Simba Tundu Lissu: Historia Yake na Je, Unaweza Kumuona Wapi Live Baada ya Kizimkazi?

Simba Tundu Lissu: Historia Yake na Je, Unaweza Kumuona Wapi Live Baada ya Kizimkazi?

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), mnyama anayeongezeka umaarufu sasa nchini ni “Simba Tundu Lissu” alizaliwa Dar es Salaam Zoo, nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam eneo la Mwasonga, Kigamboni.

Alizaliwa Januari Mosi, 2018, hivyo kwa sasa ana miaka 7. Simba huyu ana asili ya Hifadhi mchanganyiko za Mapori ya Akiba ya Grumeti na Ikorongo yanayopatikana katika Mfumo Ikolojia ya Serengeti, Kaskazini mwa Tanzania ambako ndiko wazazi wake walikotokea kabla hawajahamishiwa Dar es Salaam Zoo. Hivyo Simba Tundu Lissu ni “born town.”

“Tabia za Simba Lissu”

“Simba Tundu Lissu” ni mnyama mwenye tabia za kipekee ikiwemo upole na mwenye urafiki kwa wageni wanaomtembelea katika Bustani ya wanyamapori ya Dar es Salaam Zoo. Mara nyingi hujulikana kwa utulivu wake na anaonekana kufurahia uwepo wa watu wanaomzunguka. Hata hivyo, kama ilivyo kwa wanyama wa porini, Tundu Lissu ana silika ya kujihami na kwa nadra anaweza kuwa mkali pale anapohisi maisha yake yako hatarini. Tabia hizi zinamfanya kuwa simba wa kuvutia na anayehitaji kuzingatiwa kwa makini katika mazingira yake.

Taarifa ya TAWA inaonesha kuwa baba yake alizaliwa na kuishi Pori la Akiba la Grumeti karibu na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti huku mama yake akiwa na asili ya maeneo ya Ushoroba wa Tarangire-Manyara na alifahamika baadaye kwa kuishi eneo lililohifadhiwa la Makuyuni (Makuyuni Wildlife Park).

Je, kuna wanyamapori wengine wenye majina ya Viongozi?

Jibu ni ndio wapo wanyamapori nchini wenye majina ya viongozi na wengine wako katika hatua za mwisho kutangazwa. Baadhi ambao wapo tayari na wengi wakiwa ni faru ni hawa hapa:

A: Tanapa:
1. Faru Magufuli
2. ⁠Faru Majaliwa
3. Faru Samia (yupo kwenye mchakato wa mwisho)
4. Faru Ummy Mwalimu
5. Faru Janet Magufuli
6. Faru Balozi Regine Hess

B: Ngorongoro:
1. M6 Faru Pius Msekwa
2. M7 Faru Telele
3. M9 Faru Ndugai
4. M10 Faru OBAMA
5. M14 Faru Sokoine
6. M17 Faru Lemanya
7. F31 Faru Hillary Clinton

C: Tawa:
1. Faru Semfuko
2. ⁠Faru Mabula
3. ⁠Faru Gloria

Kwanini Majina ya Viongozi?

Katika ulimwengu wa sayansi na uhifadhi ni kawaida baadhi ya wanyamapori hai au waliogunduliwa kupewa majina ya wagunduzi au watu mashuhuri duniani wakiwemo wanasiasa, wasanii, wanamichezo na wanasayansi kutokana na sababu mbalimbali.

Utaratibu Tanzania

Nimeuliza katika Mamlaka mbalimbali za uhifadhi jibu ni yes zipo taratibu za mtu kupewa jina lake kwa wanyama au wataalamu kuamua kufanya hivyo kutokana na mchango wa mhusika na sababu nyingine.

Wapo Wafalme kama Charles III wa Uingereza, Bill Clinton, John F. Kennedy, Winston Churchil na wengine wengi ambao majina yao yamekuwa yakitumiwa kuita wanyama wa nyumbani na porini.

“Uamuzi wa Mhe. Rais kumwita Simba huyu Tundu Lissu ni jambo la kawaida katika uhifadhi na sasa Simba huyo ataendelea kutambulika kwa jina hilo kama ishara kwa Lissu na wadau wengine kuendeleza Uhifadhi,” anaeleza Mhifadhi mmoja Mwandamizi kutoka Mamlaka Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
IMG-20240825-WA0036.jpg
IMG-20240825-WA0035.jpg
 
Mama anaitaka sana mitano tena, kwakuwa kwa katiba hii ni lazima atangazwe mshindi basi Lisu atumie hii fursa asikose vyote.

Kama una D mbili huwezi kunielewa.
 
Back
Top Bottom