Simba tunahitaji uniform kutoka Puma, Adidas, Nike au umbro kwa hatua hii Dewji usituangushe

FC Uster, inadhaminiwa Adidas, jezi yetu inauzwa 42,000 (Home), 34,000 (Away) na 28,000 (Alternate). 20,000 (100 Polyester).

Kuna klabu Rwanda inadhaminiwa na Puma jezi yake inauzwa 38,000 kwa pesa TZS.

Santo Domingo de los Colorados ya Ecuador inadhaminiwa na Nike, jezi zake range ni 35,000 to 50,000 TZS.

Jezi nyingi za Yanga SC na Simba SC ni 100 Polyester.
 
Kwenye madili kama hayo nadhani inakuwa ngumu, maana Simba kama taasisi zipo kama nne na zina migogoro
Taasisi huwa zinatengwa katika uhusika. Huwezi kuona Mgogoro wa Simba SC (Michezo) na Simba Araf (Mabati/Saruji).

FC Barcelona (Uhispania) / Barcelona SC (Venezuela). Zote ni klabu kubwa katika mataifa yao.

Kuna Camel 🐪 (Mavazi), Camel 🐪 (Ujenzi/Vifaa) na Camel 🐪 (Petroleum/Engineering) zote ni chapa ya dunia.

Kuna klabu nyingine inaitwa Simba SC?
 
Badala ya kuihimiza Simba itengeneze jezi zake hapa nchini ili iongeze kipato na kutoa ajira kwa watanzania wewe unawaza mambo ya aibu!!!
===
TUJITEGEMEE.

Una akili za kisukuma kuna mdau kasema hivo, wewe unawaza commodity industry wakati wenzako duniani wamehamia digital industry, kuna vitu vinaitwa tender, na biashara ni kutegemeana ndio maana halisi ya biashara kwahiyo jezi za watu 25 zifanye simba ifungue kiwanda au?
 
Sema wewe ndio huna hela.

Siku moja nenda uwanja wa taifa uone kichaa Cha mashabiki kwenye suala la hela
 
Ila kwenye mauzo ya jezi simba inafeli sana
 
Mkuu fuatilia kuna mgogoro fulani wa kimaslahi kati ya pande nne, sasa hilo la udhamini toka kampuni nyingine bila shaka litaingilia maslahi...

I think so...
 
Wanaweza kutengeneza tatizo, Watanzania wengi hatuwezi kununua hizo jezi (ni bei ghali) na wao kama wawekezaji watapata hasara badala ya faida jambo ambalo hawapendi na linawakwaza kutowekeza!
Timu nyingi kubwa jezi zao wanatengeneza Bangladesh kutokana na gharama kuwa ndogo gharama nyingine zinachangiwa na kodi
 
Mnataka kurudi shule nyie mbumbu fc? Uniform kashoneni kwa fundi cherehani, Nike hana Muda wa kutengeneza uniform za shule!!
 
Rejea post namba 15 ya uzi huu.
 
Mkuu fuatilia kuna mgogoro fulani wa kimaslahi kati ya pande nne, sasa hilo la udhamini toka kampuni nyingine bila shaka litaingilia maslahi...

I think so...
Positively!

Ni mgogoro wa chapa Simba, au mgogoro wa kimaslahi ndani ya Simba SC yenyewe?
 
Hahahaha mikia fc katika kikao wakijadiliana kupata udhamini wa Addidas

 
Ipo Congo mkuu ma inacheza ligi kuu
 
Ipo Congo mkuu ma inacheza ligi kuu
Nimeona! Simba FC (Football Club) ya Uganda iliyoanzishwa 1968, Simba F.C (Football Club) ya Rwanda na A.S Simba (Association Football) ya Congo DR iliyoanzishwa 2002.

Tukitazama hapa tunaona ambao wanaweza kuwa na utata ni Simba FC Uganda na Simba F.C Rwanda.

Simba SC (Sports Club) Tanzania yenyewe ndio timu ya kwanza katika hizo kuanzishwa na inachapa tofauti. Hamna yeyote anayemuingilia kimaslahi mwenzake isipokuwa Simba FC ya Uganda na Simba F.C ya Rwanda.

Uingereza zipo Manchester United, Manchester City na Manchester AFC.
 
DUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUH
 
Niliwaza hivyo, jezi zitengenezwe kwa mdaraja ili kila mtu anunue kulingana na uwezo wake na anachokipenda, bei ya rejareja iwe kuanzia 20,000-300,000.

Ni vigumu kumpata mtengenezaji wa jezi kwasababu hakuna udhibiti/protection ya brand logo, watu wanajipritia tu jezi kiholela mfano sasa hivi zimejaa jezi mbovu za visit tanzania madukani tena mpaka mikoani

Ili kuhakikisha timu inapata faida kwanza ni lazima tuondoe
jezi zisizotoka kwenye mfumo rasmi wa club (za kichina) na ukikutwa unauza jezi isiyo rasmi ni kesi ya kutumia logo pasipo na ruhusa ya club.

Tuanzishe mfumo na ku identify and certify mawakala wa kuuza products za simba kila wilaya, mkoa nk mfano wa kuigwa ni mwanza ambapo mashabiki wa simba walifungua duka la kuuza bidhaa official za simba pale kirumba stadium. Mfumo huu utawafaidisha club pamoja na mashabiki kiuchumi na hata matawi yashiriki kuuza bidhaa official za simba
 
Simba ina fanbase kubwa sana hapa tz na hivyo iwapo udhibiti wa jezi holela utafanikiwa mazee hii club ina uwezo wakuingiza bil 10+ kila mwaka na kwanza hao adidas, nike, puma watatufuata wenyewe ni basi tu hatujui thamani ya fanbase tuliyonayo.. naomba hii iwe agenda kuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…