King Jody
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 1,834
- 3,456
Ni wakati wa kumaliza tofauti zenu baada ya kufungwa na mtani wenu kwa idadi ya mabao mengi {1-5} Maisha lazima yaendelee, haikuwepo sababu ya msingi kumtimua kocha Robertinho mzee wa Objective football, Takwimu zinaonesha amepoteza mechi moja tu tangu ajiunge nanyi kama Head coach.
-Hakuna haja ya kuwatuhumu wachezaji kuihujumu timu, Kubalini mlizidiwa na mpinzani wenu [Yanga} ambaye yupo kwenye ubora kuwazidi kwa sasa, Huo ndiyo ukweli {kitakwimu}
Kumbukeni kuna michuano ya kimataifa inawasubiri, Msiangalie mlipojikwaa, angalieni mlipodondoka,
Kumbukeni kuna watu wanapenda kuwaona mkiendelea na migogoro ambayo kimsingi haina afya kwenye tasnia na mustakabali wa soka letu.
Simameni imara kwa ajili ya kuimarisha timu yenu, kumtafuta mchawi nani ni kujipotezea muda.
Nawatakia kila la heri watani zangu.