Simba UKAWA wapata ajali,watu watano wafariki

Simba UKAWA wapata ajali,watu watano wafariki

Habari hii ni kweli kabisa. Niliisikia Radio One saa moja jioni hii,ikiwa ni breaking newz, walilazimika kukata matangazo ya Dira ya Dunia-BBC.Ni maeneo ya Morogoro barabara ya Moro- Dodoma. Gari lao liliacha njia na kupinduka na kuua abiria 5 na kujeruhi kadhaa
 
Poleni sana SIMBA UKAWA

11080474_1578575822390731_4950177005912400476_o.jpg
 
Niliwaona pale Kimara leo wakiondoka ilikuwa saa 6 mchana na mavuvuzela yakipulizwa kwa nguvu zote. R.I.P marehemu wote
 
Dah! poleni jamani,japo kazi ya mungu haina makosa lakini inauma sana jamani,mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema.
 
Dah!!!! Mungu watie nguvu ili wapone haraka wale waliojeruiwa na uwapokee kwa mikono yako mitukufu wale wote waliotangulia mbele ya haki.
 
Poleni sana watani, ktk hili tuwe pamoja na tuweke pembani utani wetu.
Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wa ajali na kuwapa pimziko la milele marehemu, pia moyo wa faraja kwa familia zao na club ya simba.


"Yanga bila Simba raha ya soka Tza haipo"

Utani hauna mwisho,,upo mpakakwenye msiba
 
Poleni sana klabu yangu kwa msiba huu tupo pamoja, tofauti tunaziweka pembeni.
 
R.I.P

Inasikitisha sana.

Mungu uwajaalie majeruhi wote wapate nafuu ya haraka.
 
Inaumaa sanaaa poleni sana wafiwa na Mungu awape majeruhi wapone haraka
 
Dah....yaan ajali hizi kwakweli Mungu atusamehe sn tulipokisea.
Wiki moja uliyopita ajali imeondoka na kipenzi changu,nikisikia ajali tena akili yangu inakumbuka hiyo ajali iliyoniulia baba watoto wangu.
Rip baba na wote marehem wa ajali.
 
Usaliti mbaya sana, kutaka kumuaibisha mwenzako ni vibaya sana, ubinafsi mbaya sana, kiburi ni mama wa ujinga, R.I.P marehemu Mungu awape nafuu majeruhi, poleni sana wafiwa.
 
R I P marehemu wote, na majeruhi Mwenyezi Mungu awape afueni.
poleni Simba Ukawa tawi la Mpira Maendeleo.
poleni wana simba wote na wapenda mpira wote.
 
Back
Top Bottom