Simba vs Yanga April 19, 2009

Simba vs Yanga April 19, 2009

Dah! ingependeza kweli Simba wangeshinda..Leo naona game yetu haionekani kwa ma dish yetu uchwara ila ningependa kuona kikosi cha SAF mana sura mpya kibao
 
hahahahahaha "furaha ya nyani imeishia jangwani"

poleni sana wekundu. sasa mambo ya caf ndio vipi tena?
 
Utabiri wa shehe Yahaya ni feki kwani Simba na Yanga zimetoka nguvu sawa goli mbili kwa mbili.
 
Simba na Yanga leo zimetoka nguvu sawa, huku kila upande ukitegemea ushindi. Hii ni dalili kwamba timu hizi mbili zimekamiana vya kutosha.
 
Sheikh aliona 2-1 wenzake wanageuza game uwanjani...kamuulizeni mtasikia utetezi wake...
 
Ila Simba kwa kuloga nimewavulia kofia....jana wameloga pale kati kati ya uwanja kabla ya game kuanza...
 
Inabidi tufanye sensa ili kujua kuna Yanga kandambili wangapi 🙂

Ni kweli maana hadi Mkuu wa jamvi 😕; hivi yale maendeleo ya mtandao wao (yanga) yaliishia wapi?au ilikuwa ni mambo ya zimamoto kama kawaida ye2 waTZ??
Kwa upande mwengine inafurahisha kuona kumbe wanaJF nao wanafuatilia gozi la home; always, home is home
 
Ila Simba kwa kuloga nimewavulia kofia....jana wameloga pale kati kati ya uwanja kabla ya game kuanza...
Ulijua je kama wana loga au na wewe ni mwanga...kama nikuloga basi yanga ndiyo mliloga maana marefa walikuwa wana wapendelea sana au mliwapa kitu kidogo hawakujua hata muda ulishaisha wa kucheza mpira mpaka yanga alipo sawazisha....na kama hamkuwa loga au hamkuwapa kitu kidogo basi tz hutuna marefa....ila simba nafsi ya pili inatuhusu na soka jana tumelitandaza ukitaka kuamini uliza aliyefika uwanjani au fanya leo ni Jmosi halafu kesho ukalione pambano...daaaaaaaaaaaaaah simba noma sema tu ukeli.... Boban ongeza bidii hata kama "Maximo" asipokuita timu ya taifa
 
Ni kweli maana hadi Mkuu wa jamvi 😕; hivi yale maendeleo ya mtandao wao (yanga) yaliishia wapi?au ilikuwa ni mambo ya zimamoto kama kawaida ye2 waTZ??

Aaah Mkuu, yale mambo ya webusaiti ya Yanga ilikuwa ni njia tu ya kumchomolea YM vihela, si unajua wabongo walivyo mahiri kwa kupropose projects? Sasa ukiona kimya ujue hela ziko mbali kidogo !!
 
Bottom line kwa msimu wa Ligi wa 2008/09 YANGA imekuwa kidedea na SIMBA wamekuwa wateja mwaka huu... Ikumbukwe kuwa mechi ya mzunguko wa kwanza alipigwa mtu bao na wikendi iliyopita ilikuwa sare!!!

Vijana wa Jangwani kazi nzuri kazeni buti... Lakini watani eti bingwa wa Ligi anakula pointi zaidi ya 50 anayefuata anatambaa na kwenye 30s, aibu au ndio soka hii??
 
Vijana wa Jangwani kazi nzuri kazeni buti... Lakini watani eti bingwa wa Ligi anakula pointi zaidi ya 50 anayefuata anatambaa na kwenye 30s, aibu au ndio soka hii??

Mi nadhani ubingwa ni tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa Afrika. Sasa kama mtu unakuwa bingwa halafu unaishia raundi ya awali, itakuwa hivyo hadi lini? Ifikie kipindi Yanga nao wazifunge timu kubwa kubwa za Afrika kama Simba ilivyowahi kuzifunga Ismailia, Arab Contractors, ASEC Mimosas, Enyimba na Ajax Cape Town. Sio kuivurumishia mabao timu ya Shelisheli halafu unakuja kusema wewe ni mwamba!!
 
Mkuu invisble mlitutesa ila mchawi mlieenda trip hii msimwache
 
Mi nadhani ubingwa ni tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa Afrika. Sasa kama mtu unakuwa bingwa halafu unaishia raundi ya awali, itakuwa hivyo hadi lini? Ifikie kipindi Yanga nao wazifunge timu kubwa kubwa za Afrika kama Simba ilivyowahi kuzifunga Ismailia, Arab Contractors, ASEC Mimosas, Enyimba na Ajax Cape Town. Sio kuivurumishia mabao timu ya Shelisheli halafu unakuja kusema wewe ni mwamba!!

Mkuu Opaq..., nimekupata lakini hapa ishu sio kucheza ligi ya nje bali ni kuwapiga bao Simba....... Kwanza tukubali kwamba kwa Bongo kwa muda huu Yanga ni kiboko, kisha tuangalie tunajipanga vipi kwenye so-called michezo na timu kubwa... ila usisahahu Mkuu kuwa Yanga nayo ni timu kubwa sababu imeifunga Simba ambayo imezoea kuzifunga timu kubwaa..... ha ha haaaaa......

Wallahi kwetu sisi wanaYanga huu ni mwaka mkubwa sana na wa baraka kibao.....
 
Ukiboko wa Yanga wa kubebwa fisadi Manji (anayehonga kuanzia wachezaji wa timu pinzani hadi marefa) wala haunogi.
 
Bottom line kwa msimu wa Ligi wa 2008/09 YANGA imekuwa kidedea na SIMBA wamekuwa wateja mwaka huu... Ikumbukwe kuwa mechi ya mzunguko wa kwanza alipigwa mtu bao na wikendi iliyopita ilikuwa sare!!!

Mkuu uteja sio ushindi wa mechi moja...unakumbuka mara ya mwisho yeb....ops sorry Dar Young Africans kuifunga Simba (kabla ya mechi ya kwanza mwaka huu)? Hebu refresh kumbukumbu zako halafu utajua maana ya uteja.
Ninachoona kwa sasa ni timu isiyo na future (Yanga).
 
Yanga hawana cha kujilinganisha na Simba, ni sawa na mbwa anaefokea uani akitoka nje anafyata mkia.
 
Back
Top Bottom