NA MIMI NITOE MAONI KUHUSU WAZO LA WANA SIMBA KUJENGA KIWANJA CHAO CHA MPIRA.
Kwanza kabisa napongeza wazo la WanaSimba kujenga kiwanja Chao Cha Mpira. Kwako Ni kwako,kwahiyo endapo watafanikiwa Basi itakuwa Ni hatua nzuri kwa Club hiyo ya Mpira Nchini Tanzania.
Lakini wazo hili ukamilishaji wake Sio wa mda mfupi Kama tunavyofikilia kabisa,hii Ni kutokana na Gharama kubwa ambazo zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.
Mfano,Uwanja Mkubwa kabisa wa Kabumbu nchi Tanzania Ni Uwanja wa taifa Maarufu Kama MKAPA NATIONAL STADIUM. Uwanja huu ndio Mkubwa kabisa nchini Tanzania ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 60,000. Uwanja huo ulianza kutumika baada ya kukamilika mwaka 2007,na Mechi ya kwanza kuchezwa ilikuwa Kati ya SIMBA SC dhidi ya YANGA FC zote za Nchini Tanzania.
Uwanja huo ulijengwa na Kampuni ya
KICHINA Kama msaada wa Serikali ya China kudumisha ushirikiano na nchi ya Tanzania.
Uwanja huo wa Mpira ujenzi wake Mpaka kukamilika Uligharimu takribani Dolla za Kimarekani Milioni 56 za kipindi hicho($ 56M). Hizo Ni sawa na Takribani Bilioni 132 za Kitanzania (Tzs 132B).
Kwa Motisha,Rais wa Club ya Simba ameahidi Kuchangia kiasi Cha Tzs 2B. Kwahiyo Kuna Naksi ya Tzs 130B ambazo wanaSimba wanatakiwa kujitoa mifukoni mwao ili kukamilisha ujenzi huo.
Kwahesabu za harakaharaka tu,tufanye Watanzania wote Milioni 58 wawe mashabiki wa SIMBA SC,na wawe tayari kuichangia Timu hiyo(Hapa tuna-ASSUME TU). Ili kukamilisha ujenzi huo kila Mtanzania atahitajika Kuchangia kiasi Cha Dola 0.9 sawa na Tzs 2,100/=.
Swali,je Watanzania wote Ni Mashabiki wa Simba? Jibu Ni Hapana.
Je,Mashabiki wa Simba Ni Kiasi gani? Mashabiki wa Simba Nchi nzima Ni Milioni 10 lakini wenye uwezo wa Kuchangia kutokana na ushabiki wao kindakindani Ni Watu Laki moja TU. Kwamaana hiyo Kati ya hao watu Laki moja,kila Mmoja atahitajika Kuchangia kiasi Cha Tsh 1,218,000 (Milioni moja Laki Mbili na Elfu 18). Je hapo vepee? Jibu Ni haiwezekani.
Kwahiyo Simba watulie tu,Kama MO anataka Simba iwe na Uwanja wake na anaipenda Simba kweli Basi kwanini asizame mfukoni akachomoa Tsh 132B akajenga Uwanja? Utajiri wa MO Dewji Ni Zaidi ya Tsh 3500B (Trillion Tatu na Nusu)
Ukichukua utajiri wa MO ukatoa gharama za Uwanja Ni sawa na aliyechota kikombe Cha Maji kutoka Baharini,Bahari haiwezi kuathirika kabisa.
3,500B-132B= 3,368B. Yaani anabaki na Tzh Trillion Tatu na Billion miatatu na sitini na nane.
Ushauri
MO aache kuwakamua Masikini wanaSimba ili kutimiza ndoto zake.
Antony Linken