Simba wa Teranga: Kikosi cha dhahabu kilichotikisa Dunia

Simba wa Teranga: Kikosi cha dhahabu kilichotikisa Dunia

Mi nakumbuka F.Batezi anageuka kuurukia mpira ulioingia golini tayari...Angalia kwenye taarifa ya habari ITV ya saa mbili usiku kipengele cha habari za michezo utaona hicho kipande.
poapoa mkuu
 
Kocha wa hiko kikosi alikuwa Marehemu Bruno Metsu.

Hapo kikosini nawakumbuka golikipa Tony Silva, Captain Aliou Cisse ambaye kwasasa ndiye kocha mkuu wa kikosi hiko, pia Ferdinand Coly huyo jamaa mwenye rasta.

Kiungo matata kabisa aliyestafu mpira mapema kutokana na matatizo ya moyo, Khalilu Fadiga mwenye jezi namba 10.

Pia kuna Salif Diao namba 15, Henry Camara mwenye namba 7, Beki ya kulia Omar Daf mwenye namba 2.

El Hadji Diouf mwenye 11, na Papa Bouba Diop mwenye 19 ambaye aliwagunga Ufaransa kwenye mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia.

Pia walifungwa na Cameroon katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2002 kwa mikwaju ya penati.

Miaka ya 2000 ilikuwa ni wakati mzuri kama mshabiki wa soka kufatilia soka kutokana na uwepo wa kikosi kama hiki.

Ahsante mtoa mada kwa kutukumbusha mbali.

cc: Guasa Amboni
Siki zote namsikitia fadiga.. maradhi ya moyo yalimnyima nafasi yake ya kufika mbali japo jamaa mpira alikuwa akiuujua sana
 
Mechi ya ufunguzi dhidi ya bingwa mtetezi wa Kombe la Dunia, Senegal anamfunga Ufaransa iliyotimia goli 1-0 na kuendelea hapo safari ikawa ni nzuri mpaka walipotolewa na Uturuki kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2002 pale Korea Kusini na Japan. Unakumbuka kikosi hiki? Unakumbuka matukio gani kuhusu kikosi hiki? Karibuni wadau mtiririke
in-japan-und-korea-osaka-match-60viertelfinalesenegal-tuerkei-01-nv-picture-id52836745
Huyo Goalkeeper Tony Silva alifanya kazi ya hatari
 
Hii ilikuwa Senegal bora kabisa iliyowahi kutokea.
Nakumbuka game ya kwanza World cup wanakutana na mabingwa watetezi Ufaransa, game inapigwa majira ya saa nane kwa saa za kwetu.
Diof anapiga cross matata kutoka kona ya kushoto, mabeki wa Ufaransa wanazembea, Barthez anapotea na Senegal wanapata goli la kwanza.
Wanakwenda kutolewa na Uturuki nakumbuka goli linafungwa na Hassan Sassi baada ya beki za Senegal kumsahau jamaa.
Hiki kilikuwa kikosi cha dhahabu.
Senegal ilikuwa na kipa bora kabisa
Kina Henry Camara
Lile goal la Senegal dhidi ya ufaransa lilikuwa matata sana nakumbuka kuna kituo kimoja cha Runinga kama sio ITV walikuwa wanapenda sana kulionyesha
 
Ila zile dakika Za Mwisho siku wanacheza Na Ufaransa zilikuwa Za hatari mno Ufaransa ilipiga mpira mkubwa ikiwa imesheheni vipaji vyote lakini wapi mpaka mwisho Wa Afrika wanaibuka naushindi wa goli Moja.
Hicho ndio kipindi watangazaji akina Ezekiel Malongo walijipatia umaarufu. Ila goli la Dhahabu lilikuwa linaudhi
 
Yaah waafrika tulitolewa na turkey iliyo kuwa na vipaji kama nyanda rustu recber akina hakan sukur na pia hassan sas winger machachari huyu wa gala pia alikuwepo muzzy izzet ukiachilia mbali umit davala ambae alitia majalo nasi kufungwa bao.Tony sylva akina papa malick Diop habib beye (huyu alikuja staafia uingereza nadhani Doncaster pia selif diao ambae aliambatana na elhadj diof pale Liverpool bila kumsahau winga mtata khalilou fadiga (mwizi wa cheni )hakika umenikumbusha kitu japo ni juzi tu miaka 15 imepita toka tukio hilo lichukue nafasi.
Huyo Hassan Sassi Mechi Za makundi alipiga bonge la goli Na Brazil japo Brazil walisawazisha Na kuongeza moja.Kipindi hicho Brazil kumesheheni wazee wa Kazi,Cafu,Roberto Carlos,Rivaldo,Ronaldihno ndio anapata Umaarufu,Ronaldo Original,hatari tupu
 
Nakumbuka Niko darasa LA 6 na ndio tumenunua TV home, ilikuwa poa sana
We hukuwa unamsikiliza Ezekiel Malongo Na akina Sued Mwinyi?Mpira upo katikati ya Uwanja anaanza kusema Lal Lal lal go go go anakosa pale Henry Camara
 
Mi nakumbuka F.Batezi anageuka kuurukia mpira ulioingia golini tayari...Angalia kwenye taarifa ya habari ITV ya saa mbili usiku kipengele cha habari za michezo utaona hicho kipande.
Ufaransa ya 2002 ilikuwa Na gundu,nadhani 1998 huenda walifanya dhulumati,2002 waliishia makundi kama sikosei group lao walikuwa wa mwisho
 
Mwaka 2002 , Kombe la dunia korea kusini na Japan, Mechi kati ya Nigeria na Argentina ilipigwa siku ya jumapili asubuhi mida ya saa tatu asubuhi kwa majira ya africa Mashariki .

Kona ya kumi ilopigwa na Mkongwe Juan Sebastian Veron Ndio iloondoa Matumaini ya waafrica kuendelea hatua ya robo fainali. Katika mechi ili namkumbuka Diego simeon , Huyu Juan sebastian Veron alipotelea manchester.

Katika Kundi hili la kifo Muingeleza alifanikiwa kuvuka pamoja na Mjerumani, Mechi ilofuata muingeleza akalala mbele ya Brazil mida ya mchana. Mjerumani alifanikiwa kufika fainali yeye na Brazil.

Siku ya Jumapili mchana wa saa tisa Ndani uwanja wa Yokohama ,Mjerumani akalala na Vyuma viwili vya mkongwe Ronaldo luis Nazario De Lima.

Wakumbukwe wafuatao:
Oliver Khan,
Gatuso
Idetoshi Nakata,
Suzuki,
Jugen Klinsman Kocha,
Barack namba 6 Ujeruman,
Caf,
Roberto Carlos (alipotelea Real madrid)
Reonaldo,

MIAKA IMEKIMBIA..
Hivi Waingereza wanamsahau Ronaldihno?
 
mechi ile ilichezwa siku ya ijumaa mchana ,ikiwa ni mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia, ikihusisha bingwa mtetezi France na timu toka africa,
Mashabiki takribani elfu 60 hawakuamini bingwa mtetezi akidhalilishwa na timu changa toka africa.

watu kama kina Zidane, david trezegut, bathez, viel, thiery henry, Christian kalembeu.

daaah Miaka imekimbia.
Senegal walikuwa wanacheza Na Waafrica wenzao waliopata uraia Ufaransa.Maana ile timu ya Ufaransa ilijaa ngozi nyeusi balaa.Hivi Thuram alikwepo kwenye Kosi la Ufaransa,Kumbukumbuku zinapotea kidogo?
 
Habari zenu wakubwa miaka hiyo nilikua songea ni chalii mdogo sana nakumbuka nilikua nacheza stika tu
Nilikua namsikia diof fediga na camara marehem baba akiwaongelea kwakua alikua shabiki wa Newcastle huyo diof alivyo kuwa anapambwa na kufananishwa na alan sheera
nikaanza kufatilia nilikua na mkubali tokea enz hizo nilikua napenda alivyo mbabe ndio alinifanya nimpende patrice viera kisa ubabe matokeo yake wakanitupa kulipenda janga ladunia arsenal bora ninge mfata mzee Newcastle kama nilivyo mfata kwa simba na leox leiws
Umenikumbusha bigijii zenye stika Za wachezaji
 
Ufaransa ya 2002 ilikuwa Na gundu,nadhani 1998 huenda walifanya dhulumati,2002 waliishia makundi kama sikosei group lao walikuwa wa mwisho
Licha ya kutoka mapema kwenye Kombe la Dunia, Ufaransa ilikuwa imesheheni mastraika wa nguvu.
Thiery Henry alikuwa mfungaji bora EPL
Djibril Cisse alikuwa mfungaji bora ligi ya Ufaransa
David Trezguet alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Italy.

Lakini hawakufua dafu
 
Back
Top Bottom