Simba walitoa taarifa rasmi kwa timu mwenyeji kuwa saa 1:15 watautumia uwanja?

Simba walitoa taarifa rasmi kwa timu mwenyeji kuwa saa 1:15 watautumia uwanja?

Mister mimi

Member
Joined
Apr 29, 2018
Posts
89
Reaction score
106
Kwa maana kanuni inasema timu mgeni ana haki ya kufanya mazoezi katika uwanja utakaochezewa mechi angalau SIKU MOJA kabla ya mechi.

Sasa swali ni je simba walienda kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi? siku za kisoka zinahesabiwaje? Kwa mfumo wa masaa 24,48,72? Au zinahesabiwa kwa mfumo wa j3,j4,j5...?

Kama zinahesabiwa kwa mfumo wa j3,j4...., simba wako sawa kama tu walimtaarifu mwenyeji ili awaachie mlango wazi.ila kama zinahesabiwa kwa mfumo wa saa 24,basi simba hawakwenda siku moja kabla,bali walienda siku husika ya mchezo.

Na je,ikitokea kama ilivotokea leo kanuni zinaruhusu timu kususia mchezo?

Nani mwenye mamlaka kikanuni ya kuvunja mchezo?

Mamlaka ya kuvunja mchezo simba ameyatoa wapi?
Kwahiyo ukiijua tu sheria unaruhusiwa kujichukulia maamuzi?

Aaah au basi! Soka letu kivyetu vyetu!
Hakuna anayejali muda,hisia na pesa walizotumia mashabiki na wadau!
 
Hili tatizo lisingetokea kama kila mtu angekuwa na uwanja wake maana pale kwa mkapa wanapaona kila timu ni nyumbani kwao anaweza kwenda muda wowote
 
Sio tu timu mwenyeji, hata meneja wa uwanja na Bodi ya ligi haikuwa na Taarifa kuwa Simba wanataka kutumia uwanja usiku.

Unakuja ni kwanini?
 
Sio tu timu mwenyeji, hata meneja wa uwanja na Bodi ya ligi haikuwa na Taarifa kuwa Simba wanataka kutumia uwanja usiku.

Unakuja ni kwanini?
Walienda kuwanga wewe ulisikia wapi wanaoenda kuwanga makabirini wanatoa taarifa wanaenda kimya kimya ila hii imebuma wameshtukiwa baada ya kushtukiwa chezo limebuma ndio wakaja na figisu zao za papatu papatu na yule Almasi na Mngeto wa bodi ya ligi nao wamejaa kwenye mfumo pumbavu
 
Je,meneja na kamishna wa uwanja walipewa taarifa na uongozi wa simba kuwa saa 1:15 watakuja kuutumia uwanja?
Au simba walitaka meneja aache geti wazi muda wote kwa KUHISI kuwa simba watakuja usiku MUDA WOWOTE kuutumia uwanja?
Simba alicheza hivi karibuni na Azam fc kumbe wao wamefaidi uwanja zaidi kuliko yanga sc
 
Kwa maana kanuni inasema timu mgeni ana haki ya kufanya mazoezi katika uwanja utakaochezewa mechi angalau SIKU MOJA kabla ya mechi.

Sasa swali ni je simba walienda kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi? siku za kisoka zinahesabiwaje? Kwa mfumo wa masaa 24,48,72? Au zinahesabiwa kwa mfumo wa j3,j4,j5...?

Kama zinahesabiwa kwa mfumo wa j3,j4...., simba wako sawa kama tu walimtaarifu mwenyeji ili awaachie mlango wazi.ila kama zinahesabiwa kwa mfumo wa saa 24,basi simba hawakwenda siku moja kabla,bali walienda siku husika ya mchezo.

Na je,ikitokea kama ilivotokea leo kanuni zinaruhusu timu kususia mchezo?

Nani mwenye mamlaka kikanuni ya kuvunja mchezo?

Mamlaka ya kuvunja mchezo simba ameyatoa wapi?
Kwahiyo ukiijua tu sheria unaruhusiwa kujichukulia maamuzi?

Aaah au basi! Soka letu kivyetu vyetu!
Hakuna anayejali muda,hisia na pesa walizotumia mashabiki na wadau!
Kanuni haisemi siku moja kabla, bali angalau mara moja kabla ya mechi

1741444395557.png

Na mara moja kabla ya mechi, it can be two days, five days, a week or just a day before. Na inasemekana walishafanya mazoezi Ijumaa, hence kigezo cha angalau mara moja kimekamilishwa.
 
Mtu akitaka kukuroga haitaji kufika unapoishi anakuroga huko huko alipo, suala la kusema walioenda kuroga kiuchawi halipo sawa, mtu yupo pemba anakuroga hata ukiwa Mara
 
Mtu akitaka kukuroga haitaji kufika unapoishi anakuroga huko huko alipo, suala la kusema walioenda kuroga kiuchawi haiingii halikai, mtu yupo pemba anakuroga hata ukiwa Mara
Uchawi hauvuki bahari..!!
Na jihadhari, usije ukathubutu kumroga mganga..!!
 
Kanuni haisemi siku moja kabla, bali angalau mara moja kabla ya mechi

View attachment 3263807
Na mara moja kabla ya mechi, it can be two days, five days, a week or just a day before. Na inasemekana walishafanya mazoezi Ijumaa, hence kigezo cha angalau mara moja kimekamilishwa.
Elewa sentensi,"KABLA YA SIKU YA MCHEZO" ina maana haitakiwi kuwa siku husika ya mchezo.

Sawa,tufanye uko sawa,je wahusika wa uwanja walipewa taarifa juu ya ujio wa simba,au wahusika walitakiwa KUHISI tu kuwa simba watakuja muda wowote waache mageti wazi?
 
Back
Top Bottom