Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Simba yaipiga bao Yanga, yamnasa nyota Z'bar Send to a friend Thursday, 25 November 2010 20:31 0diggsdigg

Clara Alphonce na Sosthenes Nyoni

KLABU ya Simba imeshinda vita ya kugombea mshambuliaji wa Zanzibar Heroes, Ally Ahmed Shibori baada ya kumsainisha mkataba wa miaka mitatu juzi usiku.

Awali, klabu hizo mbili zilitangaza nia ya kumsajili mshambuliaji huyo, ambaye hata hivyo ameridhia uamuzi wa kujiunga na Simba.

Juzi, uongozi wa Yanga ulitangaza kutumia usafiri wa ndege kumfuata Shibori kisiwani Zanzibar ili kuwapiku watani zao wa jadi,Simba ambao walitumia ule wa boti kwenda visiwani humo.

Lakini, jana akizungumza na Mwananchi, Katibu Mwenezi wa Chama cha Soka cha Zanziba ( ZFA), Maulid Hamad Maulid alisema kuwa mchezaji huyo amefikia makubaliano na Simba tangu juzi jioni.

Alisema makubaliano hayo yalifikiwa katika kikao ambacho kilihusishwa viongozi wa juu wa klabu ya KMKM ambayo Shibori alikuwa amesajiliwa muda mfupi akitokea Duma ya Pemba inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Kwa upande wa Simba, iliwakilishwa makamu mwenyekiti wake, Godfrey Nyange ' Kaburu'.

Maulid alisema kuwa wamezungumza na KMKM , ambao ndio washindi wa pili wa Ligi ya Zanzibar kutokana na ukweli kuwa mchezaji huyo alishahamishwa hapo akitokea Duma, ingawa hajakaa kwa muda mrefu.

Alisema kufuatia mazungumzo hayo wameshakamilisha na sasa Shibori ni mchezaji huru kuvaa jezi za Simba kuanzia Januari mwakani wakati wa kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Tayari taarifa ya uhamisho huo imeshafikishwa ofisi zaShirikisho la Soka Tanzania ( TFF) na KMKM wametoa kibali cha kumruhusu mchezaji huyo kuichezea Simba," alisema Maulid.
Aliongeza kuwa wao kama ZFA tayari wameshaandika barua kwendaTFF, ili shirikisho hilo liweze kutoa kibali hicho, lakini aliongeza kuwa alishangaa kusikia juzi kusikia kuwa Yanga nao walikuwa wakimtaka mchezaji huyo, bila kufuata taratibu.

Wakati huo huo; uongozi wa klabu ya Azam umeitaka Yanga kuacha mara moja kumhadaa mshambuliaji wao Mrisho Ngassa ukisema kitendo hicho ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Juzi, mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema wakati akisoma maazimio ya kikao cha kamati ya utendaji ya klabu kilichokutana wiki hii kuwa klabu yake inafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha inamrudisha kundini Ngassa.

Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars aliuzwa na klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu kwenda Azam kwa uhamisho uliovunja rekodi nchini ambao ni Sh 58 milioni.

Nchunga alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa tayari walikuwa wamekutana na mchezaji huyo ili kuzungumzia suala hilo.

Lakini, jana katibu mkuu wa Azam, Idrisa Nassoro alisema kuwa kitendo cha uongozi wa Yanga kuzungumza na Ngassa ambaye ana mkataba badala ya uongozi wa klabu kama taratibu na kanuni za Fifa zinavyoeleleza ni ukiukwaji wa dhahiri wa kanuni na unapaswa kupingwa na wadau wote wa soka nchini.

Katibu huyo alisema kuwa mbali ya kukiuka kanuni za Fifa, pia njia zinazotumiwa na Yanga ni dhahiri zinachangia katika kuvuruga utulivu wa akili ya mchezaji huyo na kusababisha acheze chini ya kiwango.

"Tunataka ifikie wakati wadau wote wa soka tushirikiane kukemea mambo yenye lengo la kuharibu soka , kitendo cha uongozi wa Yanga kuzungumza na mchezaji wetu (Ngassa) akiwa na mkataba nasi Azam huku ligi ikiendelea ni ukiukwaji wa wazi wa kanuni za Fifa zinazozuia klabu au mawakala wa wachezaji kufanya hivyo.

"Wao kama wanamtaka Ngassa wanatakiwa kuja kwetu huo ndio ustaarabu, kama unavyojua hata alishindwa kucheza kwa kwa kiwango chake cha kawaida katika mechi za awali za ligi k utokana na mambo kama haya.

Sasa wakati ameanza kurudi kwenye hali ya kawaida ya uchezaji wanataka kumharibu tena, huu sio ustaarabu ,"alisema Nasoro.

Kiongozi huyo wa Azam alisema kuwa katika mazingira ya kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani wao kumuuza tena Ngassa wakati huu ambao kikosi chao kimeanza kuimarika na matarajio yao ya kutwaa ubingwa msimu huu yanaonekana dhahiri.

"Hivi kweli inawezekana vipi wakati timu imeanza kuimarika sisi tumuuze Ngassa ni jambo lisiloingia akilini sisi tumuuze halafu tumchukue nani ,"alisema Idrisa.

Idrisa alisena kikosi cha Azam kitaingia kambini kesho kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi ambao umepangwa kuanza Januari 15 mwakani.
 
Kwa hili simba mmenikwaza sana mimi nimejisajili ilikuchangia timu yangu (SIMBA) kila ninapo tumiwa habari zinazo ihusu simba ni muda mrefu sasa tangu nifanye hivyo nimekuwa nikikatwa pesa kweli...ajabu tarehe 14-12-2010 saa nane na dakika 28 nilitumiwa msg hii: "Real Madrid inaweza isimuhitaji Carlos Teves pamoja na kuwa bosi wake Jose Mourinho anamzimia sana, na hii ni kutokana na thamani ya pauni" na "Yasemekena kwamba, bosi wa Manchester City Roberto Mancini atamvua unahodha mshambuliaji Carlos Teves na kumuhamishia katika timu ya wachezaji wa akiba" ilibidi nijitoe dakika hiyo hiyo kwasababu lengo langu si kupata habari za Manchester City au Real Madrid na nimegudua watu wengi wamejitoa kwasababu hizo....mmeshindwa kukusanya pesa za uanachama tangu nijiunge mwaka 2007 sijalipia nikiuliza naambiwa ikifika wakati wa kulipa utajulishwa hivi wewe Rage na Kaburu hivi vitu unataarifa navyo..watu mkoani wanataka uanachama viongozi wamekaa dar tu wanategemea kuomba omba na kutumia njia chafu kuapata pesa wakati njia sahihi zipo
 
Jasili haachi asili.
Simba walidaiwa mpaka pesa za chapati walizokula wachezaji ambao walizuiwa kuondoka kwa Mama ntilie walipokuwa wamekwenda kula mpk bakuli likapitishwa na wasamaria wema kuchangia na kuwakomboa wachezaji.
So kwa style kama hizo usitegemee jipya hapo zaidi ya ushuzi tu.
 
Umesahau wakati wa enzi za marhum Rashid Ngozoma Mafruit alipopitisha mchango wa maharage kuchangia kambi ya Yebo yebo huh?
 
katika pitiapitia yangu ratiba ya klabu bingwa afrika mwakani,nimeona simba inaanza raundi ya awali na timu kutoka Comoro,mshindi wa mechi hiyo anacheza na TP Mazembe ktk raundi ya kwanza
 
jamani nauliza tu, hii thread si ilianzishwa na nyani<abiziani? ndo kusema nyani amebadili jina na kuwa ivuga au ni anza siredi tu??
 
Dewji kurejesha udhamini wake Simba Send to a friend Wednesday, 29 December 2010 20:32 0diggsdigg

Vicky Kimaro

BAADA ya muda mrefu, klabu ya Simba inatarajia kurejea tena katika medani ya soka ikijiendesha kwa udhamini wa mamilioni kutoka Kampuni ya Mohamed Enterpress ya jijini Dar es Salaam.

Tayari mmiliki wa kampuni hiyo, Mohammed Dewji ameonyesha nia ya kurejesha udhamini klabu wake kwenye klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.

Habari za uhakika ambazo Mwananchi imezipata zinasema kuwa Dewji ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini kupitia CCM yupo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na uongozi wa Simba kwa lengo la kurudi tena kwenye klabu hiyo inayokabiliwa pia na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na ile ya Mabingwa Afrika.

" Mo ataidhamini Simba kwa miaka miwili wapo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo siku yoyote kuanzia sasa wanasaini mkataba, lakini amewapa sharti la kusaini mkataba wa mwaka mmoja mmoja,wakifanya vizuri kwenye mashindano yao ndio ataongeza tena mkataba,"alisema mtoa habari huyo

Mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hakutaka jina lake litajwe alikiri : "Kwa kweli tuna shida sana ya fedha sio siri, nasi tungependa Mo atusaidie, kuna wenzangu ndio waliokuwa wanafanya naye mazungumzo na mwelekeo wameniambia kuwa ni mzuri nay Mo amekubali kutudhamini tena kwa vile tayari ameachana na Africa Lyon.

"Mimi binafsi sijaongea naye, ila wapo wenzangu ndio wanaoshughulikia suala hilo na wanakaribia kumalizana naye,"alisema kiongozi huyo.

Dewji alishawahi kuidhamini klabu hiyo miaka ya nyuma kabla ya kuachana nayo na kuinunua Mbagala Market ambayo ilipanda daraja na kisha kuibadilisha jina na kuitwa Africa Lyon.
Hata hivyo, Dewji maarufu kama'Mo' aliachana na Lyon msimu huu baada ya kufanya vibaya msimu uliopita na kuiuza kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya RBP Oil, Rahma Al- Kharoos.
 
Tusubiri taarifa rasmi kutoka kwa Mheshimiwa Mwenyekiti (MP),haya mambo ya "kuna mtu kaongea naye na mazungumzo yanaenda vizuri", inabaki kuwa ni tetesi.
 
YANGA NA SIMBA WAPAMBANA USIKU HUU ZENJI, NA SIMBA WATWAA UBINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI
Shein%2Bkukabidhi%2Bkombe.JPG
 
Back
Top Bottom