Simba Vs Majimaji

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Ni kombe la FA kesho saa moja usiku uwanja wa mkapa ambapo mtaalamu mzungu wa simba toka ubelgiji Sven Vaan Debroeck ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa simba anatarajia kucheza wachezaji wasiopata nafasi mara kwa mara

Kikubwa ni kwamba ule mfumo wake pendwa anaotumia iwe ni mechi kubwa au ndogo yaani 4-2-3-1 unatarajiwa kutumiwa
hivyo tutarajie simba itakayokuwa inacheza kwa tahadhari kubwa huku ikijilinda shidi ya majimaji ya songea

Mfumo huo pia unatarajiwa kutumia tarehe 6 katika mechi ya marudiano na platnum ya zaimbabwe..MFUMO HUO PIA UNATARAJIWA KUTUMIWA TENA NA TENA NA TENA NA TENAAAAAAA hata katika mazoezi, ni mfumo pendwa wa mtaalamu sven.
Inasemekana hata akiwa kalala usingizini huwa anaota kwa sauti na kuutamka mfumo huo huku akitabasamu kwa bashasha

kikosi kinatarajiwa kuwa..
kakolanya,duchu,gadiel,kennedy,ame,ndemla,miraji,muzamiru,bwalya,ajibu,kahata.
 
Basi simba anaweza kupigwa hii game tusiamini sijui tatzo nini cc green warriors,mashujaa
usijali mtaalamu sven ataingia kwa kujilinda na kwa tahadhari,mshambuliaji mmmoja mbele kama kawaida
 
Basi simba anaweza kupigwa hii game tusiamini sijui tatzo nini cc green warriors, mashujaa
kuhus green warriors sijui ila mashujaa nusu ya wachezaji walikuwa wamelewa pombe, dida alitapika kwenye basi kabisa baada ya mechi
 
Kwani tatizo la Simba Ni kutocheza na mastrikers wawili au Aina ya uchezaji wa Simba?
 
Kwani tatizo la Simba Ni kutocheza na mastrikers wawili au Aina ya uchezaji wa Simba?
sijui boss we unaona tatizo ni nini?aina ya uchezaji si ndiyo mfumo au?hujui mchezaji akienda kinyume na maelekezo ya kocha ni jinai?kwa mfanao kama kocha hataki wajaribu mashuti nje ya 18,kona ziwe fupi n.k...
 
Wangemaliza viporo vya ligi kabla havijachacha
 
sijui boss we unaona tatizo ni nini?aina ya uchezaji si ndiyo mfumo au?hujui mchezaji akienda kinyume na maelekezo ya kocha ni jinai?kwa mfanao kama kocha hataki wajaribu mashuti nje ya 18,kona ziwe fupi n.k...
Nyinyi ninawashangaa Sana kulalamika eti kocha hachezeshi mastrikers wawili wakati Kuna wakati anawapanga wote na ailipi ndio maana kachagua kwenda na striker mmoja.Tatizo kubwa la Simba sio Hilo Bali wapo very slowly kwenye build up pia Wana weakness kwenye defense line hata awachezeshe mastrikers wawili Kama hawatabadilika kiuchezaji it will not work
 
hakuna shida boss si ndiyo maana hata kesho nimesifia mechi ya majimaji ya kwamba tutacheza kwa tahadhari huku tujilinda?ishajulikana kwamba mfumo wa kudumu wa simba ni 4-2-3-1 msimu mzima so its all good,naskia teams zote za kisasa duniani zinacheza hivyo
 
Mechi kesho afu ...unaletea Live Updates🙄 leo
hujawahi ona?ndo utulie sasa live updates hata kama jonas mkude akionekana sasa hivi ile mitaa yake ya kawe anakunywa konyagi na kuvuta bangi kisha kesho akipangwa vijana wa majimaji wanapita katikati pale kwa kasi za chikwende au kisila ukimuona WEWE WEKA TU NI LIVE UPDATE..SAA MOJA KESHO ITAFIKA TU..kishingo ,master wa soka la kisasa Tanzania ataingia na 4-2-3-1 akicheza kwa tahadhari dhidi ya wakali wa zamani wa soka tanzania majimaji mabingwa wa ligi ya muungano 1998
 
Majimaji watacheza nayo akina Salim na akina Duchu. Watu Wazima wanatafakari mechi ya Platinum Utopolo FC
 
Mimi nakumbuka Majimaji aliku bingwa 1995 . 1998 bingwa ilikuwa timu moja kati ya hizi tatu.

Yanga,Malindi au African Sports
 
Tatizo la Simba ni kucheza taratibu.. Timu ikiwa wachezaji hawajitumi vilivyo kukaba.
 
Huyo Vani Dar Buruku ndo kipenzi cha Wanasimba? Kweli wewe una njaa Kali Hatari.!!
 
hivi simba mfumo wake hasa ni upi? na alioutumia wakati anacheza na Chikwende ni upi?
 
Ulikuwa na kocha Nini mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…