Simba Vs Yanga,January 4: Show ya 5 bila kujirudia

MIE NITAKUWA NAMWANGALIA LAMINE MORO ANAVYOSABABISHA PENATI
 
Mie ni Simba, mechi hii naiona sare ya bila kufungana au sare ya goli moja. Kwanini nayasema haya. Simba wanacheza mpira wa pasi fupifupi ila za polepole sana kiasi ambacho ni rahisi kuwadhibiti hasa kwa timu yenye walinzi wazuri na wazoefu kama wa Yanga.

Simba hawachezi mpira kwa ari na jihadi, wanacheza kiulaini sana. Kingine ambacho bado hawaja kimudu sana ni uwezo wa kupasiana mpira kwa usahihi bila kukosea sana (passing accuracy), wanapoteza sana mipira.

Nawaona Yanga wakibana nafasi na kutumia counter attacks na hivyo kuwasumbua sana mabeki wa Simba hasa wa kati kama Wawa na Nyoni ambao wapo slow kiasi fulani.

Pia Simba haina forward nzuri sana kwa sasa, ukiacha Miraji ambae sijamuona kwenye mechi kadhaa, yeye ana uwezo mkubwa wa kukimbia na mpira na kupunguza mabeki, Kagere yeye uwezo huo hana na akikabwa itakuwa ndio shida kidogo.

Kwa mtazamo huo nadiriki kusema kuwa naiona sare siku ya jumamosi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hapo mwisho ndo ulipo haribu either kwa kukariri au kwa kutokufuatilia mechi za simba, Kwenye mechi NNE za mwisho simba imefunga magoli 14 Kwenye hayo magoli Kagere kafunga Mawili.
Leo hii simba haichezi kwa kumzunguka Kagere, wanavyocheza simba inawafanya hawa viungo washambuliaji wawezi kufunga magoli, ndo mana saizi unamuona Kahata anafunga, Deo anafunga, HD anafunga.
Njia pekee ya yanga kuizuia simba ni kuwafanya viungo wa simba wa kati wasicheze.
Swala la matokeo hilo tunaziachia dk 90,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mechi zote walizoshinda magoli 14 nimewaona, kumbuka jumamosi hawachezi na AFC Arusha wala Ndanda FC wanacheza na Yanga.

Yanga ni wazuri na kwa sasa kwenye msimamo wa ligi ni wa 2 au tatu. Yanga wana mabeki wazuri na wanapenda kucheza mpira wa pasi ndefu na mbio nyingi. Nawaona Yanga wakikaba nafasi na kuwafanya Simba kupiga square passes nyingi ambazo zinapoteza muda.

Ningependa kuwaona Simba wakicheza pasi za haraka haraka (kama Al Ahly) na sio za polepole kama wanavyocheza sasa. Wakifanya hivyo watawafanya Yanga kushindwa kujipanga vizuri na kuacha nafasi za kupiga penetration passes.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale Wakubet wenzangu tuliokua tukibet Simba Win & 2+ kama kawaida hii mechi ni hela kabisa,
Yaani naona kabisa Mhindi akifilisika this time
 
Huto tujamaa ulitotutaja twote tunavifunga vitimu vya ajabu ajabu. #04Jan2020kipimohalisi
 
Kwani ukisema we ni Yanga hutoeleweka?
 
Simba mtajisifu sana, lakini hakuna foward mwenye uwezo wa kuipenya ngome ya Yanga, simba watakachofanya ni kupiga pasi zisizokuwa na malengo katikati ya uwanja , lakini kufunga sahauni,
 
Simba mtajisifu sana, lakini hakuna foward mwenye uwezo wa kuipenya ngome ya Yanga, simba watakachofanya ni kupiga pasi zisizokuwa na malengo katikati ya uwanja kuwafurahisha washabiki wao , lakini kufunga sahauni,
 
Simba mtajisifu sana, lakini hakuna foward mwenye uwezo wa kuipenya ngome ya Yanga, simba watakachofanya ni kupiga pasi zisizokuwa na malengo katikati ya uwanja kuwafurahisha washabiki wao , lakini kufunga sahauni,
Hadi sasa Yanga imeruhusu magoli 8 Kwenye mechi 11 wakati simba imeruhusu magoli 3 Kwenye mechi 13.
Idadi ya point za Yanga 24 sawa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ya simba 24.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tarehe 4 zikipungua Sana basi ni goli 6 bila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…