Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Mazembe wazuri ila TULIJIPA MOYO TU, na hata hivyo hawakufunguka kama kawaida yao kwenye home & away games vs SIMBA.
 
Hii thread mbona haiko up to date? kwa sisi ambao tupo mbali nilitegemea kupata matokeo na matukio ya mechi ya jana kati ya Simba na Tp Mazembe, kulikoni wakuu? hebu tumwagieni data yaliojili.
 
Hii thread mbona haiko up to date? kwa sisi ambao tupo mbali nilitegemea kupata matokeo na matukio ya mechi ya jana kati ya Simba na Tp Mazembe, kulikoni wakuu? hebu tumwagieni data yaliojili.

mechi illiahirishwa baada ya mazembe kuwahonga mareafrii
 
JKT yapanga kuitibulia Simba Send to a friend Sunday, 03 April 2011 20:25 0diggsdigg

Sosthenes Nyoni
NAHODHA wa timu ya JKT Ruvu, Shahibu Nayopa ameiambia Simba wao sio daraja la kuchukulia ubingwa hivyo wajiandae kutibuliwa malengo.Simba na JKT zitakabiliana katika pambano la Ligi Kuu litakalofanyika jijini Dar es Salaam Aprili 6.

Mchezo huo ambao unasubiriwa na wengi unahesabiwa kuwa mtihani wa mwisho kwa Simba yenye pointi 45 kabla kutangazwa ubingwa ili hali ikisubiri kuivaa Majimaji ambayo tayari imeshuka daraja.

Akizunguza na Mwananchi jana, Nayopa alisema kuwa hawatarudia makosa kama yale yaliyowasababisha wakafungwa katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

"Sisi si daraja bwana, kama wanafikiri watatangaza ubingwa kwetu watakuwa wanajidanganya tu kwa sababu hata sisi tunataka pointi tatu,"alisema Nayopa.

"Tuliangalia makosa yaliyosababisha tukafungwa katika mpambano wa mzunguko wa kwanza hivyo kila mmoja wetu alilitambua hilo na amelifanyia kazi,"alisema Nayopa.

Alisema kuwa ana uhakika wataibuka kidedea kwa kuwa hata katika mpambano wao wa mzunguko wa kwanza walionyesha kiwango cha hali ya juu, lakini walishindwa kutumia nafasi walizopata tofauti na wenzao.
 
hawa wanaota nini nao? tutararua
lions.jpg
 
Simba kwa kheri Afrika Send to a friend Sunday, 03 April 2011 20:33 0diggsdigg

okwi-akimtoka.jpg
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akijaribu kumtoka beki wa TP Mazembe, Stopila Sunzu wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Picha na Jackson Odoyo.

Sosthenes Nyoni
NDOTO ya mabingwa wa Tanzania, Simba kusombe kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imebaki hadithi baada kupokea kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa TP Mazembe jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao mara mbili wa Afrika, waliuanza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 18, kupitia mshambuliaji wake Given Singuluma aliyeunganisha vizuri mpira wa kona uliopigwa na Patou Kabangu.

Shija Mkina aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juma Jabu aliyeumia alipatia Simba bao la kusawazisha dakika 58, kufutia mpira wake wa krosi kwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha Kidiaba Robert asijue la kufanya.

Mshambuliaji Allan Kaluyituka alipatia Mazembe bao la pili dakika 63, baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Simba, kabla ya Mbwana Samatta kuisawazishia tena Simba dakika ya 65, akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona wa Amri Maftah kufanya matokeo hayo kuwa 2-2.

Nyota wa Zambia, Singuluma alimaliza ubishi kwa kupachika bao la tatu dakika 73, baada ya kupokea pasi nzuri ya Kaluyituka na kupiga shuti lilomshinda Juma Kaseja na kujaa wavuni.

Simba watajilaumu wenye kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha kwanza baada ya washambuliaji wake Samatta, Emmanuel Okwi na Mussa Mgosi kupoteza nafasi nyingi za wazi.

Dakika ya 3, Mgosi alishindwa kumalizia kona ya Okwi baada ya mpira wake wa kichwa kupaa juu, lakini mashabiki wa Simba wataikumbuka nafasi nzuri aliyokosa Samatta baada ya kumtoka beki wa Mazembe, Stopila Sunzu na kubaki yeye na kipa, lakini shuti lake lilidakwa na Robert Kidiaba.

Katika mchezo huo Simba walitawala sana sehemu ya kiungo na kufanya mashambulizi mengi, huku wapinzani wao wakicheza kwa kujihami na kufanya mashambulizi ya kushitukiza na kupiga mashuti ya mbali.

Awali mashabiki wanaodaiwa kuwa wa TP Mazembe walipambana na Polisi wakati wakijaribu kuingia kwenye jukwaa ambalo hakustahili kukaa.
 
Leo ndio tunakuwa mabingwa kwa kuwafunga hawa jkt,ingawa game itakuwa ngumu bt leo goli tatu zipo.
 
mmh ubingwa upo shakani
nahsi bingwa atapatikana kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, sasa sijui tff wao wanatumia kigezo kipi
 
mmh ubingwa upo shakani
nahsi bingwa atapatikana kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, sasa sijui tff wao wanatumia kigezo kipi
Naomba iwe magoli ya kufunda na siyo tofauti ya magoli....
 
Naomba iwe magoli ya kufunda na siyo tofauti ya magoli....

Ha ha ha ha
Mkuu pole sana
Kanuni inaanza na tofauti ya mabao, halafu matokeo baina ya timu mbili husika, na mwishoe mabao ya kufunga
 
Back
Top Bottom