungia Simba bao la pili dakika 43, baada ya kumlamba chenga beki Stanley Nkomolo na kupachika mpira huo wavuni.

Gumbo alipoteza nafasi ya kufunga bao lake pili pale alipopaisha juu kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Hillay Echesa.

Maafande wa JKT walirudi kipindi cha pili wakiwa makini zaidi kwa kuongeza ulinzi golini kwao na kufanya mashambulizi machache ya kushitukiza.

Mshambuliaji chipukizi Hussen Bunu aliifungia JKT bao la kufutia machozi zikiwa zimebakia dakika 9, mpira kumalizika kwa kichwa akiunganisha pasi ya juu ya nduguye Abdalah Bunu kufanya matokeo kuwa 2-1.

Katika mchezo huo Simba iliwatoa Partick Ochan na Amri Kiemba na kuwaingiza Mussa Mgosi na Abdalhaman Humoud wakati JKT wao ilimpumzisha Hussein Kikutwa na kumwingiza Pius Kisambale mabadiliko yalikuwa ni faida kubwa maafande hao walipofanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika 81.

Kocha wa Simba, Partick Phiri alisema amefurahisha na matokeo hayo na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake.

Jijini Tanga, Yanga ambayo tangu ilipoifunga Simba Oktoba 16, imezungukwa na wingu la tetesi ya kocha wao Kostadic Papic kutaka kuondoka kwa sababu ya kudai malipo ya mishahara yake, jana alishudia vijana wake wakilazimishwa sare ya tatu msimu huu.

Azam walianza mchezo kwa kasi katika dakika 10 za mwanzo walifanikiwa kufika lango kwa Yanga mara tatu, huku kiungo wake Ramadhani Chombo 'Redondo' akikosa bao la wazi kwa kushindwa kumalizia pasi ya Suleiman Kassim dakika 9.

Yanga walifanikiwa kufika langoni kwa Azam kwa mara ya kwanza dakika ya 16, kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Athumani Idd 'Chuji', kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Simba viungo wa vijana hao wa Kostadic Papic waliendeleza mtindo wao wa kutembeza viatu katikati ya uwanja hali iliyosababisha Chuji na Godfrey Bonny kuzawadi kadi za njano dakika 13 na 14 kutoka kwa mwamuzi Allanus Luwena wa Mwanza.

Winga Mrisho Ngasa aliwachambua mabeki wa Yanga na kupiga pasi nzuri kwa John Boko aliyepiga shuti lililotoka nje uwanja, naye kinara wa ufungaji msimu huu Jerryson Tegete alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Nurdin Bakari, lakini shuti lake liliishia mikono mwa kipa wa Azam, Vladimir Niyonkuru.

Dakika moja kabla ya mapumziko Kassimu alikosa bao baada ya kipa Yaw Berkyo kufanya uzembe, lakini beki ya Yanga chini ya Nadir Haruob ilikuwa makini kuondoa hatari hiyo.

Mashabiki wa Yanga waliofurika uwanjani hapo walimvamia mwamuzi Luwena wakitaka kumpiga, lakini askari wa usalama waliweza kuwahi na kuingilia kati na kuwasindikiza kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Kutokana na kuendekezwa kwa imani za kishirikina katika soka ya Tanzania, wachezaji wa Azam waligoma kuingia vyumbani kwenye Uwanja wa Mkwakwani na kupewa mawaidha yao uwanjani.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga wakionekana kutafuta bao la kuwaweka vizuri kileleni, lakini wachezaji wake Chuji, Nsa na Tegete walipoteza nafasi za kufunga dakika ya 46, 54 na 58 na kuwaacha mashabiki wao wakishika vichwa.

Beki wa Azam, Erasto Nyoni alitaka kumzawadi Tegete bao dakika ya 76, baada ya kurudisha mpira kichwa kwa kipa wake Niyonkuru wakati Jerry akiwa katikati yao, lakini kipa huyo aliyefanya kazi ya ziada kuudaka mpira huo.

Papic alisema mwisho wa mchezo timu yake haikucheza vizuri katika kipindi cha kwanza, lakini walibadilika dakika 45 za mwisho ila bahati haikuwa yao kwani washambuliaji wake walipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Naye Itamar alisema amefurahishwa na matokeo japokuwa wachezaji wake walizidiwa ujanja kipindi cha pili hivyo kuwafanya viungo kupoteza uwezo wao wa kuwachezesha washambuliaji wake.
 
Jijini Tanga, Yanga ambayo tangu ilipoifunga Simba Oktoba 16, imezungukwa na wingu la tetesi ya kocha wao Kostadic Papic kutaka kuondoka kwa sababu ya kudai malipo ya mishahara yake, jana alishudia vijana wake wakilazimishwa sare ya tatu msimu huu.
bwa hahahahhahah hahah Bwa ha ha ha ha ha aha aha ahhahhhhah ahahahha ahhahahhahahhahahhahahhahahahahhahahhahahah ahhahbha ahahhahahhBWA HA AHA HA HA AH AH AH AH AHA HA HHAH AHA AH AH bwa haha w haBWAHAHAHAHHA
BWAHAHAHAHAH HAHAHAHAHAH BWAHAHAHAHA HAHAHHAH HAHHAH HA HA H
 
Kunani tena kwa mtani, Baba yao kagoma kutoa matunzo ya familia yake nn? Naona Papic tia maji tia maji
 
Leo wekundu wa Msimba simba wanaingia uwanjani kukipiga na Kagera Sugar:
Kikosi cha simba cha leo: Kaseja, Shamte, Mafta, Nyoso, Owino, Santo, Gumbo, Okwi, Mgosi, Ochan, Kiemba....
 
Mpka dakika ya 30simba ilikuwa inaongoza kwa goli moja lililofungwa na gumbo kwa njia ya penalt dakika ya 22 na pale moro kipndi cha pili si yanga wala africa lione alie ona lango la mwenzake
 
Naona Kandambili Wamechomoa. Yanga 1 Afrika lion 1, Simba 2 Kagera Sugar 0
 
Naambiwa mpira ulisima kama dakika 15 kagera wakiwa magomea goli la simaba la pili wakidai mfungaji alikuwa ameotea...
 
Ha ha haaaa raha iliyoje mabingwa watetezi tumerejea tena kileleni , naona watani wamepata post-simba syndrome

kazi wanayo ,nguvu zote waliziweka kuizuia simba na kweli maana siku ile walilinda goli ile mbaya na nafikiri wamechoka sana na ndio maana wanatoa droo kila siku

mnyama kileleni pointi 24 na magoli 16 wakati kandambili wanendelea kusuasua kwa pointi zao 22,
 
...Kuna mtangazaji ametania kuwa 'Yanga bado wako honeymoon ya kuishinda Simba wakati wenzao wanachanja mbuga!! Usikute kuna mgomo baridi na hakuna mchezaji ambaye ameishapewa mshiko wake kutoka kwenye zawadi iliyovuvuzelwa kwa saaana ya Shilingi Milioni 50!!!
 
Nimependa sana utulivu wa Simba, baada ya mechi waliyokosa bahati dhidi ya yeboyebo....Well done vijana wekundu!:A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S 41:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…