Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Mambo 10 nilioyaona Simba vs Kaizer Chiefs


1: Simba OUT.. Jasho Limevuja, Damu imemwagika. Kutoka Robo Fainali ya 2018/19 hadi 2020/21 kila shabiki wa Simba atakuwa anaondoka Kwa Mkapa, akijipa kifuani mwake. Kuna HATUA KUBWA SANA Simba imepiga.


2: Well Done kwa wachezaji wa Simba [emoji122] Wamepambana sana. Walionyesha Thamani ya Logo ya Simba kwenye jezi walizovaa. Kwa presha ya mechi ilivyokuwa, Ukubwa wa Kaizer, kama unapenda mpira, una kila sababu ya kuheshimu MABAO MATATU, SIMBA aliyoyafunga kwa Mkapa


3: Well done Gomes[emoji122] Tactically, 'game plan' ilikuwa superb sana. Niliipenda sana Sub ya Muzamir kwa Morisson. Kama kuna mahala mpango wake ulikwama basi ni kwenye majukumu ya Kapombe. Kivipi?

4: Didier alitaka viungo wautembeze mpira na sio kutembea na mpira. Miquissone na Chama wakawekwa kwenye 'half Spaces' ili kutengeneza 'gape' kwa mabeki wa pembeni kupita na kushambulia. Sielewi kwanini Kapombe alichagua zaidi kupiga krosi nyingi za juu. Low Crosses zingeweza kuwa na manufaa zaidi


5: Simba wamepiga mashuti 32.. ON TARGET 10[emoji119] Hapa unaanza kuisifia mikono ya kipa wa Kaizer, BVUMA kisha unaelewa ni kwa kiasi gani presha ya mchezo ilivyoathiri ufanisi wa Attackers wa Simba. Mashuti mengi ya Miquissone yalikuwa Off Target. Hii sio kawaida yake. Presha ilikuwa kubwa sana.

6: Kama kuna kitu Uongozi wa Simba unatakiwa uondoke na home work kuelekea kwenye usajili wao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa, basi ni yule kitasa wa Kaizer, ERIC MATHOHO. Ujasiri wake umeisaidia sana Kaizer muda ambao wenzake walishakata tamaa

https://trc.taboola.com/operasoftwa...oYFmRjCNIDEOAGGAhkYwiWFBCZHBgYZGMI9BQQnh0YH2Q

7: Kennedy Wilson[emoji119] WOW. Ujio wake ulipunguza madhara ya Kaizer kwenye Aerial Ball.Alishinda mipira mingi kwenye kichwa cha Nurkovic, hii ikamfanya kocha wa Kaizer afikirie Plan B ambayo hakuwa nayo.

8: Chama [emoji119] What A Player.. Hakuwa na mambo mengi leo. Aliutembeza mpira kwenye njia yake kwa kasi sana. Finishing yake ilikuwa superb sana


9: Bocco kaweka kamba 2 muhimu Lakini naamini kwenye moyo wake ataziota zaidi nafasi alizokosa kuliko alizofunga

10: Asante Tshabalala. Alikuwa superb sana kwenye kuipandisha timu na kudumbukia vyema katikati muda ambao viungo wake walivamia zone ya Kaizer


Nb: Kwa pira lile, yule dereva aandaliwe mapema [emoji3]




[emoji2398]Ally Kame
Simba hawatakuwa na pesa ya kuvunja mkataba wa Eric Mathoho ila kuna walinzi wawili wanaweza kuwa mbadala wa huyo.

1.Adrian Chama wa Zesco United.

2. Salomon Charles Bievenue Banga Bindjeme wa CotornSport ya Cameroon.

3. Mohamed Quattara wa Al Hilal Omdurman ya Sudan

Hao ni defenders wazuri sana na umri wao bado sana.
 
Leo mnyama akipiga pira biriani plus ushindi mnono mbele ya wajelajela nadharia ya kikosi kipana itapita bila kupingwa
Wee mwanamke una matatizo( usiniulize nmejuaje kuwa wee ni mwanamke) na wala usipinge kuwa wewe ni mwanamke
 
Wee mwanamke una matatizo( usiniulize nmejuaje kuwa wee ni mwanamke) na wala usipinge kuwa wewe ni mwanamke
Kwa hiyo nina maumbile kama ya mama ako au????[emoji38][emoji38][emoji38] au yeye amenizidi urefu wa kina wa k yake embu njoo tujadili kwanza
 
Simba kama tutamwaacha Francis Kahata na Hassan Dilunga msimu huu basi tumtazame kwa jicho pevu Morlaye Sylla wa Horoya Fc huyu ni midfielder anayecheza Central Midfield na Attacking Midfield ni mobile kuliko Kahata na Dilunga.

Morlaye Sylla ana urefu wa 1.70m karibia sawa na Clatous Chama lakini ni strong kuliko Chama na Kahata anaweza kucheza kwenye eneo analocheza Chama kwa usahihi ule ule kama Chama ila siyo mfungaji mzuri kama Chama.

Morlaye Sylla atatuwezesha kumchezesha Tadeo Lwanga kama anchor man tofauti na sasa tunalazimika kutumia double pivot kwa sababu ya kutokuwa na Central midfielder anayeweza kucheza double role.

Mimi siyo mtaalamu wa mpira ila Morlaye Sylla ni chaguo sahihi kwetu.tukumbuke msimu ujao kama timu hizi zote zitaingia hatua ya makundi basi Horoya tutakuwa nao kundi moja tuanze kuwabomoa mapema.
 
IMG_1799.jpg
 
Unadhani kwanini Yanga hawajakanusha tetesi za kusajiliwa Shabaan Djuma lakini nguvu kubwa sana inatumika kukataa usajili wa Ajib? Akili za kuambiwa.........
 
Back
Top Bottom