Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
- Thread starter
-
- #1,061
Simba yaipiga bao Yanga, yamnasa nyota Z'bar Send to a friend Thursday, 25 November 2010 20:31 0diggsdigg
Clara Alphonce na Sosthenes Nyoni
KLABU ya Simba imeshinda vita ya kugombea mshambuliaji wa Zanzibar Heroes, Ally Ahmed Shibori baada ya kumsainisha mkataba wa miaka mitatu juzi usiku.
Awali, klabu hizo mbili zilitangaza nia ya kumsajili mshambuliaji huyo, ambaye hata hivyo ameridhia uamuzi wa kujiunga na Simba.
Juzi, uongozi wa Yanga ulitangaza kutumia usafiri wa ndege kumfuata Shibori kisiwani Zanzibar ili kuwapiku watani zao wa jadi,Simba ambao walitumia ule wa boti kwenda visiwani humo.
Lakini, jana akizungumza na Mwananchi, Katibu Mwenezi wa Chama cha Soka cha Zanziba ( ZFA), Maulid Hamad Maulid alisema kuwa mchezaji huyo amefikia makubaliano na Simba tangu juzi jioni.
Alisema makubaliano hayo yalifikiwa katika kikao ambacho kilihusishwa viongozi wa juu wa klabu ya KMKM ambayo Shibori alikuwa amesajiliwa muda mfupi akitokea Duma ya Pemba inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kwa upande wa Simba, iliwakilishwa makamu mwenyekiti wake, Godfrey Nyange ' Kaburu'.
Maulid alisema kuwa wamezungumza na KMKM , ambao ndio washindi wa pili wa Ligi ya Zanzibar kutokana na ukweli kuwa mchezaji huyo alishahamishwa hapo akitokea Duma, ingawa hajakaa kwa muda mrefu.
Alisema kufuatia mazungumzo hayo wameshakamilisha na sasa Shibori ni mchezaji huru kuvaa jezi za Simba kuanzia Januari mwakani wakati wa kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Tayari taarifa ya uhamisho huo imeshafikishwa ofisi zaShirikisho la Soka Tanzania ( TFF) na KMKM wametoa kibali cha kumruhusu mchezaji huyo kuichezea Simba," alisema Maulid.
Aliongeza kuwa wao kama ZFA tayari wameshaandika barua kwendaTFF, ili shirikisho hilo liweze kutoa kibali hicho, lakini aliongeza kuwa alishangaa kusikia juzi kusikia kuwa Yanga nao walikuwa wakimtaka mchezaji huyo, bila kufuata taratibu.
Wakati huo huo; uongozi wa klabu ya Azam umeitaka Yanga kuacha mara moja kumhadaa mshambuliaji wao Mrisho Ngassa ukisema kitendo hicho ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Juzi, mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema wakati akisoma maazimio ya kikao cha kamati ya utendaji ya klabu kilichokutana wiki hii kuwa klabu yake inafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha inamrudisha kundini Ngassa.
Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars aliuzwa na klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu kwenda Azam kwa uhamisho uliovunja rekodi nchini ambao ni Sh 58 milioni.
Nchunga alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa tayari walikuwa wamekutana na mchezaji huyo ili kuzungumzia suala hilo.
Lakini, jana katibu mkuu wa Azam, Idrisa Nassoro alisema kuwa kitendo cha uongozi wa Yanga kuzungumza na Ngassa ambaye ana mkataba badala ya uongozi wa klabu kama taratibu na kanuni za Fifa zinavyoeleleza ni ukiukwaji wa dhahiri wa kanuni na unapaswa kupingwa na wadau wote wa soka nchini.
Katibu huyo alisema kuwa mbali ya kukiuka kanuni za Fifa, pia njia zinazotumiwa na Yanga ni dhahiri zinachangia katika kuvuruga utulivu wa akili ya mchezaji huyo na kusababisha acheze chini ya kiwango.
"Tunataka ifikie wakati wadau wote wa soka tushirikiane kukemea mambo yenye lengo la kuharibu soka , kitendo cha uongozi wa Yanga kuzungumza na mchezaji wetu (Ngassa) akiwa na mkataba nasi Azam huku ligi ikiendelea ni ukiukwaji wa wazi wa kanuni za Fifa zinazozuia klabu au mawakala wa wachezaji kufanya hivyo.
"Wao kama wanamtaka Ngassa wanatakiwa kuja kwetu huo ndio ustaarabu, kama unavyojua hata alishindwa kucheza kwa kwa kiwango chake cha kawaida katika mechi za awali za ligi k utokana na mambo kama haya.
Sasa wakati ameanza kurudi kwenye hali ya kawaida ya uchezaji wanataka kumharibu tena, huu sio ustaarabu ,"alisema Nasoro.
Kiongozi huyo wa Azam alisema kuwa katika mazingira ya kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani wao kumuuza tena Ngassa wakati huu ambao kikosi chao kimeanza kuimarika na matarajio yao ya kutwaa ubingwa msimu huu yanaonekana dhahiri.
"Hivi kweli inawezekana vipi wakati timu imeanza kuimarika sisi tumuuze Ngassa ni jambo lisiloingia akilini sisi tumuuze halafu tumchukue nani ,"alisema Idrisa.
Idrisa alisena kikosi cha Azam kitaingia kambini kesho kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi ambao umepangwa kuanza Januari 15 mwakani.