Simba watakosea Kumpa Timu Dewji..

Simba watakosea Kumpa Timu Dewji..

Aliku
Sioni kama kuna shida yoyote kwani hakuna chochote anachokabidhiwa mtu bila kuwepo terms and condition za kisheria.Hivi vitu vitaenda kisheria na makubaliano ya kisheria lazima yawepo.

Hivi kwanini sisi ni waoga kwa mambo ambayo hayana msingi.

Kwa mantiki hii na kwa jambo dogo hivi hatuwezi kuendelea kwa lolote.

Kuthubutu kwetu ni kitu kisichowezekana,na tutashindwa kwa mengi kwa mtindo huu.
Naona mara hii ushasahau kilichotokea kwa Africa Lyon...
 
Napenda sana watu wanaofikiria kwa mtazamo Tofauti.

Kuna tatizo hapa
 
wakati rage akiwaita wanachama wa simba mbumbumbu wengi tuliona kawatukana ila ukweli aliwaambia ingawa hayupo.Wanachama walipaswa kuwaoji wakina Aveva kwanini wananshindwa kuipa timu mafanikio, kama tatizo ni pesa waelez vitega uchumi likiwemo jengo la msimbazi na mauzo ya jezi yanaenda wapi.Wanachama wengi wanamshabikia dewji kununua simba hisa 51% kwa bilioni 20 wakati hakuna chombo chochote kilichokaa na kuthibitisha thamani halisi ya simba ikiwa pamoja na fanbase yake.Wameshindwa kumuuliza dewji nini kilimshindwa afrika lyon mpaka akaiuza na je simba ikimshinda hatachukua maamuzi hayohayo.Dewji anatumia umbumbu wa wananchama wa simba kutekeleza malengo yake kama kweli anaipenda simba na yeye ni mwanachama mbona kikao cha jana hakuhudhuria?wanachama wameshindwa hata kuhoji taarifa ya fedha ingawa ilikuwa na mapungufu mengi kisa kudai timu auziwe dewji.wanabaki kulaumu wazee wa simba wakati hawajui wao ndio walianzisha hiyo timu na mpaka leo bado ipo.
Nachukia mikia fc, I love your logical reasoning. Thanks brother.
Kilichowazuzua watu hiyo figure, 20,000,000,000/=
 
Zama zimebalika. Timu zote zenye mafanikio Duniani zinatumia mtindo ambao Simba ndio wanataka kuutumia. Kilichopo Yanga ni tofauti kabisa na kitakacho fanywa na Simba. Natumaini Timu itakua bora kabisa
 
imenapa funzo kwamba tukija kuchonganisha na marekani tutauan kama kwenye ardhi ya gaddafi sisi ni kondokoo
 
Kuna watu wananufaika na ignorance ya wengi..simba wasipoangalia ndio utakua mwanzo wa mwisho wa timu...
We,kama we ni mojawapo ya wanaofaidika na huu uendeshaji wa timu kupitia ujanjaujanja mwisho wenu unakuja.Haiwezekani klabu yenye kila aina ya chanzo cha hela halafu wanashinda kutwa kupitisha bakuli,Hivi ww Simba ilipofikia ni ya kuchukua wachezaji kwa mkopo?Ni ya kufikia kutwa viongozi kusema Timu haina hela?Hebu tuache wivu WaTZ au labda ww ni wa upande wa pili!!!Timu iendeshwe kwa mfumo wa Hisa ila watu wajadili kwa kina,ikiwemo kutia mikataba Imara..Alaaaa!!!!
 
Aliku

Naona mara hii ushasahau kilichotokea kwa Africa Lyon...
Unajua stroke Dewji kweli ni mfanyabiashara na anapowekeza si kwamba anataka fedha yake iende bure au kutoa sadaka pesa ikaliwe.

Simba ina wapenzi wengi,ina washabiki wengi na ina base nzuri ya kuanzia.Amefanya projection ya kiasi gani atawekeza na itachukua mda gani kuanza kupata faida na timu ikajiendesha hapo hapo naye apate chake.

Kwa mtindo wa uendeshaji wa sasa,Simba haiwezi kupata maendeleo yoyote,italiwa na wanaotafuta fedha tu kisha tutaishia kufukuza wachezaji na makocha.

Unapata nini kwa uongozi wa sasa? Maana kama hufaidiki na lolote kimaslahi ni lazima utaunga mkono mabadiliko hayo..Kwa uongozi huu hatupati burudani wala maendeleo yoyote ya Club zaidi ya kero,maumivu na aibu mbele ya watani zetu.

Unafikiri ni kwanini Bosi wa Chelsie hakwenda kuanzisha Club yake,projection yake ilikuwa inakataa kulingana na muda aliojiwekea.

Hivi,huyo MO anakabidhiwa Club bila kuwa na masharti kadhaa iwapo atakiuka basi itakuwa vinginevyo?

Miaka 80 club haijui lini itamiliki uwanja wake,inashindwa na club kama Mwadui.

Mageuzi ni ya muhimu ila kwa uangalifu hasa kuhusu masharti.

Simba haina sababu ya kudhihakiwa kuwa inakula rambirambi za wachezaji,haina sababu ya kudhihakiwa kuwa inaleta wachezaji wasio na viwango hapa nchini kama wakina Kiongera kisha kulipwa fedha za bure,haina sababu ya kudhihakiwa inachukua fedha za wachezaji za usajili na mishahara,na wala haina sababu ya kudhihakiwa kuwa hailipi wachezaji inapovunja mikataba yao na kudanganya hasa katika mapato yao....nafikiri unakumbuka mambo ya kuwasili kwa fedha za Okwi na Samatta....ilileta sintofahamu kwa kuwa kuna SIRI sana na fedha zinaliwa sana.

Sasa kwa nini kurndelea na uongozi wa ubabaishaji wa namna hiyo.TUNATAKA UFANISI kwa UENDESHJI MPYA WA CLUB.
 
Simba watakua wanajirudisha nyuma miaka kadhaa kama watakubali kuruhusu Mohamed Dewji Achukue contol ya timu kwa asilimia kubwa.

Simba wamekua driven na kile kinachoonekana kama success kwa Yanga ambacho binafsi naona kama vile sio success bali ni safari kuelekea kuzimu kwa timu ya Yanga.

Simba wanaona Kwa yanga kushinda Ligi kuu na kushiriki nane bora ya Champions league kama mafanikio ya kuifanya Simba kutetereka na kuuza Asili yake.

Kinachoendelea Yanga ni kama furaha ya povu ambalo litapasuka muda wowote ikitokea mmfadhili wa sasa akaudhiwa.

Imeshawai tokea mara kadhaa miaka ya nyuma kuona wafadhili wa hizi timu wakizidump na kuleta taharuki kwa timu husika.

Vile vile sio mara ya kwanza kwa Dewji kua mfadhili wa Simba, alishawanfa hivyo na akabwaga manyanga yake.

Dewji huyu huyu baada ya kuudhiwa na Simba alianzisha timu yake ya Africa Lyon ambayo , kwa sasa hali yake haifahamiki kama imekufa au bado inaendelea kushiriki ligi mbali mbali.

Mpaka sasa sijasikia convincing argument toka kwa Dewji huyu wa sasa kujitofautisha na Dewji wa Zamani ili wana Simba wampe timu.

Waungwana wanasema " eperience is the best teacher" Hivyo nawausia wana Simba wenzangu kuwa makini na maamuzi yao, maana kuna dalili za kuja jutia huko mbele.

I stand to be corrected.
We unatakaje miaka 80 imepita sasa hakuna kusogea
 
Hio bil 20 hata GOODWILL ya simba pekee haitoshi, sembuse total market value ya Simba, huo ni mzaha mtupu
umejuaje? utafiti wa valuation ya thamani ta Simba ulifanyika lini?
 
Nasikia harufu kama ileeeeee ya YANGA ACADEMIA YANGA ASILI YANGA KAMPUNI ....vikinukia mtaa wa pili..... Yanga iliyumba sana kwa hivi vitu... Simba imeshayumba misimu mi4 sasa... Karata zinatakiwa zichangwe vizuri na Simba.....
 
Bajeti ya msimu ujao watani mapato na matumizi.... Hapo kuna pungufu karibia bilioni moja.... Inajazwaje !!??? Uwekezaji unahitajika ila uangalifu na umakini unahitajika kwa watani..... Ni hata nzuri yenye changamoto
 

Attachments

  • FB_IMG_1470055860744.jpg
    FB_IMG_1470055860744.jpg
    72.8 KB · Views: 30
Ninachojua Mimi hela ya magabacholi huwa haileti maendeleo
 
Nachukia mikia fc, I love your logical reasoning. Thanks brother.
Kilichowazuzua watu hiyo figure, 20,000,000,000/=
Kwa akili yako ndogo unaona hiyo ni kama 20000/=uwe unaona aibu hata kuiandika maana walizonazo hizo wanahesabika
 
Kwa akili yako ndogo unaona hiyo ni kama 20000/=uwe unaona aibu hata kuiandika maana walizonazo hizo wanahesabika
Hujaelewa hata mantiki ya comment yangu. Ndio wale waleee
 
Back
Top Bottom