Simba vs Planteau: Napendekeza iwe sharti kuwa hakuna kuingia bila jezi za Simba

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Naomba uongozi wa Simba hii mechi inayokuja watangaze kabisa kabla watu hawajanunua tickets kwamba hakuna kuingia bila jezi ya Simba au nguo nyekundu, itangazwe kwamba hakuna kuingia ukivaa njano, hatutaki wasaliti kwenye mechi hii.

Ijulikane mapema kama utavaa njano huingii getini, wapo wahuni watavaa Simba kwa juu wakiingia watavua, wajulishwe njano ikionekana uwanjani unatolewa, mechi ya Simba halafu wavae madera ya njano na kijani kushangilia wageni.
 
Hata Uwanja ingekua Ule wa MO, Yanga wangeingia tu hakuna wa kumzuia Mwananchi labda mkacheze nje ya nchi hii. Wananchi tupo wengi sana, yaani mlipo tupo na tunapotaka jambo letu hakuna wa kutuzuia.
 
Hizo jezi za Simba zagawiwa bure?
 
Haya mawazo ya Kijima hayawezi kutolewa na shabiki wa timu kubwa Kama Simba, wewe ni shabiki wa Vwawa United.
 
Mkitaka hvyo nendeni kachezeeni mechi kwenye uwanja wa mdosi wenu Mo Arena ila Kwa Mkapa hamuwezi mpangia mtu
Hakika umenena
Waambie hiyo jeuri wakafanyie Mo Arena sio Taifa
 
hata huko Europe hauwezi kuta timu hasimu zinafanyiana hivi. Hii ni zaidi ya chuki mkuu. Mpira ni mchezo wa fair play. Tukifika hatua hii kuna siku tutauana kisa nimevaa jezi ya njano au kijani na kuingia kuangalia mechi ya Simba.
 
Acha manyani wachangie mapato, mpira unachezwa uwanjani. Cha msingi Simba ajitahidi asonge mbele, wao wenyewe watajikuta wanavua madera yao
 
Kwa kifupi tiketi ziuzwe kwenye matawi ya Simba akija utopolo asipewe tiketi kama wanataka kuangalia mechi za kimataifa waangalie kwenye tv wako kama wachawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…