Simba tumepoteana kuanzia kwa MO mpaka Mashabiki

Simba tumepoteana kuanzia kwa MO mpaka Mashabiki

Simba Kuna ujinga mwingi mpaka inaboa. Watu baadala ya kuwekeza kwa kikosi Cha maana wanawaza uswahili tu. Waliniboa sana
Hao viongozi ni sikio la kufa msimu uliopita waliwasha moto uwanjani South wakati watu wengi Afrika walikuwa wanaitazama Simba kama timu fulani iliyokuwa inayokuja juu Afrika na kutikisa vigogo wa soka wa Afrika huku ikisifiwa kwa aina yake ya kandakanda. Wao wakaiharibu hiyo sifa baada ya kuingiza mambo ya kijinga kabisa ya kishirikina tena hadharani mbele ya kamera kibao za TV.
 
Me naamini tunayoyaona sisi hata viongozi naamini wanayaona, nakumbuka Try again nae alimkubali sana adebayor, inawezekana mahitaji yote ya simba yanapelekwa mezani shida ni MO kutoa hela, nakuhakikishia Ile bodi haiwezi kuja kusema mapungufu ya ndani ila shida ni mwekezaji anatoa hela za mafungu.
 
Kufungwa game mbili za kimataifa kati ya 6 zitakazochezwa si justification ya wao kupoteana, Simba bado wana nafasi ya kufuzu robo fainali, bado wana game 4 wanatakiwa kushinda 3 na droo moja.

Tukutane jioni leo kwa Nkapa. 😀 😀
 
Back
Top Bottom