Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
1. Usipoteze muda na Laban ni Chura mtiifu na sasa yupo dimbwini kashiba wadudu, kushindana naye kukoroma ni kujitafutia tatizo la kansa ya koo. Huu ni wakati wake. Yanga inafanya vizuri.Mkuu hakuna cha hasira wala nini. Tunachosema ni ukweli hapa hakuna ambae ameshafuzu kila timu bado ina nafasi.
Kama simba angefungwa zaidi ya goli Moja ningekwambia mwendo kaumaliza. Lakini kwa hilo goli Moja bado nafasi anayo iwapo atasahihisha nakosa yake.
Ulitegemea kwenye lile kombe la AFL simba atoe draw na Ahly kule cairo tena Ahly kutanguliwa kufungwa?
Tuziombee timu zetu zifuzu badala ya huu ushabiki usio na tija kwa taifa letu.
Daima mbele nyuma mwiko ,
#Simba nguvu Moja#
2. Acha unafiki. Hakuna timu zinaitwa timu zetu, timu yetu ni Taifa stars. Furaha ni kumuona mpinzani wako anaukosa ubingwa.
Unadhani Simba jina la mwakarobo tulijipa? Tumepewa na vyura na wanatamani mwaka huu walitumie tena.
Yanga ikibeba ubingwa itatembeza kombe mtaa kwa mtaa na Simba tutajifungia ndani kwa unyonge sana.
Hakuna sababu ya kuwa mnafiki kuwa shabiki wa Simba utaiombea Yanga ipite nusu fainali. Si kweli.