Nina uhakika 💯 Simba hataleta timu
Vikao vya ndani vya Simba vimeshaamua kutokucheza Kwa sababu zifuatazo.
1. Kuonyesha msimamo wao.
Simba washataarifu umma kuwa hawatacheza tarehe ikibadilisha kutoka 15 June. Kucheza itaonyesha hawana msimamo
2. Simba wakikubali kucheza itaonyesha wamefuata matakwa ya a Yanga
Yanga walikuja na hoja nne na zote zimetekelezwa, na Sasa wana kampeni ya kumtoa Karia na Kidao pale TFF
3. Hamasa ndogo kuelekea derby Kwa upande Simba.
Yanga wamehamasika sana na wako tayari Kwa derby ila upande wa Simba wana ubaridi, hii ni ishara mbaya Kwa upande wa Simba kuwa wanaweza kupoteza mchezo Kwa mara ya 5 mfululizo
4 Simba wakipoteza derby watakuwa wamepoteza fungate lao la kufika CAFCC
Viongozi wa Simba washawafurahisha mbumbumbu wao Kwa kufika final ya CAFCC,Sasa endapo watapigwa derby na dalili zipo wazi kuwa watapoteza itafuta kila kitu msimu huu
5 Simba hata akikatwa alama 15 za kikanuni atakuwa nafasi ya pili.
Simba ana uhakika wa kushiriki CAFCL msimu ujao, hata kama taratibu zitafuatwa na akakatwa alama,
6. Tuzo binafsi za wachezaji
Simba Kwa Sasa ana top scorer Ahoua na goli keeper Bora. Mechi ya derby inaweza ikaamu vinginevyo,
Utashaanga hilo gap linazibwa siku ya derby, ila asipoleta timu, Yanga akapewa alama 3 na magoli 3, hayo magoli ni ya timu wala siyo ya mchezaji yoyote
Sasa Kwanini alete timu apigwe, atii matakwa ya Yanga na apoteze heshima aliyoijenga msimu mzima
View attachment 3377545