change formula
JF-Expert Member
- Sep 8, 2020
- 729
- 1,559
Wewe ni mtupu kichwani,na hesabu zako za kilimo cha matikiti,kabla ya kuleta hizo hesabu zako za kufikilika lazima uelewe nini dhima ya kuanzishwa club ya Simba? Ukisoma katiba na historia ya Simba utajua kuwa Simba ilianzishwa kama club ya mpira na michezo mingine.[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mkuu kwahiyo mimi mtupu kichwani dah, nimecheka hadi watoto wananishangaa hapa.. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Waanzilishi wake walikuwa na dhima ya kupata burudani na kusaidiana katika shida na raha,historia inaonyesha hivyo, nia yao ilikuwa hivyo na wala hakujawahi kutolewa tamko au waraka wa kufuta malengo yao ya kuanzishwa.Ila kutokana na nyakati kubadilika Simba kama taasisi ya watu imepitia mabadiliko mbalimbali kulingana na nyakati husika.
Kuna nyakati za mwanzo waanzilishi wao walikuwa wakichangishana pesa ili kufanikisha shughuli zao na malengo ya club,kutokana na kupanuka kwa club na kuongezeka kwa mahitaji michango yao haikutosha,hivyo walijitokeza wafadhili ambao hawakuwa na nia ya kujitangaza bali kwa sababu za mapenzi yao kwa club na uwezo wao wa kiuchumi walitoa pesa zao binafsi kusaidia club ili tu wapate furaha.
Zama zikabadilika nao hao wafadhili michango yao ikawa haitoshi kutokana na mahitaji kuongezeka,wakaja wadhamini nia ni kuweka pesa ili watangaze shughuli zao za kibiashara,hapo ndio ikaonekana na club ibadilike pia ijiendeshe kibiashara.
Ndipo lilipokuja wazo la uwekezaji na muekezaji sharti awe mwanasimba ili kudumisha dhima yakuanzishwa club na kudumisha misingi yake,kwaio ukitizama bado lengo la kuanzishwa halijabadilishwa ni lile lile kupata burudani na kusaidia club ili kudumisha furaha na kusaidiana mwenyewe kwa wenyewe.
Kuhusu suala la kwa nini michango wakati club inajiendesha kama kampuni ya faida? Hapa kuna majibu mawili,moja ni kudumisha lengo la kuanzishwa club la kupata burudani na burudani ili ikamilike inaitaji nguvu na gharama ndio maana watu wanasafiri na timu kwenda kushangilia kwa gharama zao kila timu inapocheza, yote ni kuitafuta furaha yao,je hao kwa mawazo yako hasara yao iko wapi?
Pili Simba ni club ya wanachama na muekezaji ni mwanachama yeye ni sawa ana miliki asilimia 49%na wanachama wengine wenzake wanamiliki 51% ukumbuke Simba bado haijakamilisha mabadiliko kwa asilimia zote, hivyo kama mchango kila mtu mpenzi wa Simba atatoa kulingana na kipato chake, itasaidia kuongeza thamani ya club kwa maana ya asset na pia kuongeza kipato ambacho kinaweza kuwa na faida kwenye gawio kwa wana hisa uko mbeleni utaratibu ukikamilika.
Uelewe utaratibu huu utaongeza mapenzi kwa mashabiki kwa timu yao kwa kuona kuwa timu inawahusu na wamewajibika.
ni kama vile waanzilishi wa club waliopo wanavyoona fahari kuanzisha Simba yao itabaki historia na haitafutika milele, ni kama kuzaa na kusomesha mtoto wako akawa na future nzuri hata asipokuja kukusaidia ila atasaidia kutengeneza generation ya ukoo wako wakati huo.
Ili la kusema MO ni tapeli ni mawazo mgando na mawazo ya kimaskini au ni wivu kwa kuona MO ameleta mafanikio makubwa kwa Simba.
Umekuja na theory za darasani zisizo na uhalisia kwenye maisha ya kila siku,kumbuka MO ni mwanasimba hata akipata bado ni mwanafamilia wa Simba,au wewe kaka yako akipata utajiri kwenye ukoo wenu utanuna? Kumbuka Simba ni familia ya michezo na burudani ndio lengo lao hasa, na ndio maana waliweka sheria kumpa timu yao mwanafamilia wao mmoja mwenye uwezo, na sio mtu yeyote TU.
kumbuka kupenda hizi timu ni passion na mpenzi wa kweli hana cha kupoteza kuhusu timu yake ndio maana mpenzi wa timu ananunua jezi,analipa kiingilio uwanjani kutazama timu yake,na bado mchezaji akifanya vizuri uyo mpenzi anatoa pesa zake kumpa mchezaji zawadi!!ana safiri na timu anajilipia chakula,malazi na kiingilio ili kushangilia timu yake.
Kwa hali hio unaona mawazo yako na akili zako yapo kinadhalia zaidi kuliko uhalisia, pole sana jifunze kuchambua mambo kwa upana na sio kubishana kwa mawazo ya darasani.