Simba wa Teranga: Kikosi cha dhahabu kilichotikisa Dunia

Simba wa Teranga: Kikosi cha dhahabu kilichotikisa Dunia

daaaa nakumbuka mbali enzi hizo antena ya kushikiria na channel moja ya Uganda UBC ndo waonyeshaji tu
 
mkuu hivi ile habari ya huyo jamaa mwenye jezi namba 10 kuiba cheni ilikuwa ni kweli??
 
Mechi ya ufunguzi dhidi ya bingwa mtetezi wa Kombe la Dunia, Senegal anamfunga Ufaransa iliyotimia goli 1-0 na kuendelea hapo safari ikawa ni nzuri mpaka walipotolewa na Uturuki kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2002 pale Korea Kusini na Japan. Unakumbuka kikosi hiki? Unakumbuka matukio gani kuhusu kikosi hiki? Karibuni wadau mtiririke
in-japan-und-korea-osaka-match-60viertelfinalesenegal-tuerkei-01-nv-picture-id52836745
Diof alikinogesha sana kikosi hiki imebaki story tu raha ya world cup ya 2002 ililetwa na hawa jamaa
 
Hii ilikuwa Senegal bora kabisa iliyowahi kutokea.
Nakumbuka game ya kwanza World cup wanakutana na mabingwa watetezi Ufaransa, game inapigwa majira ya saa nane kwa saa za kwetu.
Diof anapiga cross matata kutoka kona ya kushoto, mabeki wa Ufaransa wanazembea, Barthez anapotea na Senegal wanapata goli la kwanza.
Wanakwenda kutolewa na Uturuki nakumbuka goli linafungwa na Hassan Sassi baada ya beki za Senegal kumsahau jamaa.
Hiki kilikuwa kikosi cha dhahabu.
Senegal ilikuwa na kipa bora kabisa
Kina Henry Camara
Senegal walianza kuongoza dhidi ya uturuki magoli yakakataliwa iliuma sana ila lilipofungwa la uturuki likawa goli. Wazungu wana wivu sana.
 
Nlikua STD 4
Khaaaah!!! Yafaaa muanzage na salamu zile za wanasiasa "wakubwa zangu Shikamoni" ndipo muanze changia siledi. Mie nachumbia mwaka huo tena kwa shida sio Kama siku hz mnatumiana meseji. Demu anaviziwa j2 tu, ukimkosa halo basi. Kweli aisee wahenga tulikuwa na Akili na uwezk mkubwa wa kutunza record. [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Khaaaah!!! Yafaaa muanzage na salamu zile za wanasiasa "wakubwa zangu Shikamoni" ndipo muanze changia siledi. Mie nachumbia mwaka huo tena kwa shida sio Kama siku hz mnatumiana meseji. Demu anaviziwa j2 tu, ukimkosa halo basi. Kweli aisee wahenga tulikuwa na Akili na uwezk mkubwa wa kutunza record. [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Pana mmoja muungwana katika ule uzi wa kikosi cha uholanzi alisoma comments basi alichoweza kuandika ni hivi "kwanza kabisa kaka zangu shikamoni"hakuandika kitu kingine.
 
Ukiachilia mbali swala la ulimbukeni na kuridhika wengi wao huwa walaghai wa umri ndio maana hutamba kwa muda mfupi. Ghana iliwakuta hali hiyo miaka ya 90 walikuwa wanachukua sana hizi world cup under nini nini sijui mpaka ilipokuja gundulika hiyo ghilba yao na nadhani walifungiwa kushiriki kwa muda flan. Kumbe vilikuwa vijeba nyembe nyingi tu zimepita videvuni pana visiki vya khatari.Pia nchi za ulaya wametuzidi hapo vijana wanaona kuliko kucheza timu za kwao bora wakacheze kwa wazungu mtizame chary musonda wa Chelsea huyu dogo ataishia kucheza kama sio England basi Belgium ambapo alizaliwa waqt huo baba yake Charles musonda wa zambia akicheza underletch ya ubeligiji nae kazaliwa miaka mitatu tu baada kutokea kule Gabon ambapo kikosi cha kk eleven kilipoteza maisha.
Du!! Kaka umenikumbusha Mosses Chikwarakwara waZambia mwaka hiyo aliyefariki pamoja na wale 22 kwenye hiyo ajali. Alikuwa na uwezo km Lunyamila wa Yanga. Winga machachari sana. One day nimemuona akiwa dereva.
 
Nilikua kidato cha pili, Shule ya sekondari Makutupora-Dodoma, mtihani wa Mock nililazimika kuuacha mitihani niwahi mechi. Ni kipindi hiki ndio nilikua mwanzo wa mateso ya kishabiki yanayonitesa mpaka Leo jinamizi la kuipenda Arsenal.
Pole sana. [emoji3] [emoji3] Hamia man city mwaka huu naona wapenzi wao Wanabet kwa uhakika.
 
Du!! Kaka umenikumbusha Mosses Chikwarakwara waZambia mwaka hiyo aliyefariki pamoja na wale 22 kwenye hiyo ajali. Alikuwa na uwezo km Lunyamila wa Yanga. Winga machachari sana. One day nimemuona akiwa dereva.
Hiyo ilikuwa kk au kenneth kaunda 11 sio mchezo akina derby makinka Eston mulenga palikuwa na bwana mdogo mmoja alikuwa na miaka 19 au ishirini wa kuitwa kelvin mutale ndio kwanza atoke kupiga hattrick watson changwe pana wisdom chansa huku John soko pale numba mwila
 
Back
Top Bottom