Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Simba hawakunyimwa penalty yoyote acheni uongo bwana mechi ile mlipoteza kihalali kabisa.Mkuu unaweza kuwa upo sawa, Lakini je umetazama takwimu za mabao ya timu zote kwenye msimamo wa ligi?
Kama umetazama utaona kuwa Simba inawaacha wapinzani wake kwa mbali sana kwa wingi wa mabao!
Kwenye mechi ya jana Simba ilichanganya wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza na wengi wa kikosi cha pili, na hivyo timu ilikosa muunganiko mzuri hasa kwa kipindi cha kwanza japo kuingia kwa NYONI na BWALYA kulibadili sura ya mchezo. Na ninadhani kocha alifanya hivyo makusudi kutopanga kikosi cha kwanza ili kutoa nafasi ya mapumziko kwa nyota wengi wa kikosi cha kwanza , lakini pia kutoa nafasi kwa wachezaji wa benchi kupunguza vitambi kwakuwa kama ni ubingwa tushabeba!
Kwenye mechi na Yanga , Simba ilikuwa na kasoro 3 za kiufundi, Kwanza waliingia kwa kujiamini sana kuwa walikuwa na asiklimia kubwa sana ya kushinda katika mchezo ule, wakasahau kuwa wapinzani wao nao wameshawapania!
Pili Simba waliingiza kikosi kwa kuanza mabeki wengi badala ya kunoa foward, washinde kwanza ndio wazuie kulinda ushindi. Matokeo yake timu ilishindwa kupandisha mashambulizi mbele na kujikuta wakishambuliwa wao mfululizo hadi mashambulizi hayo yakazaa goli!
Washambuliaji walikosa utulivu kila walipofika langoni mwa wapinzani wao, mfano ni mashuti manne yaliyopigwa ndani ya 18 na wachezaji Medie Kagere, Luis Mikison na John Bocco!
Kama foward ingekuwa na utulivu walikuwa wa kushinda mchezo ule achilia mbali mauzauza ya marefa kuwanyima penati mbili za wazi!
SarcasmHiyo timu kweli ushambuliaji wake hauna nguvu. Hata ukicheki takwimu imeizidi Yanga kwa magoli machache sana ya kufunga. Goli 22 tu na Ameizidi Azam kwa goli 27 tu za kufunga.
Kwa jinsi ushambuliaji ulivyo dhaifu eti Simba amemzidi Mwadui kwa magoli 104 tu.
Timu hiyo iliyoishiwa kabisa mbinu za ufungaji eti ina tofauti ndogo sana ya magoli ya kufunga na kufungwa kiasi kwamba tofauti ya magoli yake inazidi tofauti ya timu 3 zinazomfuatia. Ana tofauti ya magoli 60 na timu tatu YANGA, Azam na biashara wana tofauti kwa jumla magoli 58.
Simba lazima afungwe tena Kigoma [emoji23][emoji23][emoji23]
Unaonaje tukupe hata timu ya Ihefu uifundishe, make inaonekana sana una mbinu bora sana kuliko hata professional coaches.Mkuu umemaliza kabisa. Ni kweli kabisa Simba ndiyo timu yenye viungo bora kabisa na washambuliaji wakali kuliko wote ligi kuu lakini tatizo lao kubwa ni mizaha, kudharau baadhi ya mechi, kukosa umakini, kuridhika wakishapata goli mbili/tatu na nidhamu ya ukabaji kuanzia mbele (pressing). Viungo wa Simba wanatengeneza kwa wastani nafasi za wazi zisizopungua kumi (kutegemeana na mechi) kwa washambuliaji wao katika kila mechi lakini zinazotumiwa kwa usahihi ni mbili mpaka tatu. Kila siku nasema iwapo benchi la ufundi la Simba wangekuwa wakali na washambuliaji wangekuwa makini basi Simba ingekuwa inatoka uwanjani na goli tano mpaka saba kwenye mechi moja. Mfano mdogo mechi ya Coastal Union Simba walishinda goli 2 - 0 kwenye mechi ambayo viungo wao waliwatengenezea nafasi zaidi ya nane ukiacha kabisa zile ambazo mshika kibendera alizozizuia kwa off side anazozijua yeye mwenyewe binafsi.
Wanosema Simba itapigwa tena Kigoma siwashangai kwa sababu matatizo makubwa ya Simba bado sijaona kama yamerekebishwa na nadhani Yanga walishayafanyia kazi katika mechi iliyopita na watayafanyia kazi tena mechi ijayo:-
1. Pasi fupi fupi kwenye eneo lao. Hatari yake ni kuwa adui akiunasa mpira basi ni majanga kwao. Kennedy Juma alizipiga hizi pasi mkaa zaidi ya tano na wachezaji Azam walizinasa lakini wakashindwa kuzitumia. Ila usitegemee kabisa Yanga wakazinasa hata tatu tu halafu wakose hata goli moja. Na kumbuka wakati Simba wanapiga hizi pasi fupi fupi kwenye eneo lao tayari Yanga wanakuwa wamesharudi wote nyuma kwenye goli lao kujipanga na kuwazuia Simba kwa urahisi halafu wanapiga "counter attack" kupitia kwa Kisinda.
2. Simba wanacheza taratibu sana hata pale wanapotakiwa kutumia kasi utaona bado wachezaji wao wanapakapaka mpira rangi bila sababu za msingi badala ya kufanya "counter attack". Wajifunze kucheza "direct football" kwenye baadhi ya mechi amabzao wanahitaji matokeo kwa nguvu. Katika mechi iliyopita dhidi Yanga Simba walikuwa wanatumia wastani wa pasi nane mpaka kumi kufika kwenye goli la Yanga wakati Yanga walikuwa wanatumia pasi tatu tu kufika kwenye goli la Simba. Faida ya kufikisha mpira kwenye goli la adui wako mapema mara nyingi inakuwa unamlaizimisha kufanya makosa kwa kuwa anakuwa bado hajajipanga.
3 Washambuliaji wa Simba kushindwa kukaba kuanzia mbele pale adui anaopukwa na mpira. Katika mechi iliyopita ilifika mahali Morison anatembea uwanjani wakati huo huo Mohamed Husein yupo kikaangoni anapigishwa jaramba na Tusila Kisinda.
4. "Back pass" hizi ndio ugonjwa mkubwa Simba. Katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga niliwashangaa sana viungo wa Simba pale ambapo benchi la ufundi lilipojilipua kwanza kwa kuingiza washambuliaji wawili halafu wakajilipua zaidi kwa kuingiza mshambuliaji wa tatu lakini bado wao walikiuwa wamelala wanapiga "back pass" nyingi tu wakati washamnbuliaji wanasubiri mipira mbele. Kwa mtindo ule hakukuwa na haja ya kuingiza washambuliaji wote watatu kwa pamoja.
5. "Spirit" ya mapambano. Hili nalo ni gonjwa sugu kwa Simba. Ukiwaangalia Yanga hawana wachezaji wazuri kama Simba lakini wao wanacheza kwa jasho, machozi na damu mpaka dakika ya mwisho. Wanajitolea na ni jihad kweli kweli wakati wenzao wa Simba wanacheza kifadha fadha kwenye mechi ya watani jadi kama vile wanacheza na Coastal.
6. Dharau. Simba waliidharau sana Yanga ndio maana ile "suprise" ya mpira wa kasi waliopiga Yanga ndani ya dakika 15 za mwanzo wachezaji wa Simba waliduwaa wasijue la kufanya na benchi la ufundi la Simba lilipigwa ganzi lisijue cha kufanya kujiokoa mpaka wakapigwa goli.
7. Kukosa umakini na papara kwa washumbuliaji wa Simba. Na hili bado halijarekebishwa kwani ukitazama mechi dhidi ya Coastal na dhidi ya Azam utaona hili tatizo bado lipo. Katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga washambuliaji wa Simba walikosa nafasi za wazi zaidi ya tatu kutokana na papara.
8. Washambuliaji wa pembeni. Wakati Yanga wanajua kutumia vizuri kasi yaTusila kutafutia matokeo wao Simba hawajui namna nzuri ya kutumia kasi ya Miquispne na Dilunga kutafutia matokeo.
Usiku wa deni haukawii kukucha tarehe 25 Julai sio mbali Simba wasipojirekebisha wakienda tena kucheza mpira badala ya kutafuta matokeo tu kama walivyofanya wenzao Yanga katika mchezo uliopita basi wasishangae tena yakawakuta kama yaliyowakuta kwa Mkapa.