Simba vs Everton itaonyeshwa channel gani hapa bongo

Ukweli simba lazima watafute mbadala wa okwi, bocco na kichuya hawa watu wasipokuwepo Simba inapata taabu sana ya ushindi. Kwahiyo naiona Gor Mahia wakienda UK.
Kichuya anajituma lkn wale aliozoea akiwapa mapande wanamaliza hawapo.
 
Mechi mbili Gor Mahia kashinda ndani ya dakika 90. Simba katoa sare lakinu kapenya kwa matuta. Bado tunajiuliza nami anaenda Goodison Park?
 
Naona nafasi ya simba ndogo sana kuifunga Gor mahia
 
Mkuu
Mkuu simba kama madrid. Wakiona kombe uwanjani hakuna wa kimzuia
Any has a chance to win that game na hasa kwa mpira walioonyesha Gor leo,Wapo vizuri.Simba huko mbele si wazuri na sijui kwa nn akina Boko hawajaenda Kenya.Au usupastaa?Kila laheri kwa Chama langu Simba Tho
 
Me mshabiki wa Simba ila kwa jinsi nilivoona game zilivochezwa basi Gor mahia anashinda hii game.
 
Gor Mahia vs Simba itakuwa mechi tamu sana labda uwanja uharibu ladha kama uliwaharibia Singida.
Mabingwa hawa wa Kenya unaweza kudai ndio timu bora so far lakini watakutana na wahenga wenzao na bila shaka timu zote zitaulizana 'maswali magumu'.

Ubora wa Simba umebadilika sana siku hizi.....HAIHITAJI kucheza mpira mazuri ili kupata matokeo. Hili ndilo suala muhimu wakenya pamoja na mashabiki wao wanapaswa kulizingatia. Lakini je Simba itaweza kuizuia Gormahia isifunge goli hata moja kwa dkk 90 zote? Wakenya hawa wana wastani wa kufunga goli moja kila baada ya dkk 36 za mchezo.

Achana na ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo kila mwenye kujua mpira anafahamu ni kutokana na kupanguliwa kwa mfumo wa ushambuliaji uliojengwa kuwazunguka Okwi na Bocco, lkn kitu kizuri ni kuwa taratibu washambuliaji wapya wanaendelea kuelewana taratibu na unaona mechi ya pili wameonesha kitu tofauti na mechi ya kwanza na bila shaka mechi ya fainali wanaweza kuoenyesha kitu kikubwa zaidi kuliko zilizotangulia.

Timu yoyote itakayopata bao la kwanza ndio itakayochukua ubingwa kwa sababu, kama Simba atapata bao, defence yao chini ya Manula ni roho ya paka, lakini kama Gormahia watapata bao la kwanza, uwezo wa Simba kukuomboa bao ni mdogo sana.

Uzuri mchezo wa mpira haunaga utabiri na ndipo utamu wake ulipo.
 
Hiki ndio kiliwachowaponza mikia mwaka ule wanacheza na Stella Abijan. Badala wajadili mikakati ya ushindi wao wako bize kujadili kombe watalipitisha ruti gani.
 
Naipenda Simba Mshabiki wa Damu , ila kwa foward ya mech mbili bila kufunga goli hata moja kuna shida Mahala.
 
Huyu mleta mada kashatia nuksi fainali yetu
 
Simba hata wakishinda hawawezi kupewa visa ya UK..wana historia ya wachezaji wao kukimbia Ulaya..Ferouz Teru yuko Denmark alijilipua ...balozi zote wanazo hizi taarifa
 
Naona mechi inanukia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…