kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Bahati (chance) ilitumika kuifikisha Simba hatua ya makundi kwenye mashindano yanayoendelea ya CAF. Kubahatisha huku ni dhahiri kutokana na idadi kubwa mfululizo ya magoli inayofungwa na ndugu zake wanaoshiriki kwenye hatua hiyo. Kufungwa sio ajabu kwenye mashindano lakini kufungwa magoli 5 kwa 0 na timu mbili tofauti kunaonyesha kuwa hizo timu sio rika lako bali, umejichomeka tu by chance. Mfano, goli alilofunga Chama kwenye mechi na Nkana lililo ivusha Simba ni la kubahatisha tu na hawezi kufunga tena goli la style ile milele.
TFF inahusika na aibu hii, lazima iingalie ligi yake vizuri kwakuangalia na kusimamia waamuzi, ratiba, makocha, usajili, viwanja na kanuni zinazoendesha soka nchini ili zitoe washindi watakaoweza kwenda kushindana huko mbele ya safari.
Timu inaweza kushindwa Kwa 1-0, 2-1, 3-2 au hata 5-3 au 5-4 lakini sio 5-0 mara mbili na timu mbili tofauti kwenye mashindano husika.
Hii sio aibu kwa Simba tu bali ni aibu pia Kwa TFF, mdhamini wa Simba na Tanzania yote. Hii pia inashusha hata haiba ya bidhaa za mo (mdhamini) kwenye soko
Ikitokea hiv mwenyekiti wa TFF, Simba, kocha lazima wajiuzulu kwa kupeleka timu mbovu (5-0 x 2) kwenye mashindano.