Simba Tufungwe Mechi 2 Mfululizo, Salam kwa MO Kutuletea Makonda

Simba Tufungwe Mechi 2 Mfululizo, Salam kwa MO Kutuletea Makonda

Huu unaitwa mfano bomba! Watu sijui wanashindwa kuelewa nini!
Makonda aliyochochea huko jiji akayamalize na asipewe nafasi kuleta mitafaruku Simba.
Marehemu Ruge alimfanya Makonda rafiki na Clouds kukawa nyumbani kwake, nini alikuja kufanya baadae? Wamjuao huyo jamaa wanasema ndivyo alivyo ana mentality za kichawichawi yaani kila alipo lazima awachonganishe.
Ila habari za chini ya kapeti ni kuwa MO amekuwa blackmailed kutoa nafasi hiyo na si kwa hiari yake. Sasa wanasimba tumsaidieni kumsemea kuwa hatumtaki Makonda.

Sent using Jamii Forums mobile app
...🤔🤔🤔.duh! ⚽⚽⚽
 
Umezungumza vizuri sana, Cheo alichopata Makonda ni cha kujitolea tu.
Hana mshahala hapa SSC.
Hatii hasara yoyote.
Wala hahitaji chochote toka SSC.
Zaidi anataka kutoa mchango wake kwa timu bure kabisa.
Je sisi SSC hatuhitaji michango ya kujitolea ya wadau wa Simba ?
Kazi za kujitolea huwa hazikataliwagi.
Pia kumbukeni wahenga wanasema.
Adui wa Jana ni rafiki wa leo, na rafiki wa Jana, Leo ni adui."
Msimhukumu mtu miaka yote. Huenda ametubu kuliko Ninyi.
Tumwachie Mungu atuhukumu.
Amina



Sent using Jamii Forums mobile app
Acha unyang'au wew, japo mimi si mshabiki wa simba lakini kumleta bashite ni kujitakia laana katika club yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkataba wako MO Dewji na klabu ya Simba haukuhusisha kutuletea kwenye timu watu upendao/wanaokushinikiza ili wawe sehemu ya timu.
Huwezi kumleta Paulo Makonda ndani ya timu yetu hata kidogo. Makonda ana tuhuma nyingi zinazo gusa maisha ya watu jee kama watu wenye mahusiano na walio umizwa kama ni wanachama au washabiki wa Simba wanajisikiaje?
Mtu mwenye mikono michafu juu ya maisha ya watu anasababu gani kuingizwa timu ya Simba? Unataka kuigeuza Simba ionekane sio Klabu ya burudani na michezo bali ya maumivu na mateso kwa watu?
Hatutaki, hatutaki. Kwanza ushauri katika nini atafit kuutoa huyo? Kila jambo anafeli na kuharibu ndio aje Simba?
Sasa bora tuwashawishi wachezaji wapoteze mechi mbili za Alliance na Coastal ili kukuonyesha hatumtaki Bashite. Au kushawishi mechi ya kesho kuzomewa timu kwa jina LA Bashite hadi utakapo tengua maamuzi hayo yenye mrengo wa siasa, maana pengine umelazimishwa tuu kufanya hivyo na Wasiojulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
hii inanikumbusha Taifa Stars ilivyokuwa kwenye AFCON finals mwaka jana..... Bashite alipojihusisha na timu 75% ya Watanzania walikuwa wana support timu (nchi) pinzani kila zinapocheza na Stars.

Simba naona kimeanza kunuka nako!!
 
Sema sitaki ,Mimi mwanachama wa simba naunga mkono tena ikibidi alete watu wengine influential kabisa Simba inapaswa kuwa taasisi ndani yake yenye watu maarufu kabisa ikibidi hata raisi wetu ,waziri mkuu ,makamu wa raisi wawe washauri wa SSC
Kwani wewe uko timamu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunamuonea huyu baba bure siku ya kuoigwa risasi kwa lissu hakuwa ddm kama mnavosema. Alikuwa kwenye kampeni ya Dar Afya chek ambayo na mimi nilikuwa nahudumu. Hapo hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa akubali kumteua au alikishe zile picha akiwa na kanga .
Bashite ni mafioso
IMG-20200131-WA0202.jpg
 
Kwa hivi sasa Club ya Simba ina mshauri mkuu ambaye anatambulika na Marekani kama gaidi anaye ua watu.
Timu yangu Simba tunakwama wapi?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom