Simba wa Teranga: Kikosi cha dhahabu kilichotikisa Dunia

Mi nakumbuka F.Batezi anageuka kuurukia mpira ulioingia golini tayari...Angalia kwenye taarifa ya habari ITV ya saa mbili usiku kipengele cha habari za michezo utaona hicho kipande.
poapoa mkuu
 
Siki zote namsikitia fadiga.. maradhi ya moyo yalimnyima nafasi yake ya kufika mbali japo jamaa mpira alikuwa akiuujua sana
 
Huyo Goalkeeper Tony Silva alifanya kazi ya hatari
 
Lile goal la Senegal dhidi ya ufaransa lilikuwa matata sana nakumbuka kuna kituo kimoja cha Runinga kama sio ITV walikuwa wanapenda sana kulionyesha
 
Ila zile dakika Za Mwisho siku wanacheza Na Ufaransa zilikuwa Za hatari mno Ufaransa ilipiga mpira mkubwa ikiwa imesheheni vipaji vyote lakini wapi mpaka mwisho Wa Afrika wanaibuka naushindi wa goli Moja.
Hicho ndio kipindi watangazaji akina Ezekiel Malongo walijipatia umaarufu. Ila goli la Dhahabu lilikuwa linaudhi
 
Huyo Hassan Sassi Mechi Za makundi alipiga bonge la goli Na Brazil japo Brazil walisawazisha Na kuongeza moja.Kipindi hicho Brazil kumesheheni wazee wa Kazi,Cafu,Roberto Carlos,Rivaldo,Ronaldihno ndio anapata Umaarufu,Ronaldo Original,hatari tupu
 
Nakumbuka Niko darasa LA 6 na ndio tumenunua TV home, ilikuwa poa sana
We hukuwa unamsikiliza Ezekiel Malongo Na akina Sued Mwinyi?Mpira upo katikati ya Uwanja anaanza kusema Lal Lal lal go go go anakosa pale Henry Camara
 
Mi nakumbuka F.Batezi anageuka kuurukia mpira ulioingia golini tayari...Angalia kwenye taarifa ya habari ITV ya saa mbili usiku kipengele cha habari za michezo utaona hicho kipande.
Ufaransa ya 2002 ilikuwa Na gundu,nadhani 1998 huenda walifanya dhulumati,2002 waliishia makundi kama sikosei group lao walikuwa wa mwisho
 
Hivi Waingereza wanamsahau Ronaldihno?
 
Senegal walikuwa wanacheza Na Waafrica wenzao waliopata uraia Ufaransa.Maana ile timu ya Ufaransa ilijaa ngozi nyeusi balaa.Hivi Thuram alikwepo kwenye Kosi la Ufaransa,Kumbukumbuku zinapotea kidogo?
 
Umenikumbusha bigijii zenye stika Za wachezaji
 
Ufaransa ya 2002 ilikuwa Na gundu,nadhani 1998 huenda walifanya dhulumati,2002 waliishia makundi kama sikosei group lao walikuwa wa mwisho
Licha ya kutoka mapema kwenye Kombe la Dunia, Ufaransa ilikuwa imesheheni mastraika wa nguvu.
Thiery Henry alikuwa mfungaji bora EPL
Djibril Cisse alikuwa mfungaji bora ligi ya Ufaransa
David Trezguet alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Italy.

Lakini hawakufua dafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…