Simba wamkataa Muharami kuwa kocha wake

Simba wamkataa Muharami kuwa kocha wake

Mocumentary

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
806
Reaction score
2,049
Uongozi wa Klabu ya Simba unaujulisha umma kuwa aliyekuwa Kocha wa makipa Muharami Said Mohammed maarufu 'Shilton', hakuwa muajiriwa wa klabu hiyo na wala hakuwa na mkataba na Simba.

Simba ilimuomba Muharami kuwanoa makipa wake kwa muda kwa mwezi mmoja, wakati huo klabu ikiendelea kutafuta Kocha wa kudumu.

Kwa mantiki hiyo klabu haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo na klabu iko tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika pindi itakapohitajika kwa maslahi ya Taifa.

Uongozi wa Simba unawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo.
 
Taarifa zilizonifikia hivi punde zinadai, uongozi wa Simba SC umekanusha Muharami Sultani kuwa kocha wake, taarifa inaeleza kwamba, Muharami aliombwa kuwa kocha kwa muda wa mwezi mmoja pekee huku Simba SC ikiendelea na mipango ya kutafuta kocha mpya.

Muharami anayetuhumiwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine akiwa na wenzake nane, bado anashikiliwa na mamlaka za nchi ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

FhmU6-7WIAAjN0s.jpg
 
IMG_1501.jpg

Uongozi wa Klabu ya Simba unaujulisha umma kuwa aliyekua Kocha wa magoli kipa Muharami Said Mohammed maarufu Shilton hakua muajiriwa wa klabu hiyo na wala hakua na mkataba na Simba.

Simba ilimuomba Muharami kuwanoa makipa wake kwa muda kwa mwezi mmoja, wakati huo klabu ikiendelea kutafuta Kocha wa kudumu.

Kwa mantiki hiyo klabu haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo na klabu iko tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika pindi itakapohitajika kwa maslahi ya Taifa.

Uongozi wa Simba unawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo.

===================

Mapema leo Novemba 15, 2022 Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya alitangaza kuwa Kocha huyo amekamatwa na watu wengine 9 wakiwa na Heroin kilo 34.

View attachment 2417476
 
View attachment 2417464

Uongozi wa Klabu ya Simba unaujulisha umma kuwa aliyekua Kocha wa magoli kipa Muharami Said Mohammed maarufu Shilton hakua muajiriwa wa klabu hiyo na wala hakua na mkataba na Simba.

Simba ilimuomba Muharami kuwanoa makipa wake kwa muda kwa mwezi mmoja, wakati huo klabu ikiendelea kutafuta Kocha wa kudumu.

Kwa mantiki hiyo klabu haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo na klabu iko tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika pindi itakapohitajika kwa maslahi ya Taifa.

Uongozi wa Simba unawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo.
Wamemkataa waliyemuomba kuwafundisha hao makipa..!! Kwani mkataba ni nini?

Simba waseme tu kwamba mzigo unawahusu, sema battery imechomoka ndo wanahaha
 
Kama ni hivi Mimi ni Mbumbumbu wa mikataba maana eti nilifundishwa kuna mkataba wa maandishi na mkataba wa maneno. Mwalimu yule Mburula akanambia eti mkataba si lazima uandikwe.
 
Sawa ila wajibu haya maswali.. kwanini hawakutoa taharifa kabla kuwa ni kocha wa muda.

Hata kama umemuomba afundishe kwa muda huyo tiyari ni mwajiriwa wako.

Na kama ni hivyo basi waandike barua kwa tume ya kudhibiti na kuzuia madawa ya kulevya yenye lengo la kuomba radhi kwa taasisi na club ya Simba FC kwa kumtuhumu kocha wa magolikipa anayedhaniwa ni mwajiriwa wa simba.
 
Upuuzi wa kiwango cha SGR, wabebe mzigo ni wao. Kama taasisi haiwezi kutokujua mienendo ya mtumishi wake.

Ngada fc
 
Huyo wa tume ya dawa za kulevya naye aliamua kuropka tu bila kujiridhisha kama huyo ni Muajiria wa Simba? anapaswa kuiomba radhi Simba na mashabiki wake kwa kusababisha usumbufu usio na sababu.
 
Watanzania sijui tuna shida gani. Sasa hii press reliease ina kanusha nini na inakubali nini.

'Simba ilimuomba na kukubaliana na Muharami kuwanoa makocha wetu ila sio mwajiriwa wetu'! Kumuomba mtu na kukuibaliana nae kufanya kitu fulani kwa malipo sio muajiriwa?

Ni bora wangesema ni muajiriwa wa muda

Watanzania kila kitu kubisha tu yaani, siasa siasa siasa kila mahali.

Kibusara ilitakiwa simba kuomba radhi kwa mtumishi wake kutuhumiwa hii kashfa alafu waoneshe kuwa hicho ni kitu personal na waoneshe kusikitika na kuahidi kumchukulia hatua akibainika, simple tu
 
Simba hawawezi kukwepa hii kashifa ni yao na mtuhumiwa anajulikana kama mtumishi wao. Kutoa ufafanuzi huu wakipuuzi nikuonesha walivyohaha. TAKUKURU NA TFF wafanye uchunguzi Kuna hatari kubwa Sana ya wachezaji wa simba kutumia madawa haya.

Pole ngada fc🤣🤣
 
Huyo wa tume ya dawa za kulevya naye aliamua kuropka tu bila kujiridhisha kama huyo ni Muajiria wa Simba? anapaswa kuiomba radhi Simba na mashabiki wake kwa kusababisha usumbufu usio na sababu.
Nawe unataka kuchemka!
 
Back
Top Bottom