permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 11,682
- 14,241
Hisa kibongo bongo zinazengua, kampuni isipokuwa na strategy ya kueleweka watu watapoteza hela kwa thamani ya hisa kushuka.Njia rahisi kwa Simba kujenga uwanja ni kuingia ubia na Kampuni duniani kote wanafanya hivyo hata kama watachangia fedha lakini at least 55% - 65% ya Bajeti itoke kwenye Kampuni hizo zingine hata wakichangia sawa
Kwa upande mwingine
kama mfumo wao wa HISA unaeleweka wangeingia DSE pale wakaweka lengo lao then watu wakanunua HISA wangefanikiwa haraka sana.
Hata mimi nimekuwa na mtazamo huo maana inawezekana kabisa ili tunawe ishu ya kiwanja hadi miaka 50 ijayo ndo labda tuanze kufikiria kuongeza ukubwa wa KiwanjaNitachangia laki nasubiri utaratibu ila tungejenga uwanja mkubwa zaidi wa kuchukua watu elfu 60
Unajikuta kichwa wakat umekopy kila kitu toka ig [emoji23][emoji23][emoji23]Ulimwengu wa Giza, Ulimwengu wa Mwanga.
Mashabiki wa Ua Jekundu wanaishi kwenye Dunia ya hisia,wanayatazama Mambo kichwa chini Miguu juu wapo kwenye Ulimwengu ambao Giza ni Chakula chao pendwa hawajui Vivuli vya ukweli na ukweli wenyewe
Kwasababu maamuzi yao ya msingi kuhusu maisha yanatengemea hisia zilizolala kwenye kesi ya VVIP.Kuwepo Kwao kwenye Hisia na Akili zao kuviringishwa na mgando wa fikra za kinazi kumewafanya wanaamini mnara wa Babeli ulijengwa Kwa fedha za kashata,waamini Nou Camp ilijengewa Kwa mafuta ya Vitumbua.
Pia Kufungwa Kwao minyororo ya Giza la ujinga na kutumia tumbo kutoa maamuzi ya msingi kumewafanya kuamini project ya kujenga Uwanja ni kama kukanda ngano,Waamini Samaki anaweza kupanda juu ya mti Kwa vipande vya shilingi vilivyolala mfukoni mwa waashi.
Nafikiri huu ni wakati wa kuzamisha vichwa vyao kwenye vilindi vya maji,Ni wakati ambao wanapaswa kuangalia Kila jambo kwenye Ulimwengu wa Mwanga,kwenye Ulimwengu ambao kanuni inasema kujenga Uwanja kunahitaji busara kuliko Hisia za Mtoto kunyinwa Maziwa ya VVIP.
Haya yanatokea kwasababu ya uvivu wao kufikiri na kuamua kuwa walevi wa Hisia kuliko mantiki na Ujinga mtamu umetawala pembe zote za Dunia yao iliyojaa Giza.
Ameshajitoa vya kutosha hadi analemewa so hatuwezi kusita katika hili eti tunamtegea never , yaani tutahakikisha tumechanga hata wachawi msimame kuturoga , hela ni zetu wewe baki na zako usichange.Na ishu ya kuwa na elimu ya makampuni hatuihitaji katika hili we are serious hadi tuuone uwanjaWakuu tukiacha siasa za maji taka za Usimba na Uyanga. Nataka nichangie huu mjadala kwa namna tofauti, kwa namna ambayo nitaiweka kidogo kisomi na hapa naomba tuache ushabiki.
1. Simba ni kampuni ambayo iko na 2 shareholders, MO and Members on the other hand. Kwa mtiririko huohuo shareholders wako na share 49% na 51% respectively.
Kama ndio hivyo basi SIMBA SC ni Mali ya MO na WANACHAMA kwa upande mwingine. Hata hivyo kama SIMBA ni kampuni na hao ni wabia wake, haitakiwi shabiki achangie kiasi fulani katika ujenzi wa ASSETS za Klabu kwa sababu shabiki akichangia ina maana unamwongezea MTAJI MMILIKI.
2. Ilitakiwa ifanyike analysis nzima juu ya gharama za ujenzi kisha gharama zile zigawanywe kwa uzito sawa na SHARES yaani kama ujenzi ni BIL 20 basi MO atapaswa kutoa Bil 9.8 na WANACHAMA Bil 10.2. Yes ni kampuni hivyo Mo hapaswi kusema watu wachangie wakati yeye ni mwanahisa na anapata INCOME through hiyo kampuni si sahihi. Kwanini aombe michango wakati kampuni ni yake kwa 49%?.
3. Watanzania wenzangu, kabla ya kurukia kitu lazima mkae chini na mtafakari kwa kina juu ya masuala haya. MO anawakosea sana Simba, na always yy hujifanya kama anasaidia lkn ukweli ni kwamba yeye ni Mwanahisa kwanini atake mashabiki wamchangie? Kama ndio hivyo basi ajitoe kuwa mmoja wa wamiliki ili watu wachangie wakijua yeyote anaweza kuwa kiongozi wa SIMBA.
4. Rai yangu kwa wapenda michezo, haki na wapenzi wa hii klabu kupaza sauti na kugundua UTAPELI wa wazi anaofanya huyu MO DEWJI.
KWA UCHACHE NAWASILISHA.
NB. Kama uelewa wako kuhusu umiliki wa makampuni ni FINYU usiquote huu mchango.
Shida yetu Simba iwe na uwanja wake tu mengine ya anamiliki nani bakini nayo ninyi yaani mimi nishindwe kutoa elfu 10 eti kisa itakuwa ni kumtajirisha Mo kwa kitu ambacho uwepo wake tu utakuwa furaha kwetu , TUTACHANGA tu maadam sio dhambi mbele za MunguWewe ni kilaza, pitia hoja zako zote kila uelimishwapo kuhusu SIMBA unajaza mafua kichwani. SIKIA MO NI MMILIKI HALALI WA SIMBA KWA 49% na WANACHAMA WANAMILIKI 51% Kwahiyo KAMA ILIVYO AZAM AMBAPO BAKHRESA ANAMILIKI KWA 100% NA SIMBA INAMILIKIWA KWA 49% NA MO. HIVYO NI JUKUMU LAKE KUJUA GHARAMA ZA UWANJA NA KISHA AKAE YEYE NA WANACHAMA WAGAWANE KULINGANA NA UBIA WAO AMBAO NI 51% KWA 49%.
Unapochangia kitu tuliza akili yako na acha ushabiki wako wa kimpira usio na maana.
Kwa mfano wewe ukichangia hiyo pesa na UWANJA UKAJENGWA hujui kuwa UTAKUWA MALI YA MO KWA 49%?? kwa maana itakuwa ni ASSET ya SIMBA?
Sasa kwanini atake mchangie wakati anajua wazi kuwa yeye ni mmiliki? Anataka tumpe mtaji aongezee kwenye mtaji wa AWALI?
Ushauri mzuri ila umeshapiga hesabu za ikiwa mashabik watatoa sh 1000 na wawe 5000 kwa miezi 12?Kwa bajeti nzuri na kubwa duniani kote, Viwanja hutumia mpaka miaka minne au mitano kukamilika, vile vya kuanza kabisa chini! Hivyo unahitaji resource za kutosha sana, maana kuchanga tu Watu watachoka
Klabu nyingi duniani zimeingia ubia na Makampuni makubwa katika ujenzi wa Viwanja vyao kisha kukubaliana suala la mapatano kuhusu malipo
Mfano Atletico Madrid baada ya kuvunja Vicente Calderon na kujenga uwanja mpya chini ya udhamini wa Kampuni ya wachina wakakubaliana kwenye naming rights
Uwanja unaitwa METROPOLITANO ila kutokana na sababu za kibiashara unaitwa WANDA METROPOLITANO, hii Wanda ni Kampuni ya Kichina
Hivyo Simba wanaweza kuingia ubia na Kampuni moja Tajiri, jumlisha na pesa yao wakapata uwanja mzuri, wa kisasa na wenye kuingiza hata Mashabiki 30,000 sio mbaya sana
Ni ukweli mchungu kuwa huwezi kusimamisha uwanja wa hadhi ya Simba kwa michango tu mfukoni, bali kumeza vidonge vichungu vya kukopa, kuingia ubia na Kampuni Ili kufanikisha!
Pia Simba wajiandae kusacrifice kipindi cha miaka hadi mitano ya kufanya vibaya uwanjani kwasababu watashindwa kufanya vizuri ktk masoko ya usajili wa wachezaji bora wenye gharama kwasababu ya Pesa nyingi imeelekezwa kwenye ujenzi wa uwanja
Waitishe Mkutano Mkuu wa dharura kukubaliana, kujenga uwanja ni Uamuzi wa hasira, sasa ni hatari sana kufanya maamuzi ingali na hasira, hivyo kuzifanya hasira ziwe rasmi wanapaswa kuitisha Mkutano Mkuu wakubaliane, kwenye faida na hasara pia
Muwe waelewa , aliyeanzisha hoja hii ni Magori sasa unamlaumu vipi Mo kukubaliaba na Magori watu wachange?Naona kwa mbali unaanza kuelewa. Iko hivi mkataba wowote una VOID ikiwa uko nje ya sheria mama (Company act) kwa vyovyote vile gharama za ujenzi wa UWANJA lazima ziendane sawa na kiwango cha uwekazaji.
Hakuna shortcut kwenye kuongoza hizi kampuni mkuu. Mo arudi tena akae na wanahisa wenzake (WANACHAMA) watafute VALUER wajue gharama nzima ya ujenzi kisha kila upande uchangie kulingana na HISA ZAKE.
Kubwa zaidi upande wa wanachama ndio ulipaswa utoke uombe wanachama wake kuchangia maana ndio upande wao ma sio MO aombe watu wachangie akijua wazi ni JUKUMU lake kutoa 49% ya gharama.
Unawakatisha tamaa watu ila inawezekana niambieHapana , sidhani kama ni jukumu lake kigharamia 49%za ujenzi wa uwanja. Uwanja una gharama Sana za ujenzi. Hao wanachama Wana buku buku tu. Haiwezi kufika huko. Labda wajenge kama chamazi. Ila kama uhuru au taifa. Nguzo moja ya uwanja tu unakuta imelamba mamilioni ya pesa. Dawa ni kukopa tu.
Hesabu za makaratasi hizo boya wewe.. nani achangie buku kila mwezi? We unadhani watu MIL 5 ni mchezo eeh.Unawakatisha tamaa watu ila inawezekana niambie
Watu milion 5 wakichangia sh 1000 kila mmoja kwa mwezi itakuwa sh ngapi kisha izidishe mara miezi 36 yaani miaka 3 uone uwanja unakamilika au la
Tzs 24B. Fedha zote zilitoka mfukoni mwa BAKHERESA. Makapuku wa Simba hawawezi kuchanga 22B Tzs. Historia inakataa,Hakuna Rambirambi(Michango) bongo iliyowahi kufikia hicho kiasi.Uwanja wa azam uligharimu shingapi?
Nadhani Simba wanahitaji uwanja ambao ni twice than Azam complexUwanja wa azam uligharimu shingapi?