Gor Mahia vs Simba itakuwa mechi tamu sana labda uwanja uharibu ladha kama uliwaharibia Singida.
Mabingwa hawa wa Kenya unaweza kudai ndio timu bora so far lakini watakutana na wahenga wenzao na bila shaka timu zote zitaulizana 'maswali magumu'.
Ubora wa Simba umebadilika sana siku hizi.....HAIHITAJI kucheza mpira mazuri ili kupata matokeo. Hili ndilo suala muhimu wakenya pamoja na mashabiki wao wanapaswa kulizingatia. Lakini je Simba itaweza kuizuia Gormahia isifunge goli hata moja kwa dkk 90 zote? Wakenya hawa wana wastani wa kufunga goli moja kila baada ya dkk 36 za mchezo.
Achana na ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo kila mwenye kujua mpira anafahamu ni kutokana na kupanguliwa kwa mfumo wa ushambuliaji uliojengwa kuwazunguka Okwi na Bocco, lkn kitu kizuri ni kuwa taratibu washambuliaji wapya wanaendelea kuelewana taratibu na unaona mechi ya pili wameonesha kitu tofauti na mechi ya kwanza na bila shaka mechi ya fainali wanaweza kuoenyesha kitu kikubwa zaidi kuliko zilizotangulia.
Timu yoyote itakayopata bao la kwanza ndio itakayochukua ubingwa kwa sababu, kama Simba atapata bao, defence yao chini ya Manula ni roho ya paka, lakini kama Gormahia watapata bao la kwanza, uwezo wa Simba kukuomboa bao ni mdogo sana.
Uzuri mchezo wa mpira haunaga utabiri na ndipo utamu wake ulipo.