kilwakivinje
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 6,184
- 9,407
Kocha na mchezaji wa zamani wa Al Ahly,Mokhtar Mokhtar amesema kwenye michuano mipya ya African Football League,timu yao wanahofia mechi dhidi ya Mamelodi Sundowns ambao wanaweza kukutana nao nusu fainali na sio hii dhidi ya Simba katika hatua ya robo fainali
Mokhtar amesema Simba ndio wanatakiwa kuwa na hofu na sio wao kwani wasiwasi wao upo kwa Mamelodi Sundowns.
“Simba ndio wanatakiwa kuogopa kukutana na Al Ahly,ila mimi ninahofia kukutana na Mamelodi Sundowns”
“Al Ahly wana uwezo wa kuifunga timu yoyoye ndani ya Afrika, lakini mahesabu yetu siku zote hubadilika tukiwa tunaenda kukutana na Sundowns” Amezungumza Mokhtar kupitia mtandao wa Kingfut wa Misri.
Atakayeshinda mechi ya robo fainali ya Simba SC na Al Ahly,kwenye hatua ya nusu fainali atakutana na mshindi wa robo fainali ya Mamelodi Sundowns na Petro de Luanda ya Angola