Mkuu unaweza kuwa upo sawa, Lakini je umetazama takwimu za mabao ya timu zote kwenye msimamo wa ligi?
Kama umetazama utaona kuwa Simba inawaacha wapinzani wake kwa mbali sana kwa wingi wa mabao!
Kwenye mechi ya jana Simba ilichanganya wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza na wengi wa kikosi cha pili, na hivyo timu ilikosa muunganiko mzuri hasa kwa kipindi cha kwanza japo kuingia kwa NYONI na BWALYA kulibadili sura ya mchezo. Na ninadhani kocha alifanya hivyo makusudi kutopanga kikosi cha kwanza ili kutoa nafasi ya mapumziko kwa nyota wengi wa kikosi cha kwanza , lakini pia kutoa nafasi kwa wachezaji wa benchi kupunguza vitambi kwakuwa kama ni ubingwa tushabeba!
Kwenye mechi na Yanga , Simba ilikuwa na kasoro 3 za kiufundi, Kwanza waliingia kwa kujiamini sana kuwa walikuwa na asiklimia kubwa sana ya kushinda katika mchezo ule, wakasahau kuwa wapinzani wao nao wameshawapania!
Pili Simba waliingiza kikosi kwa kuanza mabeki wengi badala ya kunoa foward, washinde kwanza ndio wazuie kulinda ushindi. Matokeo yake timu ilishindwa kupandisha mashambulizi mbele na kujikuta wakishambuliwa wao mfululizo hadi mashambulizi hayo yakazaa goli!
Washambuliaji walikosa utulivu kila walipofika langoni mwa wapinzani wao, mfano ni mashuti manne yaliyopigwa ndani ya 18 na wachezaji Medie Kagere, Luis Mikison na John Bocco!
Kama foward ingekuwa na utulivu walikuwa wa kushinda mchezo ule achilia mbali mauzauza ya marefa kuwanyima penati mbili za wazi!