Simba wadhamiria kukamilisha uwanja wao, Mo Dewji achangia Bilioni 2

Kwanza kabisa napongeza wazo la WanaSimba kujenga kiwanja Chao Cha Mpira. Kwako Ni kwako,kwahiyo endapo watafanikiwa Basi itakuwa Ni hatua nzuri kwa Club hiyo ya Mpira Nchini Tanzania.
Nyie nyie nyie!! Wazo tena?! Angalau miaka 10 iliyopita tulisikia "wazo" la ujenzi wa uwanja ambao ungegharimu Sh 75 Billion, yaani hadi leo bado wazo tu?!

Tukaambiwa Waturuki ndio wajenzi wa uwanja, na tukaoneshwa hadi pori huko Bunju litakalojengwa ambalo lingejengwa uwanja wa 75B! Bado miaka 10 baadae mnatuambia tena habari za "wazo"!
 
Wafuge vizuri nyau wa kutosha, walinzi wa milango wasaidizi
 
Kwahiyo Simba watulie tu,Kama MO anataka Simba iwe na Uwanja wake na Simba kweli Basi kwanini asizame mfukoni akachomoa Tsh 132B akajenga Uwanja? Utajiri wa MO Dewji Ni Zaidi ya Tsh 3500B (Trillion Tatu na Nusu)
Makolo acheni kudanganya watu! Huo sio "utajiri" wa Mwamedi bali ni "utajiri" wa Familia ya Mzee Gulamabbas Dewji!! Hata ukienda kwenye page ya METL, Mwamedi pamoja na tabia yake yote ya kupenda kujimegea nyama kwa wingi, hapa akaamua kusema ukweli kwa sababu nyama yote angekula peke yake, akina Fatema wasingekubali. Mwamedi anatujuza 👇👇👇

" After studying business at Georgetown University, I joined my father’s business in 1999, since then MeTL Group has grown significantly, diversifying to sectors never before thought possible. This company profile will outline the depth of MeTL Group’s presence in Tanzania, the brand that we have and how far we have come over the years."

Sasa sijui siku hizi pale METL wanatengeneza maroketi hadi atuambie amefanya diversification ambazo katu hapo kabla haikufikiriwa kwamba ingewezekana!! Mafuta ya kula yameanza kuzalishwa TZ tangu enzi za Nyerere! Juice zilizojazwa maji, zimeanza kutengenezwa tangu enzi za Nyerere! Sabuni zilikuwepo hadi Mbuni ambazo Mwamedi mwenyewe kafulia wakati akiwa anasoma primary au hata chekechea!! Kuna kipi kipya cha kutuambia "...sectors never before thought possible"?
 
Yanga mpo vizuri kwenye mipango nani afanye nini, ila kwenye matokeo waachieni Simba, sijui huwa inakuwaje utaskia tu Simba kamtoa Zamalek hata wamefikaje haieleweki eleweki, GO GO GO SIMBA, ONE TEAM ONE DREAM.
 
Mo no.mbabaishaji.

Anatoa bl 2 bila kusema kwanza ile 20 katoa au hajatoa? Na simba ni kampuni sasa inakuaje mtu mmoja mmoja aanze kuchangishwa wakati wana HISA ZAO?
 
Mtaji mkubwa wa simba ni washabiki.Washabiki wa simba wana uchungu mkubwa kuliko wanachama. Viwanja vingi vilijengwa kwa nguvu za wananchi kwa kuongeza bei kwenye vinywaji kama bia na soda ingawa baadae ccm ilivipora na kufanya mali yao. Mashabiki wanaweza wasichangie moja kwa moja ila wanaweza kwenye mechi zao tiketi zikaongezwa bei ili pesa ya ziada ikaenda kwenye mradi wa ujenzi. Pia wangetengeneza bidhaa kama kofia, miavuli, kalenda wakahimiza mashabiki wanunue ili mapato yaende kwenye uwanja ingawa sijui mkataba wao na vunjabei ukoje.
 
Jamaa mjanja Sana, kasha wakimbia tayari. Yaani uwanja wa watu 30, 000/= unao karibia thamani ya 40 bilion unachangia 2 bilion kweli?
Ni suala la mipango tu,Simba na Yanga zina wanachama na wapenzi Kwa mamilioni wakihamasishwa wanaweza kuchangia kabisa,tatizo mnapenda kutanguliza kushindwa kabla ya kuanza. Mbona CCM inamiliki viwanja vingi tu na vilijengwa kwa kuchangia.
 
Haya nenda kashitaki CAS kuwa Mo hana hela bali ni za babake. Hivi Utopolo mnakwama wapi na hoja zenu muflisi?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
BAKHRESA hakuhitaji michango na alifanya kimyakimya.
Sasa umiliki wa bakhesa kwa azamu ni sawa na huo wa mo kwa simba?timu ambayo ikifululiza matokeo mabaya"mnasema ondoka tuachie timu yetu"??ajichanganye kutumia karibia bilioni 20, kujenga uwanja, ??ki ufupi uwanja hauwezi kujengwa kwa njia hii hata siku moja!!!mashabiki wenyewe kuchangia hiyo 1000 ya uanachama kwa mwezi ni tabu, ndio umwambie kwenye mambo ya billions?wao ni kutoa povu tu tiachie timu yetu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…