Simba tumefungwa lakini nimeridhika

Kuhusu chama, tumefungwa na Yanga Chama akiwepo
 
Kwamba ukusikia tiketi zimepanda bei mzunguko toka huku 3 hadi 10

Kwamba hufahamu watu walikuwa na hofu ya kipigo hasa nyau angalia jukwaa lao hawakujitokeza kabisa

Kuna uwezekano mechi ijayo nyau akajitokeza matola (mganga wa timu) na wengine wachache zaidi
 
Hii ramli itakurudia si muda, Kule stani bakora alisema yanga akimfunga nyau Basi buggati akamtoleee posa kwa bibiake naamini kwa usiku wa leo ameshajifunza kulala Bila chupi
Hujawah kuona na hutoona

Ushindi wako mkubwa vs Simba uliiona ni 2-0
 
Hivi mechi ngapi Chama alizocheza dhidi ya Yanga na matokeo yalikuwa vipi? kuna watu wanaongea hapa utasema Simba alikuwa anashinda wakati Chama yupo Simba matokeo yalikuwa ya kusuasua tu kwa miaka 3 sasa dhidi ya Yanga.
 
Hatuna team hapo, angalia kuanzia kwenye pre-season tunafanya madudu tu.
 
Kutoka washabiki laki 120 mpaka alfu 30 sababu ya kiingilio? basi league viwanja vitakuwa vitupu ikiwa wao kwa wao tu uwanja mtupu wakija kucheza sijui na JKT....
 
Hivi mechi ngapi Chama alizocheza dhidi ya Yanga na matokeo yalikuwa vipi? kuna watu wanaongea hapa utasema Simba alikuwa anashinda wakati Chama yupo Simba matokeo yalikuwa ya kusuasua tu kwa miaka 3 sasa dhidi ya Yanga.
Shida sio Simba kufungwa, shida ni team kuchezwa mpira kama Majimaji.

Au unaona tulicheza mpira kama bingwa mtetezi?
 
Wewe jamaa acha uongo. Kati ya Simba na Yanga ni timu ipi iliyokuwa na maandalizi mazuri ya msimu? Yanga wameenda Morocco hakuna lolote cha maana walichokifanya. Wamerudi Tanzania wamecheza mechi mbili tu za kirafiki ( vs Zanaco na vs DTB) baada ya hapo wameangukia moja kwa moja kwenye mechi mbili za klabu bingwa.
Simba wamekaa Morocco takribani mwezi mzima na huko wamecheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki. Hawakuishia hapo wamerudi Tanzania wakaweka tena kambi Arusha wanacheza tena mechi moja ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya eagle noir. Kisha wakicheza mechi ya kirafiki na timu za Tanzania dhidi ya coastal union na fountain gate. Wakamalizia mechi ya mwisho ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Tp Mazembe.

Unaona kabisa Yanga imeachwa na Simba pakubwa sana kwenye upande maandalizi ya timu hivyo wanaopaswa kunufaika na muunganiko ni Simba zaidi, wanaopaswa kunufaika na match fitness ni Simba
 
Shida sio Simba kufungwa, shida ni team kuchezwa mpira kama Majimaji.

Au unaona tulicheza mpira kama bingwa mtetezi?
Mimi sijali tumecheza vipi muhimu matokeo ukichukuwa point 3 ndio muhimu sio tumepiga sana chenga haisaidii kitu siku zote mshindi tu ndio anakumbukwa sio aliyepiga pass nyingi, ya pass nyingi yanaishia studio tu nje aliyeshinda anafurahia. Turudi kwenye basic ya mpira ushindi sio hizo statics mambo ya kuiga huko corner ngapi, off target ngapi sijui block ngapi hayana umuhimu wowote kwangu binafsi.
 
Matokeo huyapti bila kucheza mpira, otherwise yanakuwa ni ya kubahatisha.

Tukubali tu kuwa jana tulizidiwa.!
 
Maoni yako tu ila hujui kwanini chama aliuzwa hakuna mchezaji wa permanent simba.
Timu ni nzuri tu huwezi kutoa majibu kwa mechi moja au mbili hata ulaya haya hutokea chelsea kapigwa man u pia kagongwa kwa hiyo tuseme timu hizo mbovu zote.
Kama huna uvumilivu usishabikie mpira na usipotoshe watu.
 
Matokeo huyapti bila kucheza mpira, otherwise yanakuwa ni ya kubahatisha.

Tukubali tu kuwa jana tulizidiwa.!
Aliyeshinda jana anastahili kwa sababu ya kacheza na kushinda. Mpira unaweza kupiga pass alfu moja mashuti alfu moja kama hujafunga ni bure tu kuna team hata huko nje wanakaa nyuma tu wakienda mara moja mbele goal. Kwa jana ni Yanga wanastahili pongezi wamepata tulichokuwa tunakita wote. Hongera Yanga
 
Biashara matangazo mzee

Promotion haikufanyika ipasavyo

Msimu ujao wajitahidi katika hilo
 
Jana mtani kaupiga mpira. Yanga amestahili kwa mara ya kwanza kwa hivi karibuni Yanga imecheza vizuri dhidi ya Simba
 
Hapo umenena mkuu, Yanga wamepata walichostahili kulingana na namna walivyocheza.

Tuna haja ya kuongea juhudi kwenye kusuka upya first eleven maana mpaka Sasa tunabahatisha tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…