Simba tulifika kibahati 16 Bora Africa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Bahati (chance) ilitumika kuifikisha Simba hatua ya makundi kwenye mashindano yanayoendelea ya CAF. Kubahatisha huku ni dhahiri kutokana na idadi kubwa mfululizo ya magoli inayofungwa na ndugu zake wanaoshiriki kwenye hatua hiyo. Kufungwa sio ajabu kwenye mashindano lakini kufungwa magoli 5 kwa 0 na timu mbili tofauti kunaonyesha kuwa hizo timu sio rika lako bali, umejichomeka tu by chance. Mfano, goli alilofunga Chama kwenye mechi na Nkana lililo ivusha Simba ni la kubahatisha tu na hawezi kufunga tena goli la style ile milele.

TFF inahusika na aibu hii, lazima iingalie ligi yake vizuri kwakuangalia na kusimamia waamuzi, ratiba, makocha, usajili, viwanja na kanuni zinazoendesha soka nchini ili zitoe washindi watakaoweza kwenda kushindana huko mbele ya safari.

Timu inaweza kushindwa Kwa 1-0, 2-1, 3-2 au hata 5-3 au 5-4 lakini sio 5-0 mara mbili na timu mbili tofauti kwenye mashindano husika.

Hii sio aibu kwa Simba tu bali ni aibu pia Kwa TFF, mdhamini wa Simba na Tanzania yote. Hii pia inashusha hata haiba ya bidhaa za mo (mdhamini) kwenye soko

Ikitokea hiv mwenyekiti wa TFF, Simba, kocha lazima wajiuzulu kwa kupeleka timu mbovu (5-0 x 2) kwenye mashindano.
 
Hakuna bahati kwenye mpira
Bahati ipo, unatakà kusema Yanga inayo timu inayoifanya iongoze ligi? Simba kama imefika pale Kwa uwezo basi isingefungwa 5-0 x 2 na timu 2 tofauti za 16 bora. Afadhali kama ingefungwa hivyo na timu moja tu ingekuwa habari nyingine. Kiukweli Simba ingetakiwa itolewe na Nkana siku ile ila bahati ilitumika kwa Chama kufunga bao la akadabla wakaiondosha Nkana. Ona Chama anavyovurunda mechi za makundi hadi anatolewa nje kupisha under dogs. Yale magoli kama aliyoifunga Nkana hadi watu wote wakasisimkwa na kuonekana kama wehu yako wapi?
 
Nakubali kwenye mpira kuna bahati ila sio ya kutilia maanani kwamba bahati itakuvusha.
....Je Kuwafunga Js Soura napo tulibahatisha??..
.... Yote kwa Yote mpira hauendeshwi kwa bahati ndio maana watu wanaweka Pesa zao kwenye mpira sio bahati
 
Nakubali kwenye mpira kuna bahati ila sio ya kutilia maanani kwamba bahati itakuvusha.
....Je Kuwafunga Js Soura napo tulibahatisha??..
.... Yote kwa Yote mpira hauendeshwi kwa bahati ndio maana watu wanaweka Pesa zao kwenye mpira sio bahati

ngaja urudiane na soura huko kwao algeria ndio tutajua ulibahatisha au uliwafunga kwa uwezo...

mechi za marudiano ndizo zitaeleza kama simba ni kikosi kipana au kikosi chembamba
 
ngaja urudiane na soura huko kwao algeria ndio tutajua ulibahatisha au uliwafunga kwa uwezo...

mechi za marudiano ndizo zitaeleza kama simba ni kikosi kipana au kikosi chembamba
Bado haifanyi kuwa tulishinda kwa bahati
Tunampiga Mbambane 4-1 dar, na 4-0 ugenini Tuliwazidi uwezo au bahati?.. Tunampiga Nkana 3-1 dar na ugenini tukala 2-1 agg(4-3) yaani goli 4 tumebahatisha??
Acha unazi basi
 
Bado haifanyi kuwa tulishinda kwa bahati
Tunampiga Mbambane 4-1 dar, na 4-0 ugenini Tuliwazidi uwezo au bahati?.. Tunampiga Nkana 3-1 dar na ugenini tukala 2-1 agg(4-3) yaani goli 4 tumebahatisha??
Acha unazi basi

hao kina mbabane, nkana.. wabahatishaji wenzako.. mziki huko huku wakata viuno na wala harua harua.. tunasubiri marudiano tuone kama una kikosi kipana au una kikosi chembamba
 
Bas wabahatishaji wapo wengi tu 16 bora maanake mwingine kapigwa 8-0 na vijana wa Moise Katumbi.
 
...Mfano, goli alilofunga Chama kwenye mechi na Nkana lililo ivusha Simba ni la kubahatisha tu na hawezi kufunga tena goli la style ile milele....
Aisee, kumbe hii ndio hoja! Haya sawa, ngoja nipite kwanza
 
...Yale magoli kama aliyoifunga Nkana hadi watu wote wakasisimkwa na kuonekana kama wehu yako wapi?
Mkuu, unataka magoli yawe yanafungwa kwa staili ya kisigino kila wakati ndio uhalalishe kuwa sio bahati? Mbona akina Messi na Ronaldo wanafunga mabao kwa staili tofauti zinazobadilika kutokana na jinsi walivyopokea pasi? Nao wakifunga mabao makali wanakuwa wamebahatisha? Yaani nashindwa kupata your point kukomalia goli la Chama
 
Nakubali kwenye mpira kuna bahati ila sio ya kutilia maanani kwamba bahati itakuvusha.
....Je Kuwafunga Js Soura napo tulibahatisha??..
.... Yote kwa Yote mpira hauendeshwi kwa bahati ndio maana watu wanaweka Pesa zao kwenye mpira sio bahati
Kwahiyo Simba ina uzani sawa na As Vita na al haly? Kufungwa 5-0 kunaonyesha kuwa hakuna uwiano kabisa
 
HII SIO AIBU YA TFF, HII NI AIBU YA SIMBA. TATIZO LINALOITAFUNA SIMBA NI BENCHI LA UFUNDI

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly benchi la ufundi. Kufungwa siyo tatizo ila kufungwa tano ni uzembe wa kocha, unaenda Alexandria ukiwa unaujua vizuri uwezo wa timu yetu na unaujua vizuri uwezo wa Al ahly, then unaenda kuattack, unamuqnzishq rashid juma( ambaye alikuwa anapoteza mipira mingi kwa sbabu ya kukosa uzoefu) badala ya kumuanzisha hata mzamiru asaidie kwenye kuzuia. Ningemuelewa sana kama gemu ya dar ndiyo acheze attack gem lakin siyo ile gem.
Pia kocha msaidizi wa vital alisemq kwamba simba tunacheza sana pasi zisizo na maana hasa chama. Mara nyingi anapiga pasi za nyuma na fupi fupi. Kinchotkiwa na kupiga pasi za kwenda mbele ambazo ni zenye madhara jambo ambalo kocha anatakiwa kufanyia kazi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana atukufika kibahati isipokuwa atukujipanga dhidi ya mechi za ugenini na tumekosa mipango ya kujua wapi tutafute ushindi au sare mkuu.

Kwa mfano mechi tuliofungwa na As vita ilikuwa ni kipimo tosha cha kujua cha kwenda kufanya dhidi ya Al Ahlly tutaendaje kucheza open game dhidi ya team kama Al Ahlly na kuruhusu magoli mengi kiasi kile?

Ukiangalia kiundani hatuna mipango ya wapi tukacheze mpira wa kufunguka na wapi tucheze mpira wa kujilinda na kufanya mashambulizi ya kustukiza.

We fikilia tumeenda kucheza mfumo wa kufunguka dhidi ya As vita wakati sisi tulishakusanya point tatu dhidi ya js soura ilitupasa tucheze kimakini kwa kujilinda dhidi ya As vita kwao amabo tunajua ilishapoteza mechi dhidi ya Al Ahlly kwaiyo kivyovyote walikuwa wanahitaji ushindi kwao.

Maana mechi za ugenini kutafuta sare yoyote kufunga ni majaliwa ilitupaswa tutumie mfumo wa 3-5-2 tukiwa tunajilinda na kushambulia kwa kustukiza.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubishi wa kocha umetuponza mkuu.kocha wa nkana alimwambia usiende kwenye ligi ya mabigwa na beki zile lkn mwenyewe amewaamin kubwa walisema wataziba no ya kapombe lkn bado anacheza huyohuyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa, basi angefunga la aina yoyote ile anayoijuwa yeye ilimradi isisomeke 5-0
 
hao kina mbabane, nkana.. wabahatishaji wenzako.. mziki huko huku wakata viuno na wala harua harua.. tunasubiri marudiano tuone kama una kikosi kipana au una kikosi chembamba
simba imevuka hatu ya awali imeingia makundi wewe umekomalia wamebahatisha.
Haina ubishi 16 bora sio mzaha ni moto balaa mpaka uwe umejipanga kweli.
wale makirikiri waliomtoa yanga hatua ya awali utasema wana mpira mkubwa wa kuwasumbua yanga? Au ubovu wa timu zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…