Simba tuondoe wachezaji kwa heshima

Simba tuondoe wachezaji kwa heshima

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
Katika Miaka Minne ya Simba Imefanya makubwa kwa hiyo hata kama tunawaondoa wachezaji tuwaondoe kwa heshima.

Wamefanya makubwa lakini pia viongozi wa Simba anzisheni mambo ya kusajili wanachama online kama CCM wanavyofanya kwa kiingilio cha 10,000 na kila mwaka tulipe 20,000 na mapato na matumizi yatangazwe kila mwaka. Hii itatupa nguvu sana Simba. Bila kufanya hivi tutaendelea kuwa tegemezi. MO lazima tuwe naye lakini pia hii mhm kuwa na wanachama walio hai.

Wachezaj wafuatao tunaweza kuwapumzisha
  • Mugalu
  • Kagere
  • Bocco
  • Lwanga ni Injury
  • Onyango Umri
  • Mzamiru
Wengine wabaki maana kupata wachezaj wazuri Africa mtihani
 
Nakuunga mkono, Ila hapo kwenye wachezaji wakuachwa tunapishana kidogo- hasa ma- pro- wachezaji wapo tatizo nadhani bajeti ndogo ya usajili- Kama lengo ni kufanya vizuri kimataifa- wachezaji mapro wakubaki ni wawili tu- Enock Inonga- na Clotus Chama.
 
Hao wengine utalipia pesa ya kuvunja mikataba yao na hao wapya utalipia gharams zao?
 
Manura naye atemwe ana makosa yakujirudia mengi.

Banda aondolewe, timu yetu isiwe ya kukuza vipaji
 
Ni mapema sana kustafisha timu nzima, tuwape mda na mapumziko ya kutosha
 
Halafu hizi mashine ziongezwe kwenye kikosi msimu ujao, ili kuongeza idadi ya magoli pale mbele! David Molinga "Falcao" , Super Julio (Namungo) na Ditram Nchimbi! (Mchezaji huru)
 
Ila pia wazee wa SIMBA tumewaaacha sana ndio maana vipigo vya YANGA zinatuandamana
 
Katika Miaka Minne ya Simba Imefanya makubwa kwa hiyo hata kama tunawaondoa wachezaji tuwaondoe kwa heshima.

Wamefanya makubwa lakini pia viongozi wa Simba anzisheni mambo ya kusajili wanachama online kama CCM wanavyofanya kwa kiingilio cha 10,000 na kila mwaka tulipe 20,000 na mapato na matumizi yatangazwe kila mwaka. Hii itatupa nguvu sana Simba. Bila kufanya hivi tutaendelea kuwa tegemezi. MO lazima tuwe naye lakini pia hii mhm kuwa na wanachama walio hai.

Wachezaj wafuatao tunaweza kuwapumzisha
  • Mugalu
  • Kagere
  • Bocco
  • Lwanga ni Injury
  • Onyango Umri
  • Mzamiru
Wengine wabaki maana kupata wachezaj wazuri Africa mtihani
Mugalu abaki tafadhali, hajapata kocha wa kumtumia vizuri. Amekomaa ki mashindano. Atafutiwe mshambulia kabambe mbadala wa Kagere.

Lwanga, Wawa na Onyango sio wa kuachwa kijinga, tutasaga meno, kupata mbadala ni bahati kweli.
Tuachane na makocha wazungu Kwanza.
 
Scouting ya club imepwaya sana, watoke waende nje kuangalia vipaji.

Tunahitaji wachezaji wa kuipambania timu, humu nchini vipaji vipo tuongeze na wa nje ili upatikane mseto hatari.

Miaka 4 tulibweteka hakuna muendelezo mzuri wa kuleta wachezaji, lazima wengine watoke alafu damu mpya ziingie kuongeza chachu ya ushindi.
 
Kolo nawashauri. Ondoeni wachezaji ila mbakize 50% au 60%. Mkiondoa 80% mtapata tabu sana. Itawachukua 5 seasons kupata kikosi. Hamjajifunza kwa yanga?
Wakupunguza ni 10% tuuu. Tatizo sio wachezaji kaka, ni menejimenti ya wachezaji tuuu.
 
Back
Top Bottom