Simba Tufungwe Mechi 2 Mfululizo, Salam kwa MO Kutuletea Makonda

Kashindwa kukuza brand za mengine ndio aweze Simba? Nyie watu vipi? Wengine tumekuwa na Simba tokea mshamba huyo wa Kolomije hajazaliwa hivyo hatumtaki ebo!
Simba sio ya kuwa na watu wenye mikono iliyojaa damu

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha chuki bhana haitajenga chochote .....pale yuko limited hawezi fanya chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kashindwa kukuza brand za mengine ndio aweze Simba? Nyie watu vipi? Wengine tumekuwa na Simba tokea mshamba huyo wa Kolomije hajazaliwa hivyo hatumtaki ebo!
Simba sio ya kuwa na watu wenye mikono iliyojaa damu

Sent using Jamii Forums mobile app


Hivi kama mashabiki tunafanyeje jamani mi usiku sijalala hata insta nime unfollow kila kitu cha Simba.
 
Aliyekudanganya Simba SC ni kwa ajili ya Pwani tu nani?
Unamjua hata muanzilishi wa Sunderland wewe?
.
Timu iliyokuwa ya dsm hadi sasa inahangaika kuliondoa hilo jina ni Yanga inaitwa Dar Es Salaam Young African, Klabu ya Simba haijawahi kuwa na mlengo huo ndio maana tume wa overtake vyura
Shadeeya
 
Timu mumemuuzia MO halafu mnampangia kitu cha kufanya? MO anafanya atakavyo hakuna wa kumuuliza, yeye ndio analipa mshahara wachezaji na kocha, nyie kazi yenu ni kushangilia basi
 
msiompenda Makonda kupewa nafasi ya ushari mhame timu, nenda mkashabikie Dar yanga Africa, mnatoa hoja za milengo ya kisiasa badala ya uhalisia wa mtu kwenye nafasi aliyopewa. mara kaua, mara ana mkono wa damu! what!?? nyie mmeuwa wangapi? wengine mmeshirikiana kuharibu mimba kibao na wapenzi wenu kwani huko sio kuua! nyambafu.. fanya kazi makonda tuko nyuma yako...
 
Sema upendavyo kashifu utakavyo kikubwa tumeyataka wenyewe yani pamba ya mwanza au lipuli ya Iringa iwe na historia tofauti na Wazawa wa mikoa ilipoanzishwa...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema sitaki ,Mimi mwanachama wa simba naunga mkono tena ikibidi alete watu wengine influential kabisa Simba inapaswa kuwa taasisi ndani yake yenye watu maarufu kabisa ikibidi hata raisi wetu ,waziri mkuu ,makamu wa raisi wawe washauri wa SSC
 
Mkuu unaonekana u mjinga kupindukia. Wewe si lolote na si chochote kwa kila kitu kuihusu Simba. Usiweke misimamo yako ya kisiasa kwenye mambo usiyokuwa na uwezo nayo. Kikubwa unachoweza kufanya ni kuacha kuishabikia simba kama kweli hapo awali ulikuwa na mapenzi nayo.
Mo ndo mwenye timu kwa sasa wengine wote tunabaki kama mashabiki tu. Hatuna mchango wowote popote ukiacha viingilio vyetu mpirani ambavyo havitoshi kwa chochote. AU UNATAKA WASHAURI WA MO KWENYE TIMU WAPIGIWE KURA?
 
Hivi kwa akili yako finyu Makonda anashauri nini kwenye mpira?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ni chuki zako binafs mkuu cc wanasimba tunaunga mkono boss mo alichoamua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulikuwa na wanasiasa ndani ya Simba toka enzi na enzi labda wewe ndio haujui mbwiga toka porini.
Walikuwepo kina Profesa Sarungi, Profesa Kapuya na wapo wengine tuu kama Majaliwa nk. Lakini kwa nini hao wote hakuna anayepigiwa kelele zaidi ya hilo tutusa Bashite?
We bisha tuu, lakini hili utaliona mwisho wake. Makonda hawezi kuwa kwenye timu yetu.
Unaposema mie sio kitu kwa Simba unanijua au unaendekeza upumbavu wako tuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa ni chochote kwa Simba wala usingeleta ujinga wako hapa, ungepeleka hayo mawazo yako kwenye vikao husika vyenye maamuzi. Ni kweli pia kwamba sikujui lakini dalili zote zinaonesha wewe ni mmoja kati ya kajambanani wasio nyuma wala mbele waliojazana mitaani. Kutwa kucha kulalamika tu. Nakushauri ANZISHA TIMU YAKO HALAFU MAKONDA NA WOTE USIOWAPENDA WASIRUHUSIWE HATA KUJA MPIRANI SIKU INACHEZA. Vinginevyo acha mmiliki wa timu atimize yanayompasa kufanya kwa mjibu wa taratibu.
 
Simba ni mali ya MO, sasa utampangiaje mtu na mali yake? MO ametumia bilioni 4 zake kulipa mshahara, we hujatoa hata mia halafu unataka kumpangia? hata kesho akimfanya Makonda kocha sawa tu hakuna atakaethubutu kumpinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…